Nje ya Bunge hakuna Katiba ya Wananchi

Nje ya Bunge hakuna Katiba ya Wananchi

Mkandara;10030375]Mabandiko yako yote yanahusu chuki zako kwa Wazanzibar na CCM kiasi kwamba unashindwa kuelewa hata makosa mnayofanya na upande wako na ndicho nachozungumzia pasipo upendeleo. Utawachukia vipi Wazanzibar hawa wakati upo nao UKAWA? Kisha unadai Utanganyika wakati hawa hawa ndio wanaotukana hadi Muasisi wa Uhuru wako! Utanganyika upi unaotetea wewe kama sii kipofu alomshika tembo mkia. Mimi nasimama kama mimi au mwananchi, kwa kila hoja huchanganya na za kwangu sifuati mkumbo wa chama wala mtu mwingine. Mtu wangu akifanya makosa ama ujinga
Mkuu Mabandiko gani yenye chuki kwa wazanzibar?

Hapo juu umetaka kuingiza mambo ya udini, sasa unanisingizia chuki kwa wazanzibar.
Hujaeleza chuki gani niliyo nayo kwa waznz. Mkuu hebu rudi katika mstari ule wa Mkandara.

Ninafahamu hoja zangu ni nzito na kwa upungufu wa majibu unaingiza mambo ya dini na kusingizia chuki.
Onyesha wapi nilipo na chuki nao, otherwise jazaba na flip flops hazijibu hoja. Sisi tutaongelea hoja na si nje ya hapo.

Wazanzibar wengi wanataka kuvunja muungano(ingawa wameshavunja), Mkataba, serikali 3.

Hawataki S2 au Moja. Zaidi ya miaka 5 nyuma nimesimamia Tanganyika nikiwaunga mkono wznz kuwa na mamlaka kamili.
Hivi hapo mimi nawewe nani mwenye chuki?

Wewe unayewalazimisha ukisema 'watapata hasara'' au mimi ninayeheshimu maamuzi yao?

Kuhusu kuzungumza,naongea kama mwananchi haswa.

Nimeanza kuandika kuhusu Tanganyika, UKAWA hawajachaguliwa.

Nimewaonya sana wazanzibar kabla ya rasimu ya kwanza.
Nikuonyeshe kuwa hatubahatishi na wala hatuna chuki soma habari hii hapa chini.

Nguruvi3;HOJA YA MUUNGANO: ZANZIBAR INACHEZA KARATA MBOVU

Mabadiko # 98 na 99 tumeongelea vugu vugu linaloendelea la muungano.
Tulisema nia kubwa ya Zanzibar si kuvunja muungano kama wanavyotaka baadhi yao iwe.

Wao wanataka kuwepo na serikali 3, mkataba au uhusiano maalum.
Kwa hakika wameshindwa kuwashawishi Watanzania bara kwanini tuwe na vitu hivyo kama tulivyoeleza huko myuma.

Kikao vya BLW na Bunge vinaendelea na tunaona cheche hasa BLW.
Ni mwakilishi mmoja au wawili walisema hawataki muungano hadharani.
Kikubwa tunachosubiri ni kusikia wabunge kutoka Zanzibar wakiukataa muungano.

Hilo halitatokea kwasababu Zanzibar inautaka muungano kuliko inavyodhaniwa.
Wao wanataka nchi yao na baadhi ya huduma, gharama na shughuli za kijamii zihudumiwe na Tanganyika.

Turudi kwenye hoja yao mpya ambayo ni kutaka Serikali ya Tanganyika irudi kwanza ili Zanzibar ikae na Tanganyika kama washirika wa muungano.

Wanachotaka ni mambo yale matatu kwa maana kuwa uwepo wa Tanganyika na Zanzibar kama nchi mbili utazaa serikali ya muungano. Hapa tayari ni serikali 3 kama wanavyotaka kila mara. Mambo yatakyokuwemo katika serikali ya shirikisho ndio mkataba wanaoutaka, na uwepo wa mkataba ndio ushirikiano maalumu wanaousema.
Kurudi kwa Tanganyika kwao ni sawa na hoja ya serikali 3.

Tanganyika itakuwa serikali huru yenye mamlaka yake kama ilivyo Zanzibar.
Itakuwa na mihimili ya dola kamili. Zaidi ya hapo itakuwa na Vyombo vya usalama na ulinzi na hakika kiuchumi na kijamii itakuwa mbali sana ya Zanzibar. Kwahiyo serikali ya Tanganyika haitaihitaji ZNZ na itakuwa kinyume chake.

Serikali ya Tanganyika itadai ushiriki sawa na mbia mwenza Zanzibar.
Mathalani ikiamuliwa kuwa Jeshi liwe la pamoja kama sehemu ya muungano, Tanganyika itauliza Mchango wa Zbar ni nini katika kuliendesha hilo jeshi?

Na kukosekana kwa wazanzibar katika jeshi kutaathiri vipi jeshi la Tanganyika?
Mchango wa ZNZ ni nini katika kuhudumia serikali ya muungano kama mbia?

Kwa maneno mengine kwa vile Tanganyika itakuwa nchi huru kama Zanzibar na zimeungana kila moja itataka kulinda masilahi ya wananchi wake na haitakubali kuhudumia serikali nyingine bila sababu. Hoja hapa ni kuwa hakuna mdogo wala mkubwa,sasa kuleana kutaanzia wapi?

Zanzibar ikitaka mkataba, serikali 3 au mahusiano Tanganyika itatanguliza mwaswali yafuatayo;

1. Kwanini tunaihitaji kuwa na mahusiano ya aina yoyote na Zanzibar?
2. Tunafaidika na nini katika mahusiano hayo
3. Nini mchango wa Zanzibar katika mahusiano
4. Tanganyika itaathirika nini bila uwepo wa Zanzibar au mahusiano

Tanganyika haitakuwa tayari kuumia kwasababu ya mbia mwenza.
Ikitokea Zanzibar na Tanganyika zikaamua kuwa na mahusiano mengine nje ya serikali 3, hicho kitakuwa kitanzi kwa Wazanzibar.

Mathalani, wakiamua kuweka mkataba wa ajira, Tanganyika itadai haki ya ajira ZNZ kama ZNZ inavyofanya.
Zanzibar ikiweka sheria za ardhi, Tanganyika itakuwa na haki ya kuweka zake n.k.

Huko nyuma ZNZ walikuwa na sheria za Mtangayika kwenda na Passport.
Tanganyika ilipodai nao waje na passport ilichukua wiki mbili ZNZ wakafuta passport na ikawa ndio mwisho na wala hilo hulisikii tena.

Wamedai bendera, wimbo n.j lakini husikii wakidai passport, bado wanatumia ya kijani kwasababu kinyume chake ni maumivu makali.Huu ndio mfano mzuri wa kuashiria nini kitatokea. Itakuwa ni nipe nikupe na siyo nikupe.

Kwa mantiki hiyo uwepo wa Tanganyika utafuta matumaini ya serikali 3, mkataba, au mahusiano maalumu kwasababu moja muhimu, Tanganyika itakuwa na dola isiyoyohitaji Zanzibar na kila hoja itakapokuja itakumbuna na swali moja'
'' Ili iweje na iwe nini na kwa faida gani''

Hapa ndipo nasema ZNZ iendelee na harakati za kujitoa katika muungano ambazo zinaungwa mkono na Watanganyika.
Kinyume chake mbinu zinazofikiriwa zitaiwezesha Zanzibar kunufaika kama ilivyo sasa hazifai na hazitakubalika.

Vurugu za Zanzibar zimewafungua macho Watanganyika na kuona jinsi gani ukarimu na fadhila zao kwa ndugu zao unavyokuwa shuburi.

Ni kwa muktadha huo, serikali 3, mahusiano, mkataba au kurudi kwanza kwa Tanganyika hakutaisadia ZNZ kwa namna yoyote. Wenye lugha zao wanasema ZNZ imefungua 'can of worms' sasa tusiburi tu.
Nami nasema hii ni karata mbovu sana na inazidi kuiweka znz katika wakati mzuri wa kujitoa na si vinginevyoTusemezane
Huu 'utunzi kama anavyouita Mkandara'' uliandikwa na Nguruvi3 kabla ya kuanzishwa Mchakato, kuundwa kwa tume ya Warioba au UKAWA . Wananchi tuliona haya.

Utunzi huu unasimama wenyewe na thamani yake kama ilivyokuwa miaka kbala ya UKAWA au Warioba na tume.

Kahiyo sisi tunaongozwa na akili hatuongozwi na hisisa hisia au mashaka au hofu. T
tunaongozwa na fikra, hatuandiki utunzi tukiweka akili zetu rehani kwenye udini.
Tunaongozwa na fikra na mantiki na siyo WENGI WAPE.

Mkandara na leo narudia kusema wazn wamefungua can of worms.

Kilichopelekea hilo ni elimu ndogo . Leo Mdondoaji na takashi wapo wapi?
eo tunwaambia bila shaka hatuwahitaji hata kwa bahati mbaya na hawana la kusema, wanufyata tu. Njia nyeupee hawana la kujibu

Muungano ni kuwasidia wao hawatusaidii lolote na wala hakuna prospect za mzanzibar kutusaidia jinsi alivyojaa chuki na husuda kwa Mtanganyika. Ni ukweli huo Mkandara. Nani anakupenda akuchome moto! Si wamechoma Watanganyika moto, lini umesikia sisi tumewatia vibiriti.

Nitakufafanulia kwanini elimu yao ni ndogo sana, lakini kwanza tafakari hapo ili uone kuwa tunaona miaka 4 minne au mitano mbele. Hatusombwi na hisia hisia za kusilimu au kubatizwa. Huko hatupo kwasababu ni eneo la watu wasio na hoja. Period.
 
Mkandara;10030375] Mimi nimesema haya kwa kuonyesha wewe mtunzi mzuri wa hekaya kwa sababu umeingia hadi ndani ya rasimu ya CCM imeandaliwa vipi kana kwamba ulikuwepo wakati hakuna mahala popote CCM wameeleza hayo
Ulitegemea CCM waonyeshe mbinu zao!!!
Ya Lowassa na Nyerere yanazungumziwa kutokana na habari iliyotolewa lakini hakuna mtu alosema nani aliandaa faili la EL na lilikuwa wapi...Ndio maana nasema wewe mtunzi mzuri wa riwaya
Ukiacha mimi, wapo watunzi wengi wameliongelea hili kuanzia magazetini na hata sasa.
Ule utajiri wa EL aliohoji Nyerere EL kautolea ufafanuzi robo juzi na bado unahojiwa. Kazi za watunzi hufanana
Huu ni upuuzi mwingine ..mkuu wangu unashindwa kutazama impact ya sera mbovu na kuilalamikia CCM na utawala wake wa miaka 50 imeshindwa mnasingizia Muungano na Wazanzibar.Hivi Uhuru wetu ulilenga kuunganisha nchi ngapi?
Hapana Mkuu, huna sababu ya kutukana, unaeleweka tu kwa kuandika kawaida.
Litendee jukwaa haki na umri unakuzuia.

Utasemaje umeona haraka za uhuru kama huwezi kuona tusi uliloandika Mkuu. I
nshallah, pumua kidogo ili tuendelee..Bandiko lilipoita umesema nina chuki na CCM, vipi wewe mwenye mapenzi leo uone sera zao mbovu?
I mean huu ni ujinga mkuu wangu, kama kuna failure zozote za maendeleo nchini basi ni CCM walotukwamisha! ni CCM wa kulaumiwa na kutowapa nafasi tena ya kuongoza nchi.
Mbona mimi nikisema haya maneno unasema nina chuki na CCM!!!!
Iwe tuna serikali za nchi 2, au 3, tuwe na mikoa 17 au 30 ni CCM wa kulaumiwa na sio hadithi za serikali 3.
Kinachopimwa mafanikio sera zake sio wingi wa serikali, ukubwa wa nchi ama idadi ya watu.
Wakati mwingine mkuu unachosha sana.
Ungewaambia wazanzibar kwanza.
Wao wanataka mamlaka kamili, wanataka Mkataba hata wewe umesema hilo.

Leo unasema serikali si muhimu. Kama zisingekuwa muhimu katiba ingekuwepo tayari.
Tena hapo juu umesema ''huwezi kuandika katiba kama huna serikali'' hapa umesahau uliandika nini unasema idadi ya serikali si muhimu. ama idadi si muhimu, umuhimu wa kuandika katiba kwa kuangalia serikali unatoka wapi?

Tulia mkuu, jazba, unapoteza mwelekeo,hukumbuki umeandika nini bandiko moja nyuma.
Tulia tu, na uwe tayari kujifunza. Usitukane, pingana kwa hoja na kubali.
Na huu ndio ujinga mwingine, rasilimali ni pomoja na watu, Hivyo unaposema rasilimali huoni kama watu wachache kutumikia watu wengi ndio inaweza kuwa tatizo?

Zanzibar wanalipa kodi zao na zinakuja bara TRA kwenye watu wengi ambao majority ya nguvu kazi hawana ajira.
Ndio maana tunataka kodi za TRA zibaki znz, tunataka watumie uchache wao na rasilimali zao kujiendeleza.
Hatuna sababu ya kuchukua chochote Zanzibar.

Njia rahisi, wanayo serikali yao, watuache na Tanganyika yetu.
Kama wanataka, narudi wakihitaji waje kwa mambo wanayodhani tutawasadia,si kugawana mali yetu kama zetu

Mkandara, mapato ya znz ni bilioni 400 kwa mwaka. Ni kidogo kuliko ya soko la Kariakoo.

Nadhani ni bora kwenda kuiba kariakoo kuliko TRA znz.
Makusanyo yao wastani ni bilioni 20 kwa hesabu za haraka kwa mwezi. Kama kuna mtu anawaibia, hiyo ni dhambi kubwa sana.
Kwanini mtu asiende kuiba Breweries aende kuibia waznz?

Uisiaminishwe maneno ya mitaani, hakuna senti ya mznz inayovuka bahari.

Hisia ni kitu kibaya, wazanzibar na wenzetu wameaminishwa wanaibiwa na Tanganyika.
Leo tunajua Meya wa Ilala anamiliki uchumi mkubwa kuliko Znz, na ni bora kwenda kuchukua fedha Ilala kuliko znz.

Kuna watu wanahisi znz ina uchumi karibu na China. Hisia ni kitu kibaya sana. Just feelings!
Pasipo Elimu huwezi kujenga nguvu kazi ya kizazi kipya! kizazi kipya sio kutegemea gas na Tanzanite bali vijana wengi zaidi kuhitimu elimu ya juu na uwekezaji ktk elimu na nguvu zao ndani. Kati ya watu 10,000 wa bara ni mmoja tu mwenye elimu ya juu, na kati ya watu 100 hamsini hawana kazi.

Walipa kodi halali nchini hawafiki millioni 5 wakati wenye uwezo wa kufanya kazi ni zaidi ya millioni 20, tazama mtaji wa nguvukazi hii inavyopotea na kuoza bure. Mungu atupe nini zaidi isipokuwa sisi kazi yetu kulaumu Zanzibar na Wakoloni.
Ni kweli lakini haihalalilishi tubebe zigo tena lenye gubu.

Tumewabeba wznz miaka 50 bado hawana nidhamu, kila siku kelele.
Ni wakati wakapunguze ile milioni 20 isiyofanya kazi ili tubaki na milioni 18.5.

Kwa taarifa yako hiyo milioni 1.5 ya wznz inachukua zaidi ya milioni 20 ya wasiofanyakazi.
Hawa wasiofanya kazi wanaishi vijiweni, wznz wanadai hata kisicho chao tena kwa kelele.

Tumechoka tuwaache na nchi yao na wao watuache na yetu.
Kama wanahitaji msaada basi waje kwa adabu, tuanze na 7 4 au 1.
Ikishindikana kwani ni lazima, tuvunje jahazi tugawane mbao kila mtu alee watu wake.

Sisi hatuna cha kupoteza wala hatuwahitaji kwasababu hawana impact yoyote katika maendeleo yetu.

Zanzibar ni liability sio asset.Siku hizi tunawambia wala wasipate tabu njia nyeupee
Mkuu Kila napokusoma umeshindwa kutenganisha Kero na mapungufu yetu. Na ndio ktk vijiwe na maneno ya mtaani huwaambia kuhusu Utanganyika kama vile tunavyo bishana ya Yanga na Simba. Ni maneno ya kawaida kwa watu wa Pwani lakini kwa watu kama nyie msojua mnachukulia hasira

Mimi na hao kina Barubaru, Mdondoaji,Takashi tunaweza kaaa meza moja tukazungumza pasipo kutoana macho lakini sio wewe
Ahaa!! Mkandara unaingiza liile suala nililosema kuwa ukiona mtu analijadili basi jua kuna tatizo kubwa zaidi.
Always I'm trying to avoid that premise, I have a lot to offer not on that ground, sorry !!

Mimi na wewe twaweza kaa meza moja na kula hakuna tatizo.
Kinachotakiwa ni uvumilivu tu na kukubali ukweli. Ukiambiwa ukweli hutukanwi,anayekuambia ukweli ni muumini,uongo umekatazwa

Nacheka sana unapozungumzia znz na mimi, mimi kwetu Bububu. Je hilo linanizuia nisiseme ukweli?
Hizi Kero hazinisumbui Wao pia wanaona sisi ni kero vile vile kama mume na mkewe nyumbani haya ni mambo ya kawaida kabisa. Na hata siku moja sintokaa kula meza moja na mtu kama Jussa ambaye fikra zake ni za Kinafiki.

Wewe usomjua ndio unambeba kwa ujinga ule ule wa Miafrika kuamini yupo pale kukusaidia.
Haa kama sisi tunawaona kero na wao wanatuona kero tunasababu gani za kuishi katika dhiki, kwanini tusiishi kama Kenya na Uganda.
Wazanzibar wanataka hivyo

Wazanzibar hawataki muungano wa Nyerere lanatullah, wewe kwanini huelewi mkuu.
Hawataki na Nyerere alisema hatawapiga mabomu.

Sisi tunasema hatuna sababu za kuwazuia kuondoka. Nini kinawazuia kuondoka?
Mkuu wazanzibar hawataki muungano huu wa Mr Lanaatullah Nyerere, wewe unapata nguvu za kuwatetea kutoka wapi?
 
Makonda anataka kutuaminisha kuwa kikwazo cha upatikanaji wa katiba mpya ni UKAWA kususia bunge la katiba kitu ambacho sio kweli.

Mchakato wa katiba umekwama sababu ya wao CCM kutaka kuumiliki mchakato huu uendane na ILANI yao. Ndio maana wamekuwa wakitokwa mapovu ya hasira kuanzia Mwenyekiti mpaka yeye Makonda baada ya kuona tume ambayo waliichagua WAO yenye asilimia kubwa ya wajumbe toka chama CHAO ikitoa rasimu kutoka kwa WANANCHI na kinyume na ILANI yao!

Ndio maana kila aliyepata nafasi ya kuongea amekuwa busy kuishambulia tume hususan mwenyekiti wake Mzee Warioba tena kwa kejeli, matusi, vijembe na meneno mengine mengi yasio na staha kwa mzee kama huyu aliyetumikia nchi hii kwa miaka mingi.

Mchakato huu ukifa wasitafute mchawi kwa UKAWA bali wao wenyewe!
 
Nguruvi3,
Mkuu Mabandiko gani yenye chuki kwa wazanzibar?

Hapo juu umetaka kuingiza mambo ya udini, sasa unanisingizia chuki kwa wazanzibar.
Hujaeleza chuki gani niliyo nayo kwa waznz. Mkuu hebu rudi katika mstari ule wa Mkandara.
Mkuu una matatizo wala sii kidogo kwa sababu hata sikuelewi unachoongea unatapatapa na maneno kama vile mfa maji. Unapoulizwa swali unarukia sehemu nyingine kabisa na kuanzisha yako. Unajaribu ku prove kipi hasa unapokwepa kwepa ovyo! Ya kwamba huna chuki na Wazanzibar kwa kuandika mada ile ambayo umenukuu yalokwisha zungumzwa na Wazanzibar?. Kisha unaanza kujenga Fikra zako za riwaya ati wakifanya hivi, sisi tutafanya hivi yaani ni hadithi ile ile ya SISI against WAO halafu unasema huna chuki?.

Mkuu hata kama wapo Wazanzibar kama kina Jussa wenye chuki nasi (bara), haihitaji Mtanzania bara mwenye weledi juu ya sokomoko na chokonoko za kisiasa kuanzisha ama kuendeleza chuki hizo ni kutofahamu nia na madhumuni ya watu kama Jussa. Haya, hayo mambo ya Udini umeyatoa wapi tena?.. Puuuh! nimechoka maana huelezeki wala hueweki.
 
Makonda anataka kutuaminisha kuwa kikwazo cha upatikanaji wa katiba mpya ni UKAWA kususia bunge la katiba kitu ambacho sio kweli.

Mchakato wa katiba umekwama sababu ya wao CCM kutaka kuumiliki mchakato huu uendane na ILANI yao. Ndio maana wamekuwa wakitokwa mapovu ya hasira kuanzia Mwenyekiti mpaka yeye Makonda baada ya kuona tume ambayo waliichagua WAO yenye asilimia kubwa ya wajumbe toka chama CHAO ikitoa rasimu kutoka kwa WANANCHI na kinyume na ILANI yao!

Ndio maana kila aliyepata nafasi ya kuongea amekuwa busy kuishambulia tume hususan mwenyekiti wake Mzee Warioba tena kwa kejeli, matusi, vijembe na meneno mengine mengi yasio na staha kwa mzee kama huyu aliyetumikia nchi hii kwa miaka mingi.

Mchakato huu ukifa wasitafute mchawi kwa UKAWA bali wao wenyewe!
Mkuu nikuulize kitu, Hivi kweli wewe unaamini hiyo rasimu ya Warioba, CCM hawakuipata na kuisoma kabla hata haijakabidhiwa Bungeni? wewe unafikiri kweli CCM walikaa kusubiri hadi baada ya rasimu ile kukabidhiwa Bungeni au waliisha isoma na kujiandaa mapema kabisa. Kumbuka baada ya tume ya Warioba kumaliza kazi JK alianza kutaja majina ya watu watakao unda baraza la katiba na sii kabla, kisha kila mara Warioba na Salim walikuwa waki mbrief JK kila hatua ya rasimu hiyo hivyo wanajua kilichokuwa kinaendelea toka mwanzo, wewe na mimi pamoja na hao wajumbe wengine ndio walokuwa hawajui lakini sio CCM.

Na JK asingeweza kukataa ama kupiga vita maoni ya wananchi ndani ya rasimu ile kama mnavyodai wakati akikutana na tume ya Warioba. Angepinga yeye hayo maoni ya wananchi kabla ya bunge kama mnavyotaka sidhani kama wananchi wangemwachia mzima na ingekuwa mbaya zaidi ya ilivyo sasa hivi maana kayapinga hata kabla hayajafika kujadiliwa yeye nani?.. Hivyo maamuzi yoyote angeyachukua wananchi msingekubaliana naye maadam ni kinyume cha mlivyotegemea.

Amini maneno yangu, JK hakutakiwa kuwaunga mkono UKAWA kabisa, hasa baada ya kumtukana mwalimu kuwa ni kazi yake yeye, kuudhihaki Muungano wenyewe na kibaya zaidi kuiwekea shaka hata Hati ya Muungano wenyewe kwa kusema Nyerere ali gushi saini ya Karume. These are heavy allegations, tena ndani ya Bunge la katiba likisikilizwa na Watanzania wote kupitia luninga ya taifa! Jamani acheni mchezo na hiyo UKAWA yenu mnaharibu wenyewe kisha mnaisema CCM - Na YES CCM wasingekubali serikali 3 kwa sababu ushahidi na accusations zilotolewa pale bungeni against serikali 2 ilikuwa aibu na Utumbo mtupu!.
 
Nikipata muda nitaweka jamvini nilipoku- quote na kukeuleza mubashara ukiona mtu anaingiza chembe za dIni katika mijadala kama hii ujue kuna tatizo kubwa sana.

Umejaribu sana kuniingiza nikakuambia huko kwenye udini ni swimming pool of hoodlums, mimi siingii.
Mara mbili umezungumzia udini wazi.

Nitarudi niweke quote wanajamvi wataamua nani mkweli kuhusu hili suala.
 
Mkandara kule ulipokuwa unanikokota niende ni kama inavyosomeka hapo chini.

1. Hivi unajuaje mimi nina dini au mpagani au siamini kabisa. Soma maneno yako ya kubatizwa hapo chini. Mkuu unaporomoka sana namna hii, mimi inanisikitisha maana nakujua ni smart.

2. Unajadilina na mimi, unapotumie nyie, una maana akina nani? Tena umetanguliza maneno ya pwani na akina mdondoji n.k. ukashadidia nyie. Ama! Kwanini mimi unifanye plural. Ukweli ni kuwa kuna ulilolenga.

Mkandara ni hivi dini zinapaswa kuwafanya watu wawe smart, kwabahati mbaya that's not the case for some, especially
waliopokea dini, ambao hawachukia muda wa kuifahamu. Hapo ndipo unakuta fanatics n.k.

Na tafadhali usiwe sorry na mimi kwa sababu wewe sii mwelewa ni shabiki na mwenye chuki binafsi. Hutaki kujifunza isipokuw akwa yale ulobatizwa nayo kama muumini wa dini.

Nilichokiandika mimi ni kutokana na ukweli uliokuwepo na sijam quote mtu kama yeye ndiye mwanzishi kama unavyofanya wewe kwa kusema ati CCM waliandika rasimu yao na Sitta ndiye aloishinikiza kama vile ulikuwepo ktk vikao vya CCM. Ni mwongo na mtunzi mzuri sana wa hekaya sanifu na ndicvho pekee kinachonivutia kwako japo najua fika Unaongopa!..
..
Mkandara;10030375] Mkuu pengine hunifuatii kwa makini. Kila napokusoma umeshindwa kutenganisha Kero na mapungufu yetu. Kama swala ni kero za Wazanzibar hata mimi nimezizungumzia sana huko nyuma na Wazanzibar wanajua. Mbali na hivyo nawajua zaidi yako wewe kihistoria na hali halisi yao leo.

Na ndio ktk vijiwe na maneno ya mtaani huwaambia kuhusu Utanganyika kama vile tunavyo bishana ya Yanga na Simba. Ni maneno ya kawaida kwa watu wa Pwani lakini kwa watu kama nyie msojua mnachukulia hasira na kuanza kutukanana kwa matusi ya nguoni.

Mimi na hao kina Barubaru, Mdondoaji,Takashi tunaweza kaaa meza moja tukazungumza pasipo kutoana macho lakini sio wewe.
Nimefunga mjadala wa mambo ya dini, mimi smart na kamwe siwezi kuvutwa kuingia katika swimming pool ya nincomps au hoodlums. I can swim in clear and clean water with sober mind.
Nina uwezo kwa kujenga na kubomoa hoja bila kwenda kanisani au msikitini. Nina uelewa wa dunia hii kwa imani zote.

Rudi katika mstari mkuu. Nimefunga mjadala wa suala hili.
 
Last edited by a moderator:
Nikipata muda nitaweka jamvini nilipoku- quote na kukeuleza mubashara ukiona mtu anaingiza chembe za dIni katika mijadala kama hii ujue kuna tatizo kubwa sana.

Umejaribu sana kuniingiza nikakuambia huko kwenye udini ni swimming pool of hoodlums, mimi siingii.
Mara mbili umezungumzia udini wazi.

Nitarudi niweke quote wanajamvi wataamua nani mkweli kuhusu hili suala.
Hata sikuelewi kabisa. Wewe mwenyewe umeandika na kudai kuwa - Hapo juu mimi nimetaka bla bla blaa!
Hapo juu umetaka kuingiza mambo ya udini, sasa unanisingizia chuki kwa wazanzibar.
sasa nakuuliza yametoka wapi haya ya Udini unasema utatafuta sehemu yaani haya mambo ni ya mwaka gani au? yaani hueleweki kabisa unasema hili ukiulizwa unatafuta sababu nyingine kabisa nje.

Wewe umeandika na kudai kuwa HAPO JUU mimi nimetaka kuingiza mambo ya Udini! wakati ktk mada hii hakuna mahala nime/ tumezungumzia Dini ama Udini.. wewe unakwepa na kwenda mada nyingineee.. Ama kweli wee msanii yaani kaandike sinema za drama utatengeneza utajiri haraka sana.

Sasa hiyo mifano umeelewa nilichoandika kweli? Hivi kweli wewe Unajua tofauti na ugumu wa mtu kuubali ukweli wa kisayansi dhidi ya ule imani ya dini?. Au kwa sababu nimesema Kubatizwa badala ya Kusilimu. Kwani muislaam ndiye rahisi kukubali ya kisayansi nje ya imani yake? halafu nimetanguliza neno KAMA, bado hukuelewa. Jiulize miye nimeijuaje dini yako hadi niingize Udini wakati unaweza kuwa dini moja na miye. Mbona ndio kawaida yangu siku zote kutumia mifano hii basi kama Ungekuwa Mzanzibar usingekubali kuitwa Mke kwa jinsi navyotumia neno hilo, ukiwazia maswala ya Kitandani!. Au wewe mwenyewe ndio sasa unajishtukia! Now I am getting the all picture, everything is unfolding just like that..! waswahili walisema penye ukweli siku zote uongo utajitenga. Duuuh ama kweli sikuyajua haya hata kidogo wala sikuyakisia.

Haya ya watu wa Pwani, nikuulize wewe kwani miye mtu wa Pwani? sasa iweje mtu asokuwa wa Pwani ihusiane na hoja ya Udini? au nilikuwa nazungumzia mtu kutokujua asili ya utani wa watu wa pwani (kufahamu) ya kuwa huwa sii maadui wala hawaweki chuki haihusiani na Uislaam, Ukristu wala dini yoyote ile. Na ndio maana nikakupa utani wa wana Yanga na Simba huwa hawatoani macho na hakuna Udini, Kabila wala jinsia isipokuwa kuelewa utani wao ukoje na hautakiwi kupandisha hasira ama kutoelewa maana ili nawe unaposhiriki usije chukulia kinyume kama hivi wewe hapa na hoja zako.

Nitakupa mfano hai kabisa, sisi tumezoea sana kutanguliza neno la tusi (K Mayo) katika mazunguzo iwe kusifia ama kumchambua mwenzako. Sii jambo zuri hata kidogo wala sii la kujisifia lakini ndivyo walivyokulia wenzetu ktk malezi yao, hata mama yake mzazi anaweza kumtukana mwanaye kwa tusi hilo hilo. Mimi natambua hili na hainipi shida wala hainichoshi kwa sababu nimeishi nao hawa

Siku moja rafiki yangu alikosea alipomuona jamaa mmoja akija ktk kijiwe chetu, akaanza na kusema 'K mayo, wee nakutafuta toka jana sikupati vipi wee!'... Eeehh bwana wee jamaa alilipuka na kuwa mwekundu, alikuja moto ngumi mkononi kwa sababu katukaniwa mama yake. Tukamwambia sii kweli hakuwa na maana hiyo jamaa asikubali akaondoka akisema sisi sote tunamchangia na kumtetea yule jamaa wakati kamtukania mama yake. ...Hivi ndivyo navyokuona wewe, kumbe unasumbuliwa na lugha yangu!
Bora ungesema kwa nini nakuletea ya Simba na Yanga wakati wee ni mshabiki wa Mtibwa !. oops isije kuwa tena nakuhukumu kuwa umetokea Mtibwa! damn...Jamani watu wengine..
 
Mkandara this is getting too low, turudi kwenye mada.
Mimi ninakumbia wazi I will never follow you in that swimming pool.
That is your premise, not me! Nada.

Mimi ni mzaliwa wa pwani kwa taarifa yako. Huko Zenji ni kwetu na Tanga yote ni kwetu.
Musoma ni kwetu nina alama nilizoacha nikikutajia utabaki mdomo wazi.

Unamjua Kembo Migire wa Shirati hospitali, unamjua mzee Mutaragati Chirangi(marhum), Unajua mzee Sheikh Magee(marhum), Unamjua referee Mwichumu (marhmu) na Abdi Agosi, akina Mzee Kitwara,Sheikh Mohame Chamba(Marhumu), Marhum Sheikh Mwinyiatani wa Muheza,Father libaba wa Nyangao n.k. utanijua wewe kwa sentensi mbili

Huwezi kujua ni atheist, pagan au dini gani.
Niliwahi kumwambia mzee Said na katika mnakasha I prvoved him wrong in every aspect.

Kilichoniudhi ni kusema
'
Hutaki kujifunza isipokuw akwa yale ulobatizwa nayo kama muumini wa dini''
Hata ungesema hivi ''Hutaki kujifunza isipokuw akwa yale uliosilimu nayo kama muumini wa dini'' bado ningereka.

Mimi si kijana mdogo, nimeishi dunia hii nimeona mengi kuhusu watu na hizi dini, si limbukeni wala siongozwi na hisia au ushabiki. Kinachoniongoza ni ufahamu.Ninapojadiliana na mtu na kunipeleka katika choo hicho inatia staftishi. I have to be honest with you.

Fuatilia mijadala yangu yote, mtu akishaingiza udini na kutaja taja, mimi humuacha, nina kiwango bora zaidi
Sikuona maana ya sentensi hiyo hata kidogo. Na hujaweza kushawishi jamvi ulikusudia nini.

Kadri uinavyojitetea unazidi kujianika mkuu, nimefunga mjadala wa mambo kama hayo.
************************************************************************************************************

Mkandara this is getting too low, turudi kwenye mada.
Mimi ninakumbia wazi I will never follow you in that swimming pool.
That is your premise, not me! Nada.

Mimi ni mzaliwa wa pwani kwa taarifa yako. Huko Zenji ni kwetu na Tanga yote ni kwetu.
Musoma ni kwetu nina alama nilizoacha nikikutajia utabaki mdomo wazi.
Unamjua Kembo Migire wa Shirati hospitali, unamjua mzee Mutaragati Chirangi(marhum), Unajua mzee Sheikh Magee(marhum), Unamjua referee Mwichumu (marhmu) na Abdi Agosi, akina Mzee Kitwara,Sheikh Mohame Chamba(Marhumu), Marhum Sheikh Mwinyiatani wa Muheza,Father libaba wa Nyangao n.k. utanijua wewe kwa sentensi mbili
Huwezi kujua ni atheist, pagan au dini gani.
Niliwahi kumwambia mzee Said na katika mnakasha I prvoved him wrong in every aspect.

Kilichoniudhi ni kusema
'
Hutaki kujifunza isipokuw akwa yale ulobatizwa nayo kama muumini wa dini''
Hata ungesema hivi ''Hutaki kujifunza isipokuw akwa yale uliosilimu nayo kama muumini wa dini'' bado ningereka.

Mimi si kijana mdogo, nimeishi dunia hii nimeona mengi kuhusu watu na hizi dinimmimi si limbukeni wala siongozwi na hisia au ushabiki. Kinachoniongoza ni ufahamu.
Ninapojadiliana na mtu na kunipeleka katika choo hicho inatia staftishi.
I have to be honest with you.

Fuatilia mijadala yangu yote, mtu akishaingiza udini na kutaja taja mambo kama hayo mimi humuacha kwasababu nina kiwango bora zaidi ya hicho.
Sikuona maana ya sentensi hiyo hata kidogo. Na hujaweza kushawishi jamvi ulikusudia nini.

Kadri uinavyojitetea unazidi kujianika mkuu, nimefunga mjadala wa mambo kama hayo.

Narudi kwenye mada sasa, huko endelea mwenyewe
Mimi nakutandika kwa hoja, huko unakotaka kwenda siendi.

Nimekupa kipande cha mwaka 2011 nikwaonya wznz kuhusu move yao.
Umenisoma kuwa si utunzi naongea ninachokiona kwasabanbu nimeipata akili yangu nafasi ya ufahamu wa mambo muhimu

Kuhusu chuki, mkuu, unanishtumu bure.
Mimi kusema wazanzibar wanachoma moto Watanganyika si chuki ni ukweli.
Mimi kusema wznz wameandika sheria za kumbagua Mtanganyika si muitaliano au mu oman ni ukweli si chuki.
Kusema wznz hawachangii muugano bali wanachota ni ukweli si chuki
Mimi kusema wznz wanataka kuvunja muungano si chuki ni ukweli
Mimi kusema wznz wamevunja katiba si chuki ni ukweli
Ninaposema wanapewa hata wasichostahili ni ukweli si chuki.

Ninapowaunga mkono wapate mamlaka kamili ni ukweli si chuki
Nikisema wanamlaani Nyerere laanatullah kwa muungano ni ukweli si chuki
Nikisema wapo Dodoma bila hoja bali kusinzia kwa gharama zetu, ni kweli si chuki.

Hayo yote na mengine Watanganyika wameyaona.
Elimu imewafumbua macho Watanganyika kuliko walivyokuwa wanaona.

Siku hizi wanasema wazi wanataka Tanganyika yao kwa ajili yao.
Wanawaambia wznz wazi kabisa, njia nyeupee tena mbele ya tv

Wznz wanawajibu wa kujua, kadri wanavyoitaka znz ndivyo tunaitaka Tanganyika.
Kwa bahati mbaya wamekuwa kikwazo Dodoma, wakirudi minazini midomo wazi kwa kelele.

Ni kwa msingi huo tunasema hivi, kama Tanganyika haitarudi kwa majadiliano, wazanzibar watatusaidia kwa lazima na gharama kubwa kuirudisha.
Hilo si mjadala tena ni suala la muda.

Ni ima Tanganyika,znz na Tanzania au Zanz na Tanganyika.
Tuna shida zetu tumechoka kubeba mizigo isyo na tija, isiyotuhusu wala isiyo na adabu.
Samadi inawekwa shambani haibebwi mgongoni miaka 50.

Mkuu Mag3, laiti.......

Basi baba wala sikuwezi maana wewe sii mwelewa kabisa. sasa hao watu ndio wewe kwa mwili wa pili au? Hao wote wana Uelewa wako, na maisha yao yahusiani na yako!. Mkuu wangu jaribu kusoma vitu ukaelewa kabla hujajibu. Wewe ni yule tuko naye hapa na tunajadiliana na wewe ndio hunielewi sio wao maana hawapo hapa (Mwenyezi Mungu aziweke roho mahala pema peponi). wewe ndio unayetafsiri vitu upendavyo na inavyokufurahisha ukidhani unajua, na hata ukifahamishwa kuwa umekosea bado unakuja na jingine la kuzusha vile vile.

Yaani sikuelewi kabisa mkuu unazidi kujichanganya utakuja pata maradhi ya depression usipo angalia maana sijui unasoma vitu gani, unaelewa vitu gani na unakuja kujibu vitu gani. Kwani hakuna Watanganyika wanawachoma Watanganyika wengine, hakuna mikoa ilokuwa mzigo kama Zanzibar na tunaendelea kuibeba! Hizi fikra hizi za kufikiria wewe unacho kumbe maskini wa kutupwa ndio msingi wa arguement zangu.
 
Narudi kwenye mada ninakokutandika kwa hoja na kubadili sentensi kila saa, fli flops
Nimekupa kipande cha mwaka 2011 nikiwaonya wznz kuhusu move yao na hatari inayowakabili
Si utunzi naongea ninachokiona kwasabanbu nimeipa akili yangu nafasi ya ufahamu wa mambo ya maana

Kuhusu chuki, mkuu, unanishtumu bure.
Mimi kusema wazanzibar wanachoma moto Watanganyika si chuki ni ukweli.
Mimi kusema wznz wana sheria za kumbagua Mtanganyika si muitaliano au mu oman ni ukweli si chuki.
Kusema wznz hawachangii muugano bali wanachota ni ukweli si chuki
Mimi kusema wznz wanataka kuvunja muungano si chuki ni ukweli
Mimi kusema wznz wamevunja katiba si chuki ni ukweli
Ninaposema wanapewa hata wasichostahili ni ukweli si chuki.

Ninapowaunga mkono wapate mamlaka kamili ni ukweli si chuki
Nikisema wanamlaani Nyerere laanatullah kwa muungano, ni ukweli si chuki
Nikisema wapo Dodoma bila hoja bali kusinzia kwa gharama zetu, ni kweli si chuki.

Hayo yote na mengine Watanganyika wameyaona.
Elimu imewafumbua macho kuliko walivyokuwa wanaona.

Wanasema wazi wanataka Tanganyika yao kwa ajili yao.Wanawaambia wznz njia nyeupee tena mbele ya tv

Wznz wanawajibu wa kujua, kadri wanavyoitaka znz ndivyo tunaitaka Tanganyika.

Ni kwa msingi huo tunasema hivi, kama Tanganyika haitarudi kwa majadiliano, wazanzibar watatusaidia kwa lazima na gharama kubwa.Hilo si mjadala tena ni suala la muda.

Ni ima Tanganyika,znz na Tanzania, au Zanz na Tanganyika.
Tuna shida zetu tumechoka kubeba mizigo isyo na tija, isiyotuhusu wala isiyo na adabu.
Samadi inawekwa shambani haibebwi mgongoni miaka 50.

Mkuu Mag3 wakisemezana na Mzee Mwanakijiji katika post fulani.
Nakumbuka maneno machache sana waliyosema '' Laiti ungelijua...''

Hawa watu wakubwa wanaongea kwa staha wamajistiri na kuwasitiri wenzao, hawasemi semi hovyo
 
Last edited by a moderator:
Basi baba wala sikuwezi maana wewe sii mwelewa kabisa. sasa hao watu ndio wewe kwa mwili wa pili au? Hao wote wana Uelewa wako, na maisha yao yahusiani na yako!. Mkuu wangu jaribu kusoma vitu ukaelewa kabla hujajibu. Wewe ni yule tuko naye hapa na tunajadiliana na wewe ndio hunielewi sio wao maana hawapo hapa (Mwenyezi Mungu aziweke roho mahala pema peponi). wewe ndio unayetafsiri vitu upendavyo na inavyokufurahisha ukidhani unajua, na hata ukifahamishwa kuwa umekosea bado unakuja na jingine la kuzusha vile vile.

Yaani sikuelewi kabisa mkuu unazidi kujichanganya utakuja pata maradhi ya depression usipo angalia maana sijui unasoma vitu gani, unaelewa vitu gani na unakuja kujibu vitu gani.
Mwenyezi mungu awarehemu hao na wengine waliotangulia mbele ya haki. Amina.

Ninataka uelewe tofauti na unavyonielewa mtandaoni. Uelewe kuwa huko ukerewe ni kwetu pia.

Ahsante kwa mjadala uliovuka uwezo wangu, nadhani niishie hapa. Inatosha nisije jikuta nimeingia eneo lao sheikh!

Inshallah, mfungo mwema na sijui huko kwenu futr saa ngapi.
 
Mwenyezi mungu awarehemu hao na wengine waliotangulia mbele ya haki. Amina.

Ninataka uelewe tofauti na unavyonielewa mtandaoni. Uelewe kuwa huko ukerewe ni kwetu pia.
Hee ya Ukerewe tena! haya basi labda tuongee kilugha pengine utanielewa au kwa sababu wewe Mtanganyika ndio maana ni Mkerewe pia!
 
Mkuu Mabandiko gani yenye chuki kwa wazanzibar?

Hapo juu umetaka kuingiza mambo ya udini, sasa unanisingizia chuki kwa wazanzibar.
Hujaeleza chuki gani niliyo nayo kwa waznz. Mkuu hebu rudi katika mstari ule wa Mkandara.

Ninafahamu hoja zangu ni nzito na kwa upungufu wa majibu unaingiza mambo ya dini na kusingizia chuki.
Onyesha wapi nilipo na chuki nao, otherwise jazaba na flip flops hazijibu hoja. Sisi tutaongelea hoja na si nje ya hapo.

Wazanzibar wengi wanataka kuvunja muungano(ingawa wameshavunja), Mkataba, serikali 3.

Hawataki S2 au Moja. Zaidi ya miaka 5 nyuma nimesimamia Tanganyika nikiwaunga mkono wznz kuwa na mamlaka kamili.
Hivi hapo mimi nawewe nani mwenye chuki?

Wewe unayewalazimisha ukisema 'watapata hasara'' au mimi ninayeheshimu maamuzi yao?

Kuhusu kuzungumza,naongea kama mwananchi haswa.

Nimeanza kuandika kuhusu Tanganyika, UKAWA hawajachaguliwa.

Nimewaonya sana wazanzibar kabla ya rasimu ya kwanza.
Nikuonyeshe kuwa hatubahatishi na wala hatuna chuki soma habari hii hapa chini.

Huu 'utunzi kama anavyouita Mkandara'' uliandikwa na Nguruvi3 kabla ya kuanzishwa Mchakato, kuundwa kwa tume ya Warioba au UKAWA . Wananchi tuliona haya.

Utunzi huu unasimama wenyewe na thamani yake kama ilivyokuwa miaka kbala ya UKAWA au Warioba na tume.

Kahiyo sisi tunaongozwa na akili hatuongozwi na hisisa hisia au mashaka au hofu. T
tunaongozwa na fikra, hatuandiki utunzi tukiweka akili zetu rehani kwenye udini.
Tunaongozwa na fikra na mantiki na siyo WENGI WAPE.

Mkandara na leo narudia kusema wazn wamefungua can of worms.

Kilichopelekea hilo ni elimu ndogo . Leo Mdondoaji na takashi wapo wapi?
eo tunwaambia bila shaka hatuwahitaji hata kwa bahati mbaya na hawana la kusema, wanufyata tu. Njia nyeupee hawana la kujibu

Muungano ni kuwasidia wao hawatusaidii lolote na wala hakuna prospect za mzanzibar kutusaidia jinsi alivyojaa chuki na husuda kwa Mtanganyika. Ni ukweli huo Mkandara. Nani anakupenda akuchome moto! Si wamechoma Watanganyika moto, lini umesikia sisi tumewatia vibiriti.

Nitakufafanulia kwanini elimu yao ni ndogo sana, lakini kwanza tafakari hapo ili uone kuwa tunaona miaka 4 minne au mitano mbele. Hatusombwi na hisia hisia za kusilimu au kubatizwa. Huko hatupo kwasababu ni eneo la watu wasio na hoja. Period.

Nguruvi nadhani hujaufahamu msimamo wangu hebu pitia mabandiko yangu kabla hujanituhumu mkuu.
 
Nguruvi nadhani hujaufahamu msimamo wangu hebu pitia mabandiko yangu kabla hujanituhumu mkuu.
Msimamo wako ni znz yenye mamlaka kamili, serikali 3 au mkataba.

Hivi karibuni umekata kona na kusema'' wznz wameyataka wenyewe'' nikakuuliza, sheikh Mdondoaji kulikoni mbona waniacha pwani bamvua kubwa hili? Ukanijibu umegundua kitu kwa hawa akina Jusa.
Basi niliposikia neno inshallah nikawa kimya nikisubri habari, ndio hadi leo twaonana tena.

Haya, nijaalie kwanza, na ahli, swaumu na kila jema. Tukae kitako unipe habbari, kama waelekea kule tulikokuwa tunakwenda au umekata kona zaidi. Mie sijatoa tuhma yoyote naeleze kilichojiri tu. Lau kuna sintofahamu, huu ndio wakati unieleweshe nikutake radhi niliposhindwa kukuelewa bdio uungwana.

Karibu.
 
Mkuu nikuulize kitu, Hivi kweli wewe unaamini hiyo rasimu ya Warioba, CCM hawakuipata na kuisoma kabla hata haijakabidhiwa Bungeni? wewe unafikiri kweli CCM walikaa kusubiri hadi baada ya rasimu ile kukabidhiwa Bungeni au waliisha isoma na kujiandaa mapema kabisa. Kumbuka baada ya tume ya Warioba kumaliza kazi JK alianza kutaja majina ya watu watakao unda baraza la katiba na sii kabla, kisha kila mara Warioba na Salim walikuwa waki mbrief JK kila hatua ya rasimu hiyo hivyo wanajua kilichokuwa kinaendelea toka mwanzo, wewe na mimi pamoja na hao wajumbe wengine ndio walokuwa hawajui lakini sio CCM.

Na JK asingeweza kukataa ama kupiga vita maoni ya wananchi ndani ya rasimu ile kama mnavyodai wakati akikutana na tume ya Warioba. Angepinga yeye hayo maoni ya wananchi kabla ya bunge kama mnavyotaka sidhani kama wananchi wangemwachia mzima na ingekuwa mbaya zaidi ya ilivyo sasa hivi maana kayapinga hata kabla hayajafika kujadiliwa yeye nani?.. Hivyo maamuzi yoyote angeyachukua wananchi msingekubaliana naye maadam ni kinyume cha mlivyotegemea.

Amini maneno yangu, JK hakutakiwa kuwaunga mkono UKAWA kabisa, hasa baada ya kumtukana mwalimu kuwa ni kazi yake yeye, kuudhihaki Muungano wenyewe na kibaya zaidi kuiwekea shaka hata Hati ya Muungano wenyewe kwa kusema Nyerere ali gushi saini ya Karume. These are heavy allegations, tena ndani ya Bunge la katiba likisikilizwa na Watanzania wote kupitia luninga ya taifa! Jamani acheni mchezo na hiyo UKAWA yenu mnaharibu wenyewe kisha mnaisema CCM - Na YES CCM wasingekubali serikali 3 kwa sababu ushahidi na accusations zilotolewa pale bungeni against serikali 2 ilikuwa aibu na Utumbo mtupu!.

Sasa mkuu wangu unapinga nini na unakubali nini? Sijakuelewa...

Ikiwa JK alikuwa anafuatilia hatua kwa hatua kazi ya tume ikawaje akawageuka na kuwapinga alipohutubia bunge la katiba? Alifanya hayo kwa faida ya nani? Au kwa shinikizo kutoka wapi? Na ni yeye ndio aliyefungua mlango kwa wengineo wote kumporomoshea matusi Mzee Warioba...
 
Halafu mkuu Mkandara unaposema "kumtukana Mwalimu" wamemtusi kivipi? Kueleza alipokosea ndio kumtusi? Hilo suala la hati halali au feki mbona serikali yenyewe ilikuwa na kigugumizi cha muda mrefu kulijibu?
 
Last edited by a moderator:
Sasa mkuu wangu unapinga nini na unakubali nini? Sijakuelewa...

Ikiwa JK alikuwa anafuatilia hatua kwa hatua kazi ya tume ikawaje akawageuka na kuwapinga alipohutubia bunge la katiba? Alifanya hayo kwa faida ya nani? Au kwa shinikizo kutoka wapi? Na ni yeye ndio aliyefungua mlango kwa wengineo wote kumporomoshea matusi Mzee Warioba...
Samahani mkuu pengine hatuelewani, Je unaweza kunionyesha ni wapi JK alimgeuka Warioba ktk Hotuba yake Bofya ili twende hatua kwa hatua na swala hili?

2. Swala la kumtukana mwalimu linahusiana vipi na rasimu ya Warioba? ni wapi wananchi walitaka kujua (maoni yao) ama kuelezea swala lolote linalomhusu Mwalimu ama uhalali wa hati ya Muungano?. Iweje rahisi wao Ukawa kutoka nje ya rasimu, lakini sio mtu mwingine maana nijuavyo ndani ya rasimu ile kuna maoni ya wananchi (wachache) kuhusu serikali 2 pia ambayo yalitakiwa kuzingatiwa ktk mchakato wao lakini UKAWA hawakutaka yazingatiwe ama yatazamwe isipokuwa kuvunja jahazi tugawane mbao tukiwa katikati ya bahari..
 
Mkuu Mag3 wakisemezana na Mzee Mwanakijiji katika post fulani.
Nakumbuka maneno machache sana waliyosema '' Laiti ungelijua...''

Hawa watu wakubwa wanaongea kwa staha wamajistiri na kuwasitiri wenzao, hawasemi semi hovyo
Mkuu Nguruvi3, asante kwa hiyo heshima unayonipa ambayo nina hakika kwa asilimia 100% kwamba, kama binadamu, inanipwaya; siwezi kufikia kiwango hicho. Tatizo langu kubwa ni moja...sisiti hata siku moja kuliita koleo kwa jina lake...in a nutshell, sina uvumilivu na mawazo ninayoamini ni ya kinafiki. Kama ninaishi sehemu yenye unyevu unyevu halafu najikuta nikiathirika kiafya, nahama...tofauti na Mkuu Mkandara atakayetetea kubaki hapo hapo kwa sababu tu kajikuta hapo, ni msimamo wa ajabu kweli kweli. Safari ni ndefu; huku simba na huku mbwa mwitu wote wakiwa na njaa kali, laiti angejua...!

Si uungwana kumjadili mtu na najua kwa posti hii wapo watu watashindwa kunielewa, kwao natanguliza samahani...ni upungufu tu wa kibinadamu. Mkandara nimekuja kumuelewa labda zaidi ya ambavyo ningekusudia hivyo najitahidi sana kutojibu nyingi katika michango yake. Mara nyingi, kama walivyo wasomi wetu wengi, anajikuta between a rock and a hard place kama wasemavyo waongea ung'eng'e, tabia ambayo ni rutuba kubwa ya unafiki. Hali hiyo imewafanya wasomi wetu wengi washindwe kupata jawabu la swali, wangependa wakumbukwe kwa lipi siku za baadaye katika historia ya taifa hili kwani huku wataka na kule wataka!

Nakumbuka kuna wakati kwenye mnakasha kuhusu historia ya Tanganyika na wazee wa Gerezani, Mkandara alivyokimbizwa kwa mashambulizi alipotaka kuonesha kuwa naye ni mtoto wa mjini...naam alikutana na saizi yake wanaoongea lugha moja (ya Saigoni?), hakurudi tena kwenye mjadala na badala yake sisi wakuja ndio tukaachiwaa usukani, kuwatetea wazee wetu waliolipigania nchi yetu bila kujali tofauti zao kikabila wala kidini; nachelea kusema, kutokana na msimamo wetu huo na mwelekeo wa mnakasha Mkandara alichukulia kwamba wengi wetu tumepitia ubatizo! Laiti angejua...!

Kusema kweli wengu humu hatufahamiani; wengine shule zetu ni za kuunga unga lakini pamoja na will and desire to fight for change, we happen to have the courage kwa sababu bila vyote vitatu kinachobakia ni usanii! Unafiki at its best!Unafiki wa kukataa serikali tatu kwa madai ya kuvunja Muungano wakati ni wazi mabadiliko ni lazima ili tuweze kupiga hatua kutoka point A na kufikia poin B.Wazo la serikali moja ni la kufikirika na kwa sasa kila moja wetu anajua haliwezekani labda kwa mtutu wa bunduki, kitu kisichowezekana katika karne hii na kulivalia njuga ndio usanii wenyewe! Laiti angejua...!
 
Mkuu Mag3 ya laiti..

Ili kuweza kufanya unafiki katika kiwango kizuri ni lazima uwe au ujifanye au ujitoe fahamu.
Mambo yalipochukuliwa kuingizwa katika muungano ililenga kwenda S1.
Wanafiki wakasema ni kuidhulumu znz. Nyerere akalaaniwa wengine tukisitika na wanafiki hawakukemea.

Rasimu ya kwanza ikaondoa mambo 15 ya 1964. Wanafiki wakabaini hilo si jambo jema kwa znz.
Wengine wakasema wanataka mkataba, tukauliza mkataba na znz kuhusu nini?
Wanafiki hawasemi kuwa znz inahitaji ulinzi na usalama wa bure na kulipiwa gharama ziziso na tija wala riba.

Wanafiki wale wale waliosema Nyerere laanatullah wanaungana kusema S2.
Wakiondoka hapo wanalaani Nyerere laanatullah. Unaona jinsi unafiki unavyofanya kazi.
Wanafiki wanasema znz ilikatazwa kujiunga na OIC. Halafu wanataka S2, hivi unawezaje kuwa na OIC katika Tanzania moja.
Sisi tunaosema S3 tunataka znz iende OIC na kukopa washington, wanafiki wanageuga na kutaka ya ''Nyerere laanatulah''

Hakuna Serikali moja wala mambo ya pamoja ikiwa kuna mambo ya znz na Tanzania ambayo znz imo.
Hesabu hazikubali isipokuwa kwa wanafiki tu. Huwezi kuwa nz znz pande mbili, Tanganyika ikiwa haipo.

Baada ya kuishiwa hoja, kwa ukweli kuwa serikali moja haiwezekani, S2 hazina majibu na wala hazina haki kwa Mtanganyika, wanafiki wanatumia silaha nyingine wanaoijua vema. Hawa wanafiki wanaolaani ''Nyerere lanatullah'' ndio hao hao wanataka mfumo wa Nyerere, angalia manafiki wasivyo na haya mbele ya mwenyezi mungu.

Mkuu Mag3 ndio ukinisoma, nimesisitiza kuwa ukiona mtu anatumia silaha mbovu dhaifu na chafu yenye udini ujue lipo tatizo kubwa. Kwanza kaishiwa hoja kwasababu hiyo ndio silaha rahisi na nyepesi kwa wasio na hoja, pili, unafiki unachukua nafasi na tatu, ulevi wa unafiki unamtoa mtu fahamu. Laiti....

Wznz wametaka S3 au Mkataba, tunawasidia wapate haki zao, wasinyonywe, waweze kukopa Washington, wajiunge na taasisi za kimataifa na OIC, leo tunaonekana wabaya.

Wanafiki wanakana hayo wanarudi kutuambia S2 ni nzuri, zile zile za ''Lanatullah Nyerere''.
Tena wanasema mambo yote ni yetu isipokuwa ya znz ni ya znz.
Unafiki kitu kibaya sana. Sisi tunasema wapewe wanachotaka na waendelee kwa wakati wao tunaonekana wabaya

Sisi tunaosimama na Tanganyika yetu tunaonekana maaluni kwasababu tunatetea Tgk na si zanzibar.

Tunaosema haki irudi kwa pande zote tunaonekana wabaya zaidi ya wanafiki wnaaomdanganya hata mungu.

Useme Nyerere laanatullah halafununapigia debe S2 za laanatullah, kama si kumchezea mwenyezi mungu ni nini!

Huwezi kutetea S2 ukasema unatetea znz.
 
Back
Top Bottom