Charlz ze son conscious
JF-Expert Member
- Aug 22, 2019
- 554
- 848
Mchumba anasomeshwa chuo cha biblia tu otherwise utakua unayumba!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unawezaje kutekeleza yote hayo bila kupata ile kitu? Usisikie kuna wanaume makatili sababu huwa ni hizi, imagine wewe ni mwanaume na umetekeleza hayo yote ikiwemo namba kumi na mwisho wa siku anaenda kwa mwingine utakua katika hali gani? Nisijiwekee matumaini ya kumuoa,asiwe na mpango wa kuzaa na mimi n.k lakini bado tusiwe na usiri,amekua mama yangu mzazi au? Huo muda nitakaopoteza kwake si ni bora ningeutumia kutafuta pesa za ziada...mwisho wa siku atakutangaza shoga huyuNimeharibu kivipi mkuu?
Siwezi msahau mkuu🤣🤣Usisahau kumshirikisha Baharia wa Buza
😎Nina mume
Habari!
Natumaini wote ni wazima na namshukuru Mungu juu ya kila mmoja wetu.
Natamani kushare nanyi mambo haya machache muhimu katika UCHUMBA;
1.Usiweke agano na mchumba.
Kuna Watu huwa wanajiapiza eti nisipokuoa/nisipoolewa na wewe bora nife kuliko kuoa/kuolewa.
Maagano ya namna hii yamewagharimu wengi.
Maandiko yanatambua agano la ndoa na si la uchumba.Acha mpango wa Mungu usimame kwenye uchumba wenu.
2.Usizae na mchumba ili akuoe.
Hii huwakumba Sana wadada.Wengi huingia kwenye huu mtego kwa kudanganywa na kuambiwa nizalie kwanza mtoto ndipo nikuoe.
Pia kuna wadada hujitegesha. Kuna wadada hujitegesha wenyewe wapate mimba wakidhani watapendwa zaidi.
Wengi wamezalishwa na kutelekezwa.
3.Usioe/kuolewa na mtu asiyemcha MUNGU.
Moyo wa mtu asiyemcha Mungu hauna hofu ya kitu chochote ndani yake.kufanya Jambo lolote kwako siyo tatizo kwake maana moyoni mwake hakuna hukumu.
4.Usikubali kuoa/kuolewa na mtu aliyekuwa kwenye ndoa tayari na ndoa ile ikavunjika na wewe ukataka kuingia naye kwenye ndoa bila kujua sababu za ndoa yake ya mwanzo kuvunjika.
Ni vema ukajua sababu kupitia kutafuta taarifa kwa watu wengine na si kwake maana atakudanganya.
5.Uchumba usiwe Siri.
Unaweza kujikuta unaoa/unaolewa na mume au mke wa mtu bila kujua.
6.Usioe au kuolewa na mtu kwa sababu unamhurumia.
Ni kweli kaonyesha upendo,Ni kweli anakujali lakini je!huyo mtu yumo moyoni mwako?unampenda? Au unajilazimisha kwa sababu ya zawadi anazokupa.
Ndoa nzuri ni ile ya watu wawili wanapendana na si ya upande mmoja.
7.Msichukuane kienyeji.
Ndoa Ina taratibu zake na taratibu hizo Zina baraka zake.
Usijiweke kwenye mazingira ya kuibiwa usiku.
8.Acha kujiaminisha Sana kwamba utamuoa au utaolewa naye.
Kumbuka uchumba siyo ndoa.Lolote linaweza kutokea Kama siyo upande wako basi upande wake.
Ruhusu mpango wa Mungu utimie na si utashi wako.
9.Epuka kumhonga mchumba vitu vya thamani kubwa ,kumsomesha nk.
Usiwekeze Sana kwa mchumba.
Lakini Kama unadhani uchumba ujivunjika hutaumia mpe,ila Kama unaona uchumba ukivunjika utaumia usimpe.
Simaanishi wachumba wasisaidiane,Kuna viwango vya kusaidiana wachumba.
Mengine hayo ukitaka kuyafanya weka ndani.
10.Usizini.
Tendo la ndoa ni kwa wanandoa na ndiyo maana linaitwa tendo la ndoa na si tendo la uchumba.
Ukiona mchumba anataka tendo Hili kwa Kasi kubwa huku akikwambia siwezi kuuziwa mbuzi kwenye gunia jua huyo hana mpango wa ndoa.
Niwatakie siku njema
[emoji3][emoji41]
Akutangaze shoga!!Unawezaje kutekeleza yote hayo bila kupata ile kitu? Usisikie kuna wanaume makatili sababu huwa ni hizi,imagine wewe ni mwanaume na umetekeleza hayo yote ikiwemo namba kumi na mwisho wa siku anaenda kwa mwingine utakua katika hali gani? Nisijiwekee matumaini ya kumuoa,asiwe na mpango wa kuzaa na mimi n.k lakini bado tusiwe na usiri,amekua mama yangu mzazi au? Huo muda nitakaopoteza kwake si ni bora ningeutumia kutafuta pesa za ziada...mwisho wa siku atakutangaza shoga huyu
Ntakusaidia kutubu..😅[emoji3]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ntakusaidia kutubu..[emoji28]
SawaAiseee
Ukifata hayo uliyoandika amna atakayekuoa
Bwana ajua..😅[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwani nimekosea wapi?
Sasa imagine mmedumu pengine miezi sita tu katika misingi hiyo na mnakuja kosana kwa kashfa, what will happen.... chukulia madada wa siku hizi na uhalisia wenuAkutangaze shoga!!
Atakuwa ameyumba
Niache mimi[emoji23]Bwana ajua..[emoji28]
Uhalisia wetu upi?Sasa imagine mmedumu pengine miezi sita tu katika misingi hiyo na mnakuja kosana kwa kashfa,what will happen....chukulia madada wa siku hizi na uhalisia wenu
Akhsante sana mkuuAhsante nimefurahi pia,ila kama jimbo liko wazi embu nijulishe tuyajenge unaweza kuwa malaika niliyekuwa na namngoja...
Naongozwa na kitabu cha Mithali kama kijana so utakuwa unanifahamu vyema Saint Anne.