Kama Yanga SC watatulia na Kujipanga vyema kwa Nyumbani na Ugenini watapata Alama kati ya 10 au 12 hivyo Kuvuka vizuri katika Kundi lao.
Kwa hili Kundi la Simba SC hasa baada ya kuiangala Simba SC yangu Kiufundi na kuziangalia RS Berkane na Orlando Pirates naina Simba SC kumaliza na Alama kati ya 7 au 8 hivyo Kutokuvuka.
Namaanisha nini kwa Yanga SC?
Yanga SC atashinda Mechi zake zote 3 za Tanzania ambazo ni Alama 9 kisha Yanga SC wanaweza ama kutoa Sare Mechi moja Ugenini au hata Kushinda moja Ugenini hivyo kuwa na jumla ya Alama kati ya 10 au 12.
Namaanisha nini kwa Simba SC?
Naiona Simba SC kushinda Nyumbani Mechi moja na Wakameruni kisha kutoka Sare Mechi moja Nyumbani na Kufungwa Mechi moja Nyumbani ambazo ukijumlisha hapa unapata Alama 4 za Nyumbani.
Naiona tena Simba SC kushinda Mechi ya Ugenini dhidi ya Wakameruni kisha ama kutoka Sare Mechi moja ya Ugenini au hata Kufungwa zote za Ugenini hivyo kwa ujumla Simba SC kupata Alama kati ya 7 au 8 tu katika Kundi lake.
Hata hivyo katika Mpira lolote laweza kutokea kwani Bahati nayo ina sehemu yake kubwa tu katika Mpira ila kwa Jicho langu la Sayansi ya Mpira na Ufundi wake siioni Simba SC yangu ikivuka..
Kila la kheri kwa Timu zote huko CAFCL.