rakeyescarl
JF-Expert Member
- Dec 9, 2007
- 481
- 147
Mtoto wangu alifaulu vizuri sana kidato cha 4 na kwenda shule nzuri sana kidato cha 6 na tukakubaliana kuwa akimaliza kidato cha 6 atakwenda chuo bara lolote anapotaka yeye. Ghafla baada ya muhula wa kwanza akabadirika anasema anataka kwenda kwenye chuo kiko SA. Na amekwishajaza makaratasi na amekubaliwa. Imebidi nivute subira, nimemwambia nitamjibu, ingawa nilikuwa naelekea kumbeba na kwenda kumpeleka shuleni kwake kwa nguvu kwani naona shule yake wana pass kwa 90% au zaidi. Nitashukuru kama nitapata ushauri hapa, natanguliza shukurani.