Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Jamani hili jambo linanisikitisha na linaninyima raha hadi sasa.
Ni hivi miaka ya nyuma kidogo wakati nasoma nilianza kufuga Rasta hadi namaliza chuo nipo na Rasta zangu ndefu tu.
Nipo Nimeingia kitaa baada tu ya kutoka chuo nikaamua nipunguze wingi wa zile Rasta, yaani niwe na Rasta tano tu kichwani kwa hiyo ikabidi niunge unge zile Rasta kichwani ili zitoke tano, lengo la kufanya hivyo ni kupunguza wingi wa kuwa na rasta nyingi maana nilikuwa na Msitu haswa wa rasta.
Kwa hiyo nikawa na mikonga mitano ya nywele.
Miaka imepita nikaja kunyoa zile nywele kutokana sababu flani flani hivi. Basi baada ya hapo nakuja kutana na watu tofauti tofauti wa mtaani na wa familia wananipongeza kwa kukata nywele maana wanaambiwa nilikuwa mvutaji hodari wa bangi🤔🤔.
Leo kuna mtu tuliwahi fanya nae kazi enzi hizo nimekutana nae akaniambia hongera Bushmamy naamini sasa hivi huvuti mibangi yako kama zamani, nikamuuliza ushawahi niona navuta hiyo mibangi akasema ameambiwa hivyo ila yeye hajawahi niona.
Japo niliapa pale Kuwa ukweli wa Mungu sijawahi vuta Bangi lakini naona hakuamini na wala sikuhangaika naye maana silali na sili kwake ili nilitaka ajue kuwa watu wanajua kusema uongo.
Hata wazazi wangu hadi leo wanaamini hadi sasa napuliza.
Jamani kweli hiyo kitu. Sijawahi fanya kabisa nivip naweza waaminisha kuwa sijawahi hata shika hiyo kitu na mkono wangu, au niwapotezee?