Nje ya Utani wetu wa Simba na Yanga huu ndiyo Ukweli wangu baada ya Draw ya CAFCL

Nje ya Utani wetu wa Simba na Yanga huu ndiyo Ukweli wangu baada ya Draw ya CAFCL

Mambo yanabadilika, Yanga ya mwaka Jana ya Folz na Pedro ilikuwa tia maji sana ila ikalosa padogo kufuzu makundi tena kizembe mbele ya miamba katika kundi la kifo .

Kuna Simba mbovu sana iliwahi kufuzu makundi na ilimpigan7 horoya

Mechi za CAF usiriazi unaongezeka hata bonus za ushindi zinakuwa kubwa sana
Acha kulinganisha simba na vitu vya hovyo
 
Wote Simba na Yanga hawana malengo kwa hiyo kuvuka kwao kwenda robo ni kudra tu za Mungu labda ziwasaidie. Yanga kauza Okello halafu kaleta Chekature. Hao Simba wana Doumbia ambaye kila mechi lazima apangwe wakati Mgunda kamzidi mara mia anaozea benchi. Nafasi tano za wazi mshambuliaji wa kimataifa anakosa zote halafu wapuuzi wanasema wanaenda kuchukua ubingwa wa CAF. Kwenye CAF CL timu ikipata nafasi za wazi mara nyingi ni mbili zikizidi huwa ni tatu ndani ya dakika 90 kwa hiyo ukishindwa kuitumia hata moja ndio basi tena subiri mechi ijayo.

Na mbaya zaidi mashindano yanaanza mapema kabla dirisha dogo halijafunguliwa sasa si balaa hilo. Kiufundi Simba kama wakihitaji kufanya vizuri lazima waongeze mshambuliaji wa kati, kiungo mkabaji namba sita na ikiwezekana hata golikipa asajiliwe mwingine huyo aliyepo asepe. Yanga nao mahitaji makubwa ni beki wa kati, kiungo mkabaji kama Aucho, kiungo mshambuliaji na mshambuliaji wa kati. Na kubwa kabisa Yanga wanahitaji kocha mkubwa mwenye uwezo wa kuwasimamia wachezaji bila kuingiliwa na viongozi maana tuhuma alizotoa kocha aliyeondoka kuwa kuna wachezaji hawafiki mazoezini halafu viongozi hawachukui hatua sio tuhuma ndogo.

Mwisho nawakumbusha tu mashabiki wanaoshangilia timu zao kwa kuangalia tu zimepangwa na timu gani kwenye makundi yao. Mpira haupo jinsi wanavyofikiria wao na timu huwa zinabadilika kutegemeana na makocha na wachezaji wanaowasajili. Hivyo ni vyema wasubiri mashindano yaanze ndio waanza kushangilia.
 
Yanga inabidi apambane zaidi na MC Alger maana Zamalek ana nafasi kubwa ya kufuzu kulingana na ubora wake, Simba inabidi apambane na Orlando ambaye kimsingi amemzidi Simba vitu vingi
Anyway, Yanga bingwa
 
Kama Yanga SC watatulia na Kujipanga vyema kwa Nyumbani na Ugenini watapata Alama kati ya 10 au 12 hivyo Kuvuka vizuri katika Kundi lao.

Kwa hili Kundi la Simba SC hasa baada ya kuiangala Simba SC yangu Kiufundi na kuziangalia RS Berkane na Orlando Pirates naina Simba SC kumaliza na Alama kati ya 7 au 8 hivyo Kutokuvuka.

Namaanisha nini kwa Yanga SC?

Yanga SC atashinda Mechi zake zote 3 za Tanzania ambazo ni Alama 9 kisha Yanga SC wanaweza ama kutoa Sare Mechi moja Ugenini au hata Kushinda moja Ugenini hivyo kuwa na jumla ya Alama kati ya 10 au 12.

Namaanisha nini kwa Simba SC?

Naiona Simba SC kushinda Nyumbani Mechi moja na Wakameruni kisha kutoka Sare Mechi moja Nyumbani na Kufungwa Mechi moja Nyumbani ambazo ukijumlisha hapa unapata Alama 4 za Nyumbani.

Naiona tena Simba SC kushinda Mechi ya Ugenini dhidi ya Wakameruni kisha ama kutoka Sare Mechi moja ya Ugenini au hata Kufungwa zote za Ugenini hivyo kwa ujumla Simba SC kupata Alama kati ya 7 au 8 tu katika Kundi lake.

Hata hivyo katika Mpira lolote laweza kutokea kwani Bahati nayo ina sehemu yake kubwa tu katika Mpira ila kwa Jicho langu la Sayansi ya Mpira na Ufundi wake siioni Simba SC yangu ikivuka..

Kila la kheri kwa Timu zote huko CAFCL.
Sijui itaishaje ila naona yanga yupo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kwenda robo kuliko simba, Naunga mkono maelezo yako.
 
mm nachojua huko CAF script ni ile ile tu kama ya msimu ulopita kwa yanga, kwasababu bado uongozi wa yanga umefanya makosa yale yale kama ya msimu ulopita, uzuri wa msimu ulopita walitoka makundi walau wakaambulia ubingwa ila msimu huu wanakosa vyote.
 
mm nachojua huko CAF script ni ile ile tu kama ya msimu ulopita kwa yanga, kwasababu bado uongozi wa yanga umefanya makosa yale yale kama ya msimu ulopita, uzuri wa msimu ulopita walitoka makundi walau wakaambulia ubingwa ila msimu huu wanakosa vyote.
Yanga anacheza robo bila shida, mziki upo kwa simba
 
Back
Top Bottom