Nje ya Utani wetu wa Simba na Yanga huu ndiyo Ukweli wangu baada ya Draw ya CAFCL

Nje ya Utani wetu wa Simba na Yanga huu ndiyo Ukweli wangu baada ya Draw ya CAFCL

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,685
Reaction score
128,178
Kama Yanga SC watatulia na Kujipanga vyema kwa Nyumbani na Ugenini watapata Alama kati ya 10 au 12 hivyo Kuvuka vizuri katika Kundi lao.

Kwa hili Kundi la Simba SC hasa baada ya kuiangala Simba SC yangu Kiufundi na kuziangalia RS Berkane na Orlando Pirates naina Simba SC kumaliza na Alama kati ya 7 au 8 hivyo Kutokuvuka.

Namaanisha nini kwa Yanga SC?

Yanga SC atashinda Mechi zake zote 3 za Tanzania ambazo ni Alama 9 kisha Yanga SC wanaweza ama kutoa Sare Mechi moja Ugenini au hata Kushinda moja Ugenini hivyo kuwa na jumla ya Alama kati ya 10 au 12.

Namaanisha nini kwa Simba SC?

Naiona Simba SC kushinda Nyumbani Mechi moja na Wakameruni kisha kutoka Sare Mechi moja Nyumbani na Kufungwa Mechi moja Nyumbani ambazo ukijumlisha hapa unapata Alama 4 za Nyumbani.

Naiona tena Simba SC kushinda Mechi ya Ugenini dhidi ya Wakameruni kisha ama kutoka Sare Mechi moja ya Ugenini au hata Kufungwa zote za Ugenini hivyo kwa ujumla Simba SC kupata Alama kati ya 7 au 8 tu katika Kundi lake.

Hata hivyo katika Mpira lolote laweza kutokea kwani Bahati nayo ina sehemu yake kubwa tu katika Mpira ila kwa Jicho langu la Sayansi ya Mpira na Ufundi wake siioni Simba SC yangu ikivuka..

Kila la kheri kwa Timu zote huko CAFCL.
 
Yanga SC inavuka, ila nina wasiwasi na Simba SC yangu kama itavuka kwani tusizuge hawa RS Berkane na Orlando Pirates ni mfupa mgumu kwetu labda Bahati/ Nyota tu itubebe.
yanga akikaa kizembe havuki, anatolewa jasho la mashujaa, t.r.a aje avuke kizembe kwa waarabu

nyau nae akibaki anajiona yuko vzr bila jitihad za nguvu hata amini kitakacho mkuta.
 
Huu ni utabiri!..Kwa sababu kwa current form,aina ya uchezaji,utulivu katika timu na aina ya wapinzani wanaokutana nao. Simba ana nafasi zaidi, kashakutana na orlando japo ni muda ila angalau anajua aina yake, berkane pia wamekutana mara 4 kwa misimu ya hapa karibuni.huyo colombe ni mgeni katika makundi so hasumbui pia.

Yanga walikutana na timu kama hizi msimu uliopita ila walau walikuwa na nafuu.wale walikuwa na uwezo zaidi ya hizi timu za sasa lakini Yanga yenyewe ina hali gani!...wakirekebisha shida zao katikati ya kiwanja, wachezaji wakaacha utozi wanaweza kufanikiwa.
 
yanga akikaa kizembe havuki, anatolewa jasho la mashujaa, t.r.a aje avuke kizembe kwa waarabu

nyau nae akibaki anajiona yuko vzr bila jitihad za nguvu hata amini kitakacho mkuta.
Kumbe mpaka akae kizembe. Lol.

Hizi kauli hamkawii kuzikimbia mwisho wa siku. Kuwashauri ongeeni kiasi msijimalize mkashindwa kuandika siku mambo yakienda ndivyo sivyo.
 
Kumbe mpaka akae kizembe. Lol.

Hizi kauli hamkawii kuzikimbia mwisho wa siku. Kuwashauri ongeeni kiasi msijimalize mkashindwa kuandika siku mambo yakienda ndivyo sivyo.
Mimi baada ya mechi ya kwanza ndio nitatoa utabiri In Shaa Allaah 😆
 
Huo ndio ukweli, yataburuza mkia , hawana mpira kabisa , yanga hii ni mbovu kuliko zote.
Mambo yanabadilika, Yanga ya mwaka Jana ya Folz na Pedro ilikuwa tia maji sana ila ikalosa padogo kufuzu makundi tena kizembe mbele ya miamba katika kundi la kifo .

Kuna Simba mbovu sana iliwahi kufuzu makundi na ilimpigan7 horoya

Mechi za CAF usiriazi unaongezeka hata bonus za ushindi zinakuwa kubwa sana
 
Back
Top Bottom