Matukio ni mengi;
Nishawahi kuvua samaki wa mtoni na nikawala wakiwa wabichi vilevile.
Kuna siku nyingine njaa ilinipiga sana, nikawa napitapita sehemu usiku kama saa 6, nikasikia harufu ya mkate wa ngano unaiva, ikabidi niingie kwenye kale kajiko na nikaona mlango umeegeshwa tu, basi nikazama ndani.
Nilivyoingia ndani nikakuta kweli bwana mkate ndio unaiva ule mkaa wa juu ndio unazimazima, sasa kwa furaha niliyokuwa nayo ikabidi niimbe kidogo wimbo wa kikongo MUZINAAA. Sasa kumbe kuna jamaa anaitwa ...... na yeye alikuwa amezamia kwenye hicho kijiko na yeye alikuwa anasaka mkate sema alijificha alivyoona naingia alijua ni mwenye nyumba.
Kwa hiyo nilivyoimba Muzinaaa, nikashangaa mtu anaujibu wimbo huku anacheka. Basi pale tukaanza kupiga stori utafikiri tupo kwetu.
Jamaa alikuwa na sado ya togwa ya moto alisema kuna mahali amekwapua usiku uleule.
Sema mimi nilivyoshiba nikamwacha palepale manake nasikia alikuwa na kawaida ya kujisaidia haja kubwa kwenye majiko ya watu akishashiba menyu.