Tetesi: Njama za kuwavua Uwakili waliofungua kesi kupinga Mkataba wa Milele wa Bandari zavuja ni kama ile iliyomkuta Fatuma Karume

Tetesi: Njama za kuwavua Uwakili waliofungua kesi kupinga Mkataba wa Milele wa Bandari zavuja ni kama ile iliyomkuta Fatuma Karume

Taarifa ya Wakili Msomi Alphonce Lusako inadokeza kwamba zipo njama za kuhujumu Mawakili waliopeleka kesi ya Mkataba wa kitumwa wa Bandari Mahakamani.

Mbinu iliyotumika kumhujumu Wakili Fatuma Karume ndio iliyopendekezwa kutumika kuwashughulikia hawa wengine.

Bali Alphonce Lusako ametahadharisha kwamba hata wakihujumu baadhi yao bado kuna Mawakili zaidi ya 67 wanaosimamia Kesi hiyo .

Tutaendelea kufichua kila njama zinazopangwa na Mamluki dhidi ya Wazalendo .

Usiondoke JF
Wameanza kulialia baada ya kuona wameshindwa kabla hata ya kesi kuanza. Waliifungua kw amihemko ya wanaharakati bila facts. Ndo mana hata akina tundu lisu hawezi kuthubutu kwenda mahakamani kujidhalilisha mana wanajua wanapiga Domo to kitu ambacho hakipo.

Wameanza kulialia ili waonewe huruma baada ya kuona kesi ni ngumu. Na Bado kangaroo court inawahusu.

Vijana achaneni na mihemko bila facts za kutosha.akina lisu na akina slaa wanawapoteza. Jiulizeni kwa Nini wao hawaendi mahakamani? Wanajua kwamba wanapiga Domo tu to keep the ball rolling.
 
Wa Tz tusali sana kuomba msaada wa Mungu.
Kwani inawezekana tunaona tunapambana na binadamu wenzetu kumbe tunapambana na mashetani!
 
Umezidiwa hoja kabisa. Kwani kulewa ni kosa kisheria? Serkali si inachukua kodi kwa vileo?
Iweke orodha ya walevi kutoka kwenu na clip zao? Wengine wakiwa bungeni au kwenye mikutano?
Nyie kweli ni mangedere, mnatumia huu uzushi wenu km defence mechanism, nyie kweli vilaza hizo ni mbinu za kitoto. Tii sheria bila shuruti hakuna mwenye muda na kima km hao hawana madhara yoyote waropokaji wazushi tu na wanaeleweka
 
Hapo hapana. Ninamfahamu vizuri sana huyu Mwabukusi. Ninatoka kijiji kimoja na Mwabukusi. Ninalijua shina la ukoo wake. Siyo mlevi kama ulivyoandika. Ni dhambi unajitafutia bila sababu ya maana. Kama Mwabukusi amekuzidi hoja, jipange kwanza then urudi hapa kujibu hoja za Mwabukusi.
Aisee...
Wanamsingizia sababu ya msimamo wake...
JAMBO JEMA HALIHITAJI NGUVU NYINGI..
 
Fatuma Karume hatuhusu ni mzanzibar hatuhusu wanaotuhusu ni watanganyika kwanza hata swala la bandari amekuwa kimya.
 
Taarifa ya Wakili Msomi Alphonce Lusako inadokeza kwamba zipo njama za kuhujumu Mawakili waliopeleka kesi ya Mkataba wa kitumwa wa Bandari Mahakamani.

Mbinu iliyotumika kumhujumu Wakili Fatuma Karume ndio iliyopendekezwa kutumika kuwashughulikia hawa wengine.

Bali Alphonce Lusako ametahadharisha kwamba hata wakihujumu baadhi yao bado kuna Mawakili zaidi ya 67 wanaosimamia Kesi hiyo .

Tutaendelea kufichua kila njama zinazopangwa na Mamluki dhidi ya Wazalendo .

Usiondoke JF
Na leo yametimia.... laana na iwafikie na kizazi chao haya majizi
 
Back
Top Bottom