Njaa haina adabu, uliwahi kukamatwa na njaa kisawa sawa na uliituliza vipi ?

Njaa haina adabu, uliwahi kukamatwa na njaa kisawa sawa na uliituliza vipi ?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kuna watu wanakula mahindi ya kuchoma jioni kwa kuburidisha vinywa lakini kwa mwengine ni kwajili ya kuokoa maisha, njaa isikie tu.

Kuna kipindi njaa ilinipiga kwa siku inayokaribia ya pili bila kuweka chochote tumboni, nililegea sana ila nilijifanya nina nguvu nisichekwe na wenzangu, Nimeshakopa sana sina kwa kukopa na nimeshaomba sana, watu washanijua uchumi wangu upo mahututi.

kuna banda la karibu wanauzaga chips nilifika pale wakiwa wanafunga, nilichukua rambo fasta fasta nilibeba kabeji ile iliyokatwa katwa nikatoka nduki fastaaa..... Huo ndio ukawa msosi wangu na nikashiba.
 
Siku ya pili bila kula baada ya mgogoro mzito wa kifamilia. Hatimaye nilipata Tsh 300 muda huo utumbo unatetema, nikajitosa dukani kununua Boflo (andazi la Bakhresa) nikagawana mimi na mdogo wangu! Dah! [emoji24][emoji24][emoji24] (Nilikuwa mdogo, enzi hizo kidato cha tatu)
 
Matukio ni mengi;
Nishawahi kuvua samaki wa mtoni na nikawala wakiwa wabichi vilevile.

Kuna siku nyingine njaa ilinipiga sana, nikawa napitapita sehemu usiku kama saa 6, nikasikia harufu ya mkate wa ngano unaiva, ikabidi niingie kwenye kale kajiko na nikaona mlango umeegeshwa tu, basi nikazama ndani.

Nilivyoingia ndani nikakuta kweli bwana mkate ndio unaiva ule mkaa wa juu ndio unazimazima, sasa kwa furaha niliyokuwa nayo ikabidi niimbe kidogo wimbo wa kikongo MUZINAAA. Sasa kumbe kuna jamaa anaitwa ...... na yeye alikuwa amezamia kwenye hicho kijiko na yeye alikuwa anasaka mkate sema alijificha alivyoona naingia alijua ni mwenye nyumba.

Kwa hiyo nilivyoimba Muzinaaa, nikashangaa mtu anaujibu wimbo huku anacheka. Basi pale tukaanza kupiga stori utafikiri tupo kwetu.
Jamaa alikuwa na sado ya togwa ya moto alisema kuna mahali amekwapua usiku uleule.

Sema mimi nilivyoshiba nikamwacha palepale manake nasikia alikuwa na kawaida ya kujisaidia haja kubwa kwenye majiko ya watu akishashiba menyu.
 
😁😁😁😁😁😁
 
Siku moja nimepiga mapombe yangu kuanzia sa4 asubuhi hadi sa4 usiku sikula chochote sio kwamba nilikua sina hela sema akili za pombe zinaniambia, acha ujinga usile wewe umeshiba.
Basi bwana nikarudi kiotani kulala ile imefika sa8 natetemeka njaa jasho linatoka Dunia nzima nikajitahidi kuamka nikakata kachumbari ya nyanya mbili na vitungu vitano ndio vilivyoniokoa plus maji ya kunywa lita mbili.
 
Kuna wenzenu huko mtaa wa pili wana discuss chakula gani hawapendi na huko mtaa wa tatu wanajadili jinsi kuku wa KFC walivyo wabaya! JF world is wonderful!
Ila kwa kwwli mpka leo sielewi huyu jamaa wa kfc kawarogaje watu na hayo makuku yake. Aise uchawi wa wazungu ni nomaaa.

Yaani kweli mtu unaacha kuku choma safi kabisa unaenda kula kfc😲😲😲 sielewi
 
Back
Top Bottom