Wakuu,
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeshiriki moja kwa moja katika mauaji ya halaiki ya Watanganyika zaidi ya 2,000, yaliyotekelezwa kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na askari wa kukodi (mercenaries) waliotoka Uganda na Zanzibar, katika kipindi cha uchaguzi mkuu kuanzia tarehe 29. Cha kushangaza ni kwamba, serikali na viongozi wake wamekataa kuwajibika kwa mauaji haya ya kikatili. Badala yake, wameamua kuwafungulia Watanganyika na viongozi wa chama cha siasa CHADEMA kesi za kutungwa za uhaini na ugaidi, huku wakiepuka kuwajibika kwa uhalifu wao wenyewe.
Inaonekana wazi kuwa kuna njama za kupotosha ukweli na kuwatupia wananchi lawama kwa makosa ambayo serikali yenyewe imeyafanya. Hivi sasa, mjadala mitaani umeelekezwa katika kesi hizi za uongo badala ya kujadili tukio kubwa na la kusikitisha la mauaji ya halaiki yaliyotekelezwa kwa maelekezo ya viongozi wa serikali.
Ikumbukwe kuwa zaidi ya miaka 2,000 iliyopita, Kaisari dhalimu Nero wa Dola ya Kirumi aliwahi kuuchoma moto mji wa Roma. Badala ya kuwajibika kwa kitendo hicho, aligeuza kibao na kuwasingizia Wakristo kuwa wao ndio walioufanya uhalifu huo, jambo lililopelekea mauaji ya kikatili ya maelfu ya Wakristo wasio na hatia.
Hali tunayoshuhudia sasa ni taswira ile ile: serikali inajaribu kuwatupia Watanganyika lawama kwa mauaji ambayo ilishiriki moja kwa moja kuyapanga na kuyatekeleza.
Shitukeni Watanganyika! Tusiupoteze mwelekeo kwa kufuata kesi hizi za kutungwa. Wanasheria waendelee kutoa msaada wa kisheria kwa wote walioshtakiwa kwa uonevu, lakini sisi sote tuendelee kupaza sauti bila kuchoka. Serikali lazima iwajibike kwa mauaji haya ya halaiki.
Mauaji haya yataendelea kukumbukwa na kuandikwa katika vitabu vya historia ya Tanganyika hadi siku wale wote waliopanga na kushiriki wawajibishwe ipasavyo.