love life live life
JF-Expert Member
- Sep 12, 2021
- 2,584
- 3,051
Nashukuru kwa kukili kuwa wew ni mweupe katika sayansi ,Kuna maswali mengi yana ingia hapa kwenye hoja yako, inawezekana hii confusion inajitokeza kutokana hatuja kubaliana ni aina gani ya huyo mungu ambaye unamkusudia.
Ikiwa kama sifa za mungu wako ni pamoja na kuto kuonekana, asiyepimika, undetectable nk. hivyo kuniambia kua uthibitisho wa mungu wa aina hii unahitaji sayansi utakua unatuongopea, hiyo ni logical fallacy iliyo sheheni inconsistences
Mimi wala sihitaji sayansi, logic pekee inatosha kujua ukweli na uwongo. Katika hoja yako nikiona rhetorical statements nitajua tu kua huu ni uongo. Kwa mfano mtu aniambie kua katikati ya jua kuna chupa ya chai inazunguka na ili uweze kujua kua chupa ya chai hiyo ipo unahitaji kujua centre ya sayansi ya mwanzo ilikua wapi. Hapo nimetumia logic tu wala sio sayansi
Wewe umeniambia unauza gari linalo paa angani Milion 10, mimi nimekua interested nikasema niko tayari kununua lakini kabla ya yote nahitaji unithibitishie hilo gari lipo, hapo ni mechanism gani ya sayansi inahitajika kuthibitisha hilo gari lipo au ni kitendo cha wewe kulileta nilione likiwa linapaa?
Sio sayansi yangu ina walakini, kusema hivyo tu umeonesha uwalakini. Sayansi haiko perfect na ndio mwanzo wa uwalakini wenyewe, mara kadhaa inakosea na ina admitt hilo. Kama sayansi inawalakini kivipi mwanasayansi anayeifanya hiyo sayansi akose uwalakini? na ndio maana haiishi kutafiti jibu ambalo limepatikana
Hili nililitambua mapema.
ungejua sayansi imepita wapi mpaka kufikia leo majibu yote ungeyapata