Ntaendelea kuamini kuwa mungu yupo haijalishi nikifika mbinguni nitamkuta au la!.
Ila Mungu yupo yaani kuna wakati kabisa unahisi uwepo wake karibu nawe, kuna wakati unakuwa kwenye matatizo makubwaaa sana ila ukimuita msaada unatokea pale pale.
Mimi amenifanyia mengi sana amemlinda mama yangu yupo hai, wadogo zangu etc
Kubwa zaidi hii pumzi nisiyoilipia hata sent moja napumua tu bureee Asante mungu.
Kuna wakati nakuwa namuomba Mungu nikilalamika moyo unaniambia acha kulalamika kuna nilichonacho ambacho mwingine hana naishia kusema asante Mungu.
Amini Mungu yupo
Hakuna mwenye tatizo kabisa na kipi unapaswa kuamini
Unaweza amini almost anything
Tatizo ni pale unapotaka na wengine wafate imani yako, na wasipofata uwaone waovu na kuwalaani kuwa watafia kwenye tanuru la moto
Unapofikia hatua hii, ndipo tunapotaka uthibitishe unachoamini
Hakuna aliyeweza, mpaka kwanzia page ya kwanza mpaka hii
Pia wakati una mshukuru Mungu kwa kukuweka hai wewe na Familia yako
Kuna mtoto hivi sasa somewhere,ana mpoteza mama yake kwa Cancer japo alimuomba sana Mungu amsaidie
Mungu ambaye alishindwa kuzuia Hitler asiue watu zaidi ya Million 16 ndani ya miaka 5
Point ni kwamba, maombi ni 50 na 50
Yaani kila unachoomba kina nafasi ya kutimia kwa 50%
Wewe shahidi, nusu ya yote unayoomba hayatimii
Kujipa moyo unasema Mungu atakujibu siku yoyote au wenda sio mapenzi yake
Unasahau kuwa ni just matter of coincidence
Umeomba usiku huu upate kazi, na kesho ukaitwa kwenye interview
Mungu amejibu maombi sio?
Kwenye interview kuna non believer ambae pia ali apply na akaitwa bila kufanya maombi kama wewe,
Ni just circumstance tuu
Kuomba ni sawa na kuongea peke yako
Na kama unaamini kwenye Mungu aliyepanga kila step katika maisha yako tangu ukiwa tumboni basi utakubaliana na mimi ninaposema maombi ni kujiongelesha peke yako
Fikiria hivi, kama Mungu tayari alishaanda Mpango kamili kuhusu maisha yako,
Na alijua kipi kinakufaa na kipi hakikufai,
Huoni kuomba ni kutaka kubadili mipango yake?
Kama alipanga usioe au kuolewa, huoni kuomba ndoa ni kuongea peke yako?
Pia hii hewa unayovuta haina sababu yoyote ya kuuzwa
Kuuza na kununua ni human constructions, zina maana tu kwenye akili yetu
Hujui carbon dioxide unayoitoa, inavutwa na mimea inayotoa oxygen in return
Ni fair exchange, kama unaamini katika kuuza na kununua basi kila sekunde unayopumua unanunua oxygen kwa kulipia carbon dioxide