Njaa inanukia, mvua zimegoma. Serikali zuieni kuuza chakula nje ya Nchi

Tafuta pesa ndugu Vyakula vipo tu hata nje ya nchi vitakuja tu kupitia wafanyabiashara wao uangalia gap wapi kuna mahitaji achana na mambo ya misimu. Kariakoo matunda yote mwaka mzima unapata bila kujali msimu toka hadi nje ya nchi.
Wewe na sukuma gang wenzako ndio kutwa kucha kuanzisha vi thread uchwara kuponda Serikali..

Mwendazake alikuwa anafunga mipaka wakulima wakaishia kulia hovyo ..

Saizi Serikali imeachia biashara huru mazo yamepanda mumeanza kulinganisha bei wakati huo huo hamtaki Serikali izuie mazo kuuzwa nje kwa kisingizio cha kusema tafuta pesa.
 
Chakula kichache sana..maeneo mengi wamevuna kidogo..bado chakula kina toka nje ya nchi..unategemea nini kama sio kuanza kwa kelele za njaa kwa wananchi.

Inshu sio bei inshu ni chakula kichache mwaka huu.

#MaendeleoHayanaChama
Sure mwaka jana mda km huu uku nilipo mahindi debe kijijini ilikua 2500-3000 hila now uko kijijini ni 7000- 8000. Na hakuna dalili za kushuka. Mwaka huu na mwanzoni mwa mwaka 2023 kutakua na njaa kali sana
 
Sasa kama serikali imeachia mipaka si ndo vizuri hata msimu usipokuwa mzuri chakula si kitatoka nje
 
Msije kuanza kumlaumu Samia kwamba Bei zimepanda maana mna midomo Sana nyie.


Jiweke wewe kwenye nafasi ya Mkulima,

Uhangaike kulima kwa tabu uvune halafu mtu aje akupangie bei ya kuuza (bei ya hasara) na akupangie pa kuuza (locally) pia Kwa mkopo bila riba ?

Wakitaka wanunue kwa bei ya soko ya sasa ya ku export kabla bei haipanda hapo badae.
 
Yani wakati wa Mkulima anapouza mazao yake ndio mnaibuka washauri eti azuiwe asiuze nje ya mipaka ya nchi,

Je changamoto alizopata wakati wa kulima, kupalilia, kukuza, kuvuna, kusafisha, kutunza mlimsaidia ushauri?
 
Sure mwaka jana mda km huu uku nilipo mahindi debe kijijini ilikua 2500-3000 hila now uko kijijini ni 7000- 8000. Na hakuna dalili za kushuka. Mwaka huu na mwanzoni mwa mwaka 2023 kutakua na njaa kali sana
Mwaka jana mbolea ilikuwa 35,000 -60,000
Mwaka huu 2022 mbolea 66,000-110,000 unataka Bei ifanane ?unataka mkulima apate Hasara?
 
Jamani acheni roho mbaya.mnadhani wakulima wa nchi hii lini watapata nafuuu???mbolea wamenunua kwa bei kubwa mnooo halafu Leo ati wauze kwa bei ndogo.mipaka ifungwe ili wauze kwa bei kiduchu.dah plz ushindwe mtoa post
 
Jamani acheni roho mbaya.mnadhani wakulima wa nchi hii lini watapata nafuuu???mbolea wamenunua kwa bei kubwa mnooo halafu Leo ati wauze kwa bei ndogo.mipaka ifungwe ili wauze kwa bei kiduchu.dah plz ushindwe mtoa post
Wanaolaumu kwamba Bei zimepanda na kumlaumu Samia ni nani kama sio nyie mavivu wa Dar?
 
Serikali lazima ifanye regulation kwenye uzalishaji na biashara ya mazao ya chakula hasa nafaka ili kuepuka upungufu wa mazao ya chakula ndani ya nchi (acute food shortage), huwezi ukaacha tu watu wakajisafirishia mazao kwenda nje wanavyotaka kisa wanatafuta bei ya juu.....serikali inao wajibu na mamlaka kuzuia mazao ya vyakula muhimu kwa nchi hasa nafaka kwenda nje pale inapoona kuna ulazima huo.
 
Lengo liwe kumlinda mkulima na hapo hapo kulinda maslahi mapana ya taifa. Formula ni moja tu- serikali inunue nafaka ya mkulima kwa bei ya soko.
 
Wapi huko tuje kuwatembelea kama kunafikika.

Ndio maana wanamsema kuwa boss wako haijui nchi kwavile hajatembelea vijijini kazi yake kufika mji mkuu ya mkoa na wilayani lakini hajui huko vijijini kukoje!!! Na hivi mmejiongezea posho za safari za nje mtakuwa mnazuga kwenda makao makuu ya Mkoa na kufanya mkutano mmoja, mkirudi Dodoma/Dar. mnakaa siku mbili safari ULAYA!!!
Tembeleeni vijijini mjue kama barabara zinafikika au hazifikiki
 
Uchumi uko mjini,kijijini kufanya Nini?
 
Uchumi uko mjini,kijijini kufanya Nini?

Hicho chakula mnachosema wasiuze nje mnalima mjini? Washauri hao maboss wako wanunue chakula cha kutosha huko kwenye BOHARI YA CHAKULA badala ya kupoteza fedha kwenye safari zilizokuwa na tija!!
Safari za nje za serikali zimekuwa nyingi siku hizi kwasababu wasaidizi wa Hangaya wanafuata mfano wake kama ilivyokuwa enzi ya Vasco Dagama ; ndege zilizokuwa zinajaa watendaji wa serikali!!!
 
Bado ninakusikiliza mkuu!

Twende taratibu, tutafika tu!

Serikali kila siku inapiga kelele kuhusu "Sekta Binafsi".

Hivi inakuwaje hawa wakulima wetu vijijini huwa hatuwatambui kuwa sehemu ya sekta binafsi na kuwapa kipaumbele kinachostahiki?

Hili ni swali ambalo huwa nauliza mara kwa mara lakini huwa sipati jibu juu yake.

Kwani ni lazima awe mkulima mkubwa mwenye mahekta elfu, ndiyo tutambue kuwa ni 'sekta binafsi', kwa nini, sijui!

Nchi yetu, hasa katika hii miaka ya karibuni imekuwa na vipaumbele vya ajabu sana.

Sasa njaa ikija, labda ndipo akili zitatuingia kichwani.
 
mkulima anazidi kunyonywa tu kwani hao wanaosafirisha mazao nje ya nchi ni wafanyabiashara wakubwa.walinunua mazao wakati bei yake ilikuwa ndogo wakayahifadhi kwenye maghala na sasa wanayauze nje sababu yamepanda bei (speculation).kwa hali hiyo mwananchi kabaki kama alivyo na umaskini wake.serikali iwasaidie wakulima waweze kuuza mazao yao kwa bei nzuri ambayo inampa faida ili aweze kuzalisha tena kwa tia.
 

Ni vigumu serikali ambayo ina ushirika na wafanyabiashara[ So called private sector] kuweza kuwasaidia wakulima kwasababu faida za hao wafanyabiashara zinatokana na kuwanyonya wakulima!!
 
Serikali chukueni ya kuzuia uuzaji wa chakula nje ya Nchi mapema,Chad yatangaza Hali ya hatari kutokana na njaa 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220603-141544.png
    132.8 KB · Views: 8
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…