Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Mkuu Mabandiko gani yenye chuki kwa wazanzibar?Mkandara;10030375]Mabandiko yako yote yanahusu chuki zako kwa Wazanzibar na CCM kiasi kwamba unashindwa kuelewa hata makosa mnayofanya na upande wako na ndicho nachozungumzia pasipo upendeleo. Utawachukia vipi Wazanzibar hawa wakati upo nao UKAWA? Kisha unadai Utanganyika wakati hawa hawa ndio wanaotukana hadi Muasisi wa Uhuru wako! Utanganyika upi unaotetea wewe kama sii kipofu alomshika tembo mkia. Mimi nasimama kama mimi au mwananchi, kwa kila hoja huchanganya na za kwangu sifuati mkumbo wa chama wala mtu mwingine. Mtu wangu akifanya makosa ama ujinga
Hapo juu umetaka kuingiza mambo ya udini, sasa unanisingizia chuki kwa wazanzibar.
Hujaeleza chuki gani niliyo nayo kwa waznz. Mkuu hebu rudi katika mstari ule wa Mkandara.
Ninafahamu hoja zangu ni nzito na kwa upungufu wa majibu unaingiza mambo ya dini na kusingizia chuki.
Onyesha wapi nilipo na chuki nao, otherwise jazaba na flip flops hazijibu hoja. Sisi tutaongelea hoja na si nje ya hapo.
Wazanzibar wengi wanataka kuvunja muungano(ingawa wameshavunja), Mkataba, serikali 3.
Hawataki S2 au Moja. Zaidi ya miaka 5 nyuma nimesimamia Tanganyika nikiwaunga mkono wznz kuwa na mamlaka kamili.
Hivi hapo mimi nawewe nani mwenye chuki?
Wewe unayewalazimisha ukisema 'watapata hasara'' au mimi ninayeheshimu maamuzi yao?
Kuhusu kuzungumza,naongea kama mwananchi haswa.
Nimeanza kuandika kuhusu Tanganyika, UKAWA hawajachaguliwa.
Nimewaonya sana wazanzibar kabla ya rasimu ya kwanza.
Nikuonyeshe kuwa hatubahatishi na wala hatuna chuki soma habari hii hapa chini.
Huu 'utunzi kama anavyouita Mkandara'' uliandikwa na Nguruvi3 kabla ya kuanzishwa Mchakato, kuundwa kwa tume ya Warioba au UKAWA . Wananchi tuliona haya.Nguruvi3;HOJA YA MUUNGANO: ZANZIBAR INACHEZA KARATA MBOVU
Mabadiko # 98 na 99 tumeongelea vugu vugu linaloendelea la muungano.
Tulisema nia kubwa ya Zanzibar si kuvunja muungano kama wanavyotaka baadhi yao iwe.
Wao wanataka kuwepo na serikali 3, mkataba au uhusiano maalum.
Kwa hakika wameshindwa kuwashawishi Watanzania bara kwanini tuwe na vitu hivyo kama tulivyoeleza huko myuma.
Kikao vya BLW na Bunge vinaendelea na tunaona cheche hasa BLW.
Ni mwakilishi mmoja au wawili walisema hawataki muungano hadharani.
Kikubwa tunachosubiri ni kusikia wabunge kutoka Zanzibar wakiukataa muungano.
Hilo halitatokea kwasababu Zanzibar inautaka muungano kuliko inavyodhaniwa.
Wao wanataka nchi yao na baadhi ya huduma, gharama na shughuli za kijamii zihudumiwe na Tanganyika.
Turudi kwenye hoja yao mpya ambayo ni kutaka Serikali ya Tanganyika irudi kwanza ili Zanzibar ikae na Tanganyika kama washirika wa muungano.
Wanachotaka ni mambo yale matatu kwa maana kuwa uwepo wa Tanganyika na Zanzibar kama nchi mbili utazaa serikali ya muungano. Hapa tayari ni serikali 3 kama wanavyotaka kila mara. Mambo yatakyokuwemo katika serikali ya shirikisho ndio mkataba wanaoutaka, na uwepo wa mkataba ndio ushirikiano maalumu wanaousema.
Kurudi kwa Tanganyika kwao ni sawa na hoja ya serikali 3.
Tanganyika itakuwa serikali huru yenye mamlaka yake kama ilivyo Zanzibar.
Itakuwa na mihimili ya dola kamili. Zaidi ya hapo itakuwa na Vyombo vya usalama na ulinzi na hakika kiuchumi na kijamii itakuwa mbali sana ya Zanzibar. Kwahiyo serikali ya Tanganyika haitaihitaji ZNZ na itakuwa kinyume chake.
Serikali ya Tanganyika itadai ushiriki sawa na mbia mwenza Zanzibar.
Mathalani ikiamuliwa kuwa Jeshi liwe la pamoja kama sehemu ya muungano, Tanganyika itauliza Mchango wa Zbar ni nini katika kuliendesha hilo jeshi?
Na kukosekana kwa wazanzibar katika jeshi kutaathiri vipi jeshi la Tanganyika?
Mchango wa ZNZ ni nini katika kuhudumia serikali ya muungano kama mbia?
Kwa maneno mengine kwa vile Tanganyika itakuwa nchi huru kama Zanzibar na zimeungana kila moja itataka kulinda masilahi ya wananchi wake na haitakubali kuhudumia serikali nyingine bila sababu. Hoja hapa ni kuwa hakuna mdogo wala mkubwa,sasa kuleana kutaanzia wapi?
Zanzibar ikitaka mkataba, serikali 3 au mahusiano Tanganyika itatanguliza mwaswali yafuatayo;
1. Kwanini tunaihitaji kuwa na mahusiano ya aina yoyote na Zanzibar?
2. Tunafaidika na nini katika mahusiano hayo
3. Nini mchango wa Zanzibar katika mahusiano
4. Tanganyika itaathirika nini bila uwepo wa Zanzibar au mahusiano
Tanganyika haitakuwa tayari kuumia kwasababu ya mbia mwenza.
Ikitokea Zanzibar na Tanganyika zikaamua kuwa na mahusiano mengine nje ya serikali 3, hicho kitakuwa kitanzi kwa Wazanzibar.
Mathalani, wakiamua kuweka mkataba wa ajira, Tanganyika itadai haki ya ajira ZNZ kama ZNZ inavyofanya.
Zanzibar ikiweka sheria za ardhi, Tanganyika itakuwa na haki ya kuweka zake n.k.
Huko nyuma ZNZ walikuwa na sheria za Mtangayika kwenda na Passport.
Tanganyika ilipodai nao waje na passport ilichukua wiki mbili ZNZ wakafuta passport na ikawa ndio mwisho na wala hilo hulisikii tena.
Wamedai bendera, wimbo n.j lakini husikii wakidai passport, bado wanatumia ya kijani kwasababu kinyume chake ni maumivu makali.Huu ndio mfano mzuri wa kuashiria nini kitatokea. Itakuwa ni nipe nikupe na siyo nikupe.
Kwa mantiki hiyo uwepo wa Tanganyika utafuta matumaini ya serikali 3, mkataba, au mahusiano maalumu kwasababu moja muhimu, Tanganyika itakuwa na dola isiyoyohitaji Zanzibar na kila hoja itakapokuja itakumbuna na swali moja'
'' Ili iweje na iwe nini na kwa faida gani''
Hapa ndipo nasema ZNZ iendelee na harakati za kujitoa katika muungano ambazo zinaungwa mkono na Watanganyika.
Kinyume chake mbinu zinazofikiriwa zitaiwezesha Zanzibar kunufaika kama ilivyo sasa hazifai na hazitakubalika.
Vurugu za Zanzibar zimewafungua macho Watanganyika na kuona jinsi gani ukarimu na fadhila zao kwa ndugu zao unavyokuwa shuburi.
Ni kwa muktadha huo, serikali 3, mahusiano, mkataba au kurudi kwanza kwa Tanganyika hakutaisadia ZNZ kwa namna yoyote. Wenye lugha zao wanasema ZNZ imefungua 'can of worms' sasa tusiburi tu.
Nami nasema hii ni karata mbovu sana na inazidi kuiweka znz katika wakati mzuri wa kujitoa na si vinginevyoTusemezane
Utunzi huu unasimama wenyewe na thamani yake kama ilivyokuwa miaka kbala ya UKAWA au Warioba na tume.
Kahiyo sisi tunaongozwa na akili hatuongozwi na hisisa hisia au mashaka au hofu. T
tunaongozwa na fikra, hatuandiki utunzi tukiweka akili zetu rehani kwenye udini.
Tunaongozwa na fikra na mantiki na siyo WENGI WAPE.
Mkandara na leo narudia kusema wazn wamefungua can of worms.
Kilichopelekea hilo ni elimu ndogo . Leo Mdondoaji na takashi wapo wapi?
eo tunwaambia bila shaka hatuwahitaji hata kwa bahati mbaya na hawana la kusema, wanufyata tu. Njia nyeupee hawana la kujibu
Muungano ni kuwasidia wao hawatusaidii lolote na wala hakuna prospect za mzanzibar kutusaidia jinsi alivyojaa chuki na husuda kwa Mtanganyika. Ni ukweli huo Mkandara. Nani anakupenda akuchome moto! Si wamechoma Watanganyika moto, lini umesikia sisi tumewatia vibiriti.
Nitakufafanulia kwanini elimu yao ni ndogo sana, lakini kwanza tafakari hapo ili uone kuwa tunaona miaka 4 minne au mitano mbele. Hatusombwi na hisia hisia za kusilimu au kubatizwa. Huko hatupo kwasababu ni eneo la watu wasio na hoja. Period.