Niwasimulie kisa cha Babu yangu aliyekuwa kama baba yangu

Mi ni first born,tumezaliwa wawili....miaka hiyo ya 90s baada ya mama kutalikiana na baba mzazi aliyeamua kumwoa mwanamke Mwingine na kumwingiza aishi nyumba moja na mama(dharau) ivo mama alishindwa aliamua kurudi home kwao tukuyu from magomeni mapipa DSM..... Watoto wawili,ivo akaona hatoweza kuanza maisha akiwa na watoto wote wawili....so Mimi nikaachwa kwa bibi na babu(ambaye ndo baba kwangu) nikiwa na three yrs old na kuja nichukua nikiwa na 11 yrs old maisha yake yaliposeto(yeye mama aniambiavyo maana nilikuwa nina muuliza kwann sasa na siyo vile nikiwa mdogo sana)

Story kuhusu babu sasa(baba yangu).....yeye ni mtoto wa malafyale(chifu) wa kinyakyusa,ivo wanaume wa kichifu enzi izo walikuwa wana tabia ya kuoa wake zaidi ya mmoja...so baba yake babu(nyanya yangu) kwa mke mkubwa alikuwa na watoto 10(wanawake enzi hizo walikuwa wanafyatua simbilisi akasome)....katika tembea tembea yake akampa mwanamke Mwingine ujauzito huko ivo kibusara ikabidi amshirikishe bi mkubwa kwamba anataka aongeze mke.....bi mkubwa akakataa katukatu...ivo babu alivyozaliwa akawa mtoto wa hawara

Miaka ikaenda watoto wote 11 yaan pamoja na babu wakawa watu wazima....babu(nyanya) aliwatafutia vitu vya kufanya ili waendelee kuishi na wake zao ila mtoto wa hawara(babu) bi mkubwa alikaza no kumwangaikia mbona ana mama yake na yupo peke yake ivo haitakuwa ngumu kumsaidia mwanae,na ni kweli mama wa babu yangu akaangaikiwa na ***** ivo badala ya kurithishwa shamba akarithishwa elimu ambapo akafanikiwa kuwa mgambo anaetambulika...eee bwana we kutambulika kwa kikosi chao kukawaponza,si akachaguliwa kushiriki vita ya kagera(1978) kama chambo vile(wale wanajeshi safisha njia wanaotangulizwa mbele) kiufupi walijua ndo imekula kwake lakini babu alirudi(sijui alijificha),ila alirudi na donda kisogoni but baadae alitibiwa alipona.

Kurudi kwa babu sasa ikawa kama amerudi kuja kumuaga baba yake mzazi...hatimaye malafyale(nyanya yangu) ukongwe ulikuwa umemwandama,akawa anaumwa bila kupona....siku ya kukata moto aliwaita watoto wake wote lakini cha ajabu waliitana wao tu 10 babu wakamwambia hapaswi hata kugusa mazingira Yale,wamekusanyana wasikie mzee anasemaje the last word...bwana bwana...si dingi akogoma siwez fumba macho kwa amani bila kumwona the last born (babu yangu sasa) ...akawhimiza mwiteni mwanangu,sijamlea,sijamtunza wala kumpa baraka zozote maishani mwake lakini bado Mungu anampigania....ikabidi wamwite kivivu ivoivo...akaingia chaupole wa watu...Kitendo cha kuingia tu baba yake akamwambia naomba unisamehe mwanangu ...sina cha kukupa ila naomba wewe ndo urithi home hapa,wewe ndiye utaongoza kaka zako na wanakijiji(balozi) .....nduguze na yeye pia wakahamaki....wanataka waanze kuwaka pale mzee akakata motoikawa imeisha iyo.

So after that babu akaanza kuishi pale(hadi sasa ndo tunapofikia kama kuna jambo...sanasana misiba)....maisha yakaendelee akapata mke akapata watoto 9(wote wako hai)mama yangu ni uzao wa nne kwake....lakini vita na ndugu zake haikukoma kutaka kumwondoa eneo lile kwamba hastahili...kumfukuza hawawezi ivo ikawa vita ya chinichini mpaka babu alipokufa wakati nduguze 8 wameshazikwa...then tukazika babu siku yake(ni msiba ambao nalia mpaka Leo,alitukusanya wajukuu 15 na alitulea bila ubaguzi).....Mungu amlaze mahali pema peponi chaupole....baba yangu kipenz,aliyenifundisha kulima,kufuga,kukamua ng'ombe maziwa,na vitu vingi vinavyonisaidia Leo hii

Daa,ndo ivo katika watoto 11 kabaki bibi mmoja tu ambae ni mzee sana,sana yaan.

Ndo ivo,karibuni Tukuyu wapendwa
Hata haieleweki...ungemsimulia mtu halafu umwombe akundikie. Yaani story ipo vululu vululu.
 
Aaaah, Pumbwafwu kabisa
Mie nikadhan Ma story ya kusisimua kama la UMUGHAKA
 
Mkuu mi sijaisoma ila nahisi itakua habari ya kuhudhunisha sana.Pole sana yataisha tuu.
 
Back
Top Bottom