Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Ukiwa na mwanamke mwenye furaha ni raha sana ndani.
Vitu vinakua rahisi, pia utaweka nguvu zako kwenye kazi/ biashara kwa amani. Raha ya upendo wa dhati. Wote mnakua mpo kwa ajili ya kuhakikisha mwenzio ana furaha. Wengi hudhani mwanamke anakua tu ivo bila kushughulika.
Lakini ukweli ni kuwa wewe ndio kiongozi. Wao wanafata vile wanaongozwa na wewe.
Kama umeweka mahusiano ya malalamishi utayapata kwa wingi.
Kama umeweka mahusiano ya kuchuniana, utachuniwa.
Kama umejiwekea kuwa wanawake hawaeleweki, pia utapata mahusiano yasiyoeleweka.
Sasa baada ya kuwa na huyo mwanamke na kujihakikishia kuwa huyo ndo unataka kuwa naye maishani, usisite kufanya haya.
.
Kumtoa out, kumfurahisha, kumpeti na kumfurahisha kitandani.
Usibweteke kwenye mahusiano kama mwanaume.
Msiwe tu pamoja sababu mna watoto au jamii inajua nyie ni wapenzi. Msiishie hapo. Lazima mfanye mambo yanayofanywa na wapenzi ili mfurahi zaidi.
Lazima uhakikishe furaha ya mwanamke wako ipo na inaongezeka.
Kumbuka mwanamke ameumbwa kupokea, jitoe bila kuchoka.
Umsifie mara kwa mara. Umshukuru pia kwa mambo mbalimbali.
Badilisha naye mazingira mara kwa mara. Ili kusiwepo na mazoea.
Lakini ujue hata kama unamchekesha vipi, au unampeleka wapi kama hamfanyi mapenzi ni bure.
Hivyo ni muhimu pia kuhakikisha unamfurahisha katika sekta ya kitanda.
.
Kuwa na mawasiliano mazuri.
Mawasiliano hujenga au hubomoa.
Usikubali kuwa na malumbano zaidi ya mazungumzo ya furaha.
Wote mtajikuta na hasira mnaishia kununiana. Sio jambo zuri. Unaweza sema unamkomoa lakini unajikomoa mwenyewe.
Hivyo hakikisha mnaongea vizuri. Mnatatua changamoto zenu kwa amani. We ndo kiongozi, ukimuachia mwanamke hilo jambo utajikuta unaenda na mudi zake.
Kama unaona we ni mbovu kwenye mawasiliano anza kujifunza taratibu.
Mana kila saa kulalamikiana haipendezi.
Kumbuka wanawake wameumbwa ni waongeaji, mruhusu aongee zaidi yako.
Usimkatishe katishe. Usitake kuwa sahihi muda wote.
Muda mwingine anachohitaji ni sikio lako tu, wala sio maoni yako.
Pia kama unaona mwanamke wako anajambo anataka kulisema alafu akakuambia “haina shida kila kitu kipo sawa”, usikubali endelea kumuuliza mpaka akuambie kinachomsumbua. Ukifanya hivyo ataona unamjali.
.
Kumsoma ishara zake za mvuto.
Hili ni la muhimu ili ujue ufanye nini.
Wanawake huongea kwa ishara kwanza. Japo wengi husoma ishara za mwanamke na kutafsiri vibaya, na kupelekea mahusiano kuvunjika. Mara nyingi ataanza kukupa ishara kadhaa, akishachoka na kuona huelewi ishara ndo atakuambia kwa maneno. Lakini hadi muda huo unafika tayari ameshakata tamaa na mahusiano yenu.
Mfano;
Kama zamani alikua anataka kukushika kila saa lakini sasa hataki hata msogeleane, maana yake mvuto wako kwake umepungua. Hivyo fanya vile vitu ulivokua unamfanyia zamani/ kipindi alichokua anakupenda sana.
Kama alikua anakutafuta mara 3 kwa siku kwenye simu lakini sasa inapita wiki mawasiliano mabovu, maana yake kuna sehemu umelega mpaka hana hamu sana na wewe. Hivyo fanya yale uliyokua unamfanyia mpaka akawa anakupigia mara 3 kwa siku.
Kama mpo vizuri lakini ghafla amenuna, ni ishara kuna kitu kimemkwaza hivyo ni kazi yako kumfanya afunguke ujue shida na myamalize muendelee kufurahi.
Wakati unafanya ivo usifanye ili kumfurahisha yeye tu, fanya kwa kufurahia pia. Kwa ajili ya afya yako pia ili usinung’unike. Kama unaona hutoweza kumfanyia yote hayo ili kudumisha upendo bora umwache akapate mtu anayeweza kumfurahisha kuliko kuwa kwenye nyumba yenye manung’uniko.
Na wewe pia ufanye hivyo kwa mwanamke anayekufaa na ambaye mnaendana. Kiurahisi unaweza kujua mwanamke ambae atakufaa mapema kwa kumuuliza maswali mazuri na kuongea mada zitakazokusaidia kumjua zaidi.