Na ndio maana nimetanguliza kusema kua kukubali kua kitu fulani hukijui kwasababu umeshindwa kukitafiti na kupata majibu sahihi ni jambo la busara wala sio aibu. Kutokubali kushindwa na kulazimisha majibu ambayo hayajapitia uchunguzi kwa lengo la kujipa tumaini ni ujinga kabisa.
Imagine unaelewa kabisa hiki unachokisadiki sio halisi umekitunga tu lakini unaamua kufumba macho na ubongo kujidanganya kua ni cha kweli kwa ajili ya kujipa tumaini, huu si wazimu?
Kwenye swala la imani (faith) ambayo ni common kwenye dini so nimegusa imani kwenye angle ya kiroho ambayo ni universal, sikumaanisha imani ya (trust) kama kuweka confidence kwa mtu mwingine kua hatokuangusha kwa jambo fulani. Kama mimi nilivyokuwekea confidence kua hutanijibu post yangu kwa kunitukana. Trust, Believe, Faith, Hope and Love ni somo pana na ni maneno yanayo changanya sana kimatumizi kulingana na muktadha husika
Hivyo leo hii ukimuambia mkristo kwamba Thor ni mungu wa kweli basi bila shaka hawezi kukubali kisa "thor" ni "imani ya mungu hivyo hapaswi kuhoji", well lazima akatae sababu sio "Imani" yake!.
Kuna swali ambalo hujalijibu, niliuliza kama imani haitakiwi kuhoji kwanini tuna imani zaidi ya moja kuhusu mungu huku zikipingana?
Huoni wingi wa hizo imani ulikuja baada ya watu kuanza kuhoji imani iliyotangulia ambayo walikua wakiiamini na wao kuanzisha imani yao walioona inafaa?
Kitendo cha wewe kusema (nitafanya kila njia ili kuhakikisha naokoa maisha yake) ni tayari hujui kama atapona au hatopona lakini bado unafanya kila njia ili umsaidie.
Na mpaka hapo tayari umeshaweka hope, na hope tayari ni imani.
Kama ungetaka kutumia logic basi ungeshindwa kumsaidia ndugu yako sababu hauwezi kuapply logic juu ya imani.
Hiki ulichokiandika hapa nime-notice kua we ni miongoni mwa watu ambao wanasumbuliwa na matumizi haya maneno matano trust, hope, faith, love and believe. Kwa ufupi tu ni kwamba hujaelewa mantiki yangu, mantiki yangu kwanza haikua mimi kukataa kutumia imani, tatizo linakuja kwako kushindwa kujua imani gani ambayo naizungumzia hapa.
Mzee kajifunze maana ya hayo maneno na matumizi yake kwanza unaonekana kuchanganywa sana
Kila swali ninalouliza basi linakuwa na point yake.
Ngoja niende straight kwenye point.
Trust ya kuamini kama mimi sitojibu kwa matusi bila ya kujua kama nitajibu kwa matusi au lah Na
Trust ya kuamini kuna mungu bila kujua kama yupo au hayupo, ni imani mbili zisizo na tofauti yoyote.
//Nb. Kwa imani siongelei kuhusu vitabu vya dini bali naongelea imani kama imani.
[[Imagine unaelewa kabisa hiki unachokisadiki sio halisi umekitunga tu lakini unaamua kufumba macho na ubongo kujidanganya kua ni cha kweli kwa ajili ya kujipa tumaini, huu si wazimu?]]
Kwanza kabisa mimi sitegemei vitabu vya dini kuamini uwepo wa mungu bali naamini kuhusu uwepo wa mungu kutokana na observation na misingi yangu mwenyewe.
Unaweza kuamini uwepo wa mungu bila ya vitabu vya dini. Imani na vitabu vya dini ni vitu viwili tofauti.
Kama wewe ulivyo weka trust kwamba mimi sitojibu kwa matusi ilhali hujui kama nitajibu kwa matusi au lah,
Ndio vilevile au sawasawa na kuweka trust kuwa kuna mungu lakini hujui kama yupo au lah.
Sasa mimi naweza kuuliza Je ulijuaje kama fulani hatojibu kwa matusi ikiwa hujui kama atajibu kwa matusi au lah?
Je wewe utaweza kujibu hilo swali?
AU unataka kusema " kitendo cha wewe kuweka trust kwamba mimi sitojibu kwa matusi" ni Wazimu pia.
Ukikataa then utakuwa unajipinga mwenyewe.
Pia imani ya kuamini kama kuna mungu ikiwa hujui kama yupo au hayupo, haijalishi kama kweli au sio kweli bali pia ni kugorven binadamu.
Ukweli ni kwamba watu wengi hawajitambui bila ya kuwaambia wafanye nini basi watu wangekuwa vichaa zaidi na dunia ingekuwa chafu mara mia ya sasa hivi.
Ndio maana kuna serikali, sheria na kanuni vyote hivyo ili kuhakikisha watu wanakuwa kwenye mstari sahihi na vyote hivyo lengo ni kuwa na Uongozi.
Sasa imani lengo kuu ni kuhakikisha atleast watu wanakuwa kwenye mstari, Imani ndio kiongozi wa mwisho, haijalishi kama ni kweli au sio kweli.
Ni kama wewe ulivyoweka trust ya kutojibiwa matusi hukujiuliza swali lolote bali uliamini tu, the same thing ndio kinatokea kwa wanaoamini kwenye uwepo wa mungu.
Maana ya imani ni kuamini bila kuuliza sababu ukiuliza hakuna kitu ambacho kitamake anysense.
Sasa nyie jamaa mnajaribu kuhoji credibility ya Imani kitu ambacho mnajua ni impossible kupata majibu, na hiyo ndio sababu nikawauliza kwanini mnapinga uwepo wa mungu?
Well mkashindwa kujibu na sidhani kama mtakuja kujibu.
Sababu inayowafanya nyinyi kushindwa kujibu "kwanini" ndio sababu hiyohiyo inayowafanya waamini uwepo wa Mungu washindwe kujibu.
[[Kuna swali ambalo hujalijibu, niliuliza kama imani haitakiwi kuhoji kwanini tuna imani zaidi ya moja kuhusu mungu huku zikipingana?
Huoni wingi wa hizo imani ulikuja baada ya watu kuanza kuhoji imani iliyotangulia ambayo walikua wakiiamini na wao kuanzisha imani yao walioona inafaa?]]
Hapana. Imani ni kama utamaduni na kila kundi la watu lina tamaduni zake.
Kundi la watu sababu binadamu hawaishi sehemu moja wala hawakuwahi kuishi kwa pamoja hivyo wazi kupingana na kutofautiana ni kitu cha kutegemea.
Unaposema "watu kuanza kuhoji imani iliyotangulia" ni sawasawa na kusema (leo hii watu wote billion 8 tuanze kuhoji imani moja like wote tunakaa sehemu moja) kitu ambacho ni uongo.
//swali jepesi sana.
[[Hiki ulichokiandika hapa nime-notice kua we ni miongoni mwa watu ambao wanasumbuliwa na matumizi haya maneno matano trust, hope, faith, love and believe. Kwa ufupi tu ni kwamba hujaelewa mantiki yangu, mantiki yangu kwanza haikua mimi kukataa kutumia imani, tatizo linakuja kwako kushindwa kujua imani gani ambayo naizungumzia hapa.]]
Ngoja nimention hii kitu kwanza.
kwenye kiingereza neno moja linaweza kuwa na maana nyingi tofauti na maneno mengi pia yanaweza kuwa na maana moja.
mfano ukisema faith, hope, belief, trust, optimism, expectation, confidence, credence, sureness hayo maneno yote yana maana moja kwenye kiingereza except yanatumika kutegemea na situation husika. hata kwenye kiswahili pia.
Au kama unapinga basi toa maneno tofauti kwenye kiswahili yanayowakilisha hope, faith na trust huku yakiwa na maana tofauti pia...?
Hivyo kwa mfano huo bila shaka naelewa maana za maneno hayo matano.
Tatizo ni wewe kushindwa kuelewa maana za hayo maneno hivyo unajicontradict bila kujua.
Imani unayoitumia wewe kuamini ndio imani hiyohiyo wanayoitumia waamini mungu kuamini.
Narudia hapa siongelei vitabu vya dini bali naongelea imani kama imani.