Ndio ulichosema ni kweli kwamba nilitakiwa nianze na tafsiri ya neno Mungu.
Tafsiri uliyotoa ni sahihi kulingana na huyo mwanasayansi anavyoeleza lakini tafsiri iliyokuwa bora zaidi naweza sema hivyo inapatikana kwenye vitabu vya kidini kitu ambacho toka mwanzo nlikataa kuvitumia kama reference
Neno Mungu sio kazi ya wanasayansi ndio maana naweza sema hiyo tafsiri yake inaweza isiwe bora. Wanasayansi wamepata hili neno nadhani kwa watu wanaoitwa theologists ambao misingi ya maisha yao na uelewa wa hii dunia wamekuwa wakiongozwa na Imani kitu ambacho kwa wanasayansi na wanafalsafa wanakataa pale wanapokuwa wanatafuta kujua ukweli
Ukweli tunaotafuta hapa ni juu ya kuwepo kwa Mungu. Ukitumia misingi ya kisayansi trust me ukweli utakuwa mgumu kupatikana vivyo hivyo ukifanya reasoning bado utakwama. Kwanini nasema itakuwa ngumu ni kwa sababu utakuwa unajaribu kutafuta ukweli ambao tayari upo
Mwanzo kabisa walioweza kuja na vitu tangible kuprove existence of God were prophets but kwa sasa hawa watu hatuna tena but we have their message
Kuhitimisha ni kuwa naweza nsiweze kuprove hili kwako kwa sasa but trust me after two years I will be back here with something tangible to prove existence of God
Thank You!
Nafikiri mambo ya Mungu yanawezekana kuprove kabisa
Mfano ni kwangu mwenyewe.
Mwaka jana 2020 nilipata kuambiwa na Mungu kuhusiana na huduma ambayo aliniambia ninatakiwa kuifanya lakini nikawa namuuliza maswali. Na Kati ya maswali ambayo nilikuwa namuuliza alinijibu ya kuwa nitatumia vitu Vilivyopo physically katika kuwafundisha watu.
1. Nilimuuliza nitawezaje kumleta mtoto kwenye ili nimfundishe neno lake?
Alinijibu kwa kuniuliza swali ya kuwa mtoto anapenda nini? Nikamjibu, Naye akaniambia ya kuwa katika hicho kitu ambacho mtoto anakipenda Mungu atathibitisha neno lake kupitia hicho kitu.
2. Nikamuuliza ninawezaje kumleta mtu mzima katika kipindi Cha MAFUNDISHO?
Alinijibu kwa kuniuliza swali ya kuwa mtu mzima anapenda nini? Nikamjibu, Naye akaniambia ya kuwa katika hicho kitu ambacho mtu mzima anakipenda Mungu atathibitisha neno lake kupitia hicho kitu.
Kweli nilipoanza kufundisha kumekuwa na maajabu mengi na watu tofauti tofauti ninaowafundisha wameshuhudia wenyewe kwa macho yao.
Kuna wakati hata nilipokuwa nawafundisha watoto katika masomo ya kawaida ambayo si ya neno la Mungu, Mungu alidhihilisha uwepo wake. Mfano zaidi ya utumishi wa Mungu niliopewa Mimi Ni mwalimu wa somo la jeografia. Mfano siku moja nilikuwa nikifundisha kidato Cha kwanza, na nilikuwa naelezea kuhusu mchora ramani ghafla Kuna watoto kadha wakaniambia tumeona Jambo Fulani ulipokuwa unaelezea.
Kwa maneno mengine naweza sema Mungu anajithibitisha mwenyewe kwa kazi zake na maajabu yake ambayo kwa akili za kibinadamu huwezi kuelezea mfano.
1. Kuna watu walikufa na wakafufuliwa katika ulimwengu huu ( je wanasayansi wanaweza wakatuelezea kisayansi ni mechanism gani inatumika kufua wafu) mtu amekufa vipimo vimethibitisha kwa siku tatu lakini mtu akafufuliwa. Rejea kitabu kimoja kinaitwa (raised from the dead reinhard bonnke) pia Kuna ushahidi wa video mbalimbali kuhusu hilo
2. Vipofu waliozaliwa wakiwa vipofu wakaona
3. Wagonjwa waliothibitishwa na vipimo kuwa wagonjwa. Mfano uvimbe, HIV, kansa, kupooza, na mengine mengi yakaponywa bila dawa kwa sekunde chache tu. Hayo yamethibitishwa pia na madaktari baada ya uponyanyi kwa vipimo vya kisayansi.
Ningeweza kuandika mengi lakini si rahisi kuandika yote maana ni mengi