Njia 10 za Uchumba Salama

Njia 10 za Uchumba Salama

Saint Anne

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2018
Posts
76,039
Reaction score
230,142
Habari!

Natumaini wote ni wazima na namshukuru Mungu juu ya kila mmoja wetu. Natamani kushare nanyi mambo haya machache muhimu katika Uchumba;

1. Usiweke agano na mchumba.
Kuna Watu huwa wanajiapiza eti nisipokuoa/nisipoolewa na wewe bora nife kuliko kuoa/kuolewa.
Maagano ya namna hii yamewagharimu wengi.

Maandiko yanatambua agano la ndoa na si la uchumba.Acha mpango wa Mungu usimame kwenye uchumba wenu.

2. Usizae na mchumba ili akuoe.
Hii huwakumba Sana wadada. Wengi huingia kwenye huu mtego kwa kudanganywa na kuambiwa nizalie kwanza mtoto ndipo nikuoe.

Pia, kuna wadada hujitegesha. Kuna wadada hujitegesha wenyewe wapate mimba wakidhani watapendwa zaidi.
Wengi wamezalishwa na kutelekezwa.

3.Usioe/kuolewa na mtu asiyemcha Mungu.
Moyo wa mtu asiyemcha Mungu hauna hofu ya kitu chochote ndani yake.kufanya Jambo lolote kwako siyo tatizo kwake maana moyoni mwake hakuna hukumu.

4. Usikubali kuoa/kuolewa na mtu aliyekuwa kwenye ndoa tayari na ndoa ile ikavunjika na wewe ukataka kuingia naye kwenye ndoa bila kujua sababu za ndoa yake ya mwanzo kuvunjika.

Ni vema ukajua sababu kupitia kutafuta taarifa kwa watu wengine na si kwake maana atakudanganya.

5. Uchumba usiwe Siri.
Unaweza kujikuta unaoa/unaolewa na mume au mke wa mtu bila kujua.

6. Usioe au kuolewa na mtu kwa sababu unamhurumia.
Ni kweli kaonyesha upendo, Ni kweli anakujali lakini Je! huyo mtu yumo moyoni mwako? Unampenda? Au unajilazimisha kwa sababu ya zawadi anazokupa.

Ndoa nzuri ni ile ya watu wawili wanapendana na si ya upande mmoja.

7. Msichukuane kienyeji.
Ndoa Ina taratibu zake na taratibu hizo zina baraka zake. Usijiweke kwenye mazingira ya kuibiwa usiku.

8. Acha kujiaminisha Sana kwamba utamuoa au utaolewa naye.
Kumbuka uchumba siyo ndoa. Lolote linaweza kutokea Kama siyo upande wako basi upande wake. Ruhusu mpango wa Mungu utimie na si utashi wako.

9. Epuka kumhonga mchumba vitu vya thamani kubwa, kumsomesha nk.
Usiwekeze Sana kwa mchumba. Lakini Kama unadhani uchumba ukivunjika hutaumia mpe ila Kama unaona uchumba ukivunjika utaumia usimpe.

Simaanishi wachumba wasisaidiane, kuna viwango vya kusaidiana wachumba. Mengine hayo ukitaka kuyafanya weka ndani.

10. Usizini.
Tendo la ndoa ni kwa wanandoa na ndiyo maana linaitwa tendo la ndoa na si tendo la uchumba. Ukiona mchumba anataka tendo hili kwa Kasi kubwa huku akikwambia siwezi kuuziwa mbuzi kwenye gunia jua huyo hana mpango wa ndoa.

Niwatakie siku njema
 
Asante kwa ujumbe mzuri. Wasisitize waweke mkazo zaidi hapo namba 10. Wasiachie kabisa. Itawasaidia sana. Ila kama walishaachia mwanzo waendelee tu kama usichana wao ulishapotea.
 
Huwezi kuniliza.
Ongea tu unachoona ni sawa..nipo kujifunza
Namba 3 napinga Tena Sana tu!
Mtu ni saikolojia na saikolojia ya mtu ndio huwa inaamua imani yake.. ndio maana wengi wakikua hubadili dini n.k kutokana na alivyoona yeye!.. humanity still there mama Zama ndani ujue in deeply humanity utaelewa naandika nini.. usiangalie mtu anaamini nini tu bali upi msingi wake wa kuamini..??

Ipi afadhari ya kuishi na mtu anaamini ktk Mungu lkn akili kichwani nusu kafata imani kwa kuwa amekuta hivyo tu.. kwangu kuishi na mtu muelewa Kuna maana kubwa Sana!.. unaweza usinielewe.

Namba 4
Kuna watu wameishi na ninaushuhuda huo toka 2006 mpk leo wapo fresh tena naweza sema nimejifunza mengi kutoka kwao maana changamoto walizopitia he he he..😅

Usikariri maisha

Narudi
 
Namba 3 napinga Tena Sana tu!
Mtu ni saikolojia na saikolojia ya mtu ndio huwa inaamua imani yake.. ndio maana wengi wakikua hubadili dini n.k kutokana na alivyoona yeye!.. humanity still there mama Zama ndani ujue in deeply humanity utaelewa naandika nini.. usiangalie mtu anaamini nini tu bali upi msingi wake wa kuamini..??

Ipi afadhari ya kuishi na mtu anaamini ktk Mungu lkn akili kichwani nusu kafata imani kwa kuwa amekuta hivyo tu.. kwangu kuishi na mtu muelewa Kuna maana kubwa Sana!.. unaweza usinielewe.

Namba 4
Kuna watu wameishi na ninaushuhuda huo toka 2006 mpk leo wapo fresh tena naweza sema nimejifunza mengi kutoka kwao maana changamoto walizopitia he he he..[emoji28]

Usikariri maisha

Narudi
Binafsi yangu katika hiyo point imani kwa Mungu ni lazima.
Maandiko yananiagiza nisifungiwe nira na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa.
Kama ikitokea nitakuwa naye Kuna sehemu inafundisha pia namna ya kuishi na mtu wa namna hiyo.
Hapo nimeongelea imani tu,sijaongelea kiwango Cha hiyo imani.

Hiyo point #4 naomba uisome Hadi mwisho.
Nimesema kwamba usioe/usiolewe na mtu ambaye ndoa yake imevunjika unless umejua sababu za ndoa hiyo kuvunjika.
Hujamalizia kusoma hiyo point au umeisoma kwa haraka.
Ni kweli kuna ndoa za namna hiyo zipo na zinadumu lakini asilimia kubwa huwa mwisho wake ni matatizo na huvunjika tena.
 
Back
Top Bottom