strong star
Member
- Jul 15, 2021
- 36
- 42
Je, wangapi unawajua wametimiza ndoto zao '?, Na wewe kama wewe ulishiliki vipi kuzitimiza '? ,Na pia ni wangapi unawafaham hawajatimiza ndoto zao na wameshakata tamaa katika kutimia kwa ndoto hizo '?, Na ni wangapi mpaka leo bado wanapambana ili kufikia na kutimia kwa ndoto zao ,na wewe unashiliki vipi katika kusaidia kutimia kwa ndoto hizo '? Mwisho ni wangapi unawaona wanahangaika na kutapata kwa kuishi na manung'uniko kwani ufanya kazi ambazo sio ndoto zao '?,
Njia na malezi bora kuelekea kutimia kwa ndoto za walio wengi katika jamii,
*kuwa na ndoto matalajio.
Kwanza yatupaswa kuwa na ndoto juu ya kile tunachopenda na kukifurahia zaidi kufanya , kisha
Moja : Nafasi ya mzazi/ mlezi .
Mzazi au mlezi anapaswa kuitambua ndoto ya mtoto wake ,kumtambulisha na kumfahamisha zaidi juu ya ndoto yake ,kuendelea kumtamanisha zaidi na kumuwekea hamasa katika kutimia kwa ndoto yake .
Pili: Nafasi ya jamii,
Jamii ikiwa ni sehemu kubwa ya malezi ya watoto wetu hivyo yapaswa kuitambua ndoto ya mtoto, kuiheshim na kuuthamini ,kuzidi kumpa moyo na kumuongezea hamasa katika kutimiza ndoto yake kwa kuwa "kidole kimoja hakivunji chawa pia umoja ni nguvu " tukishilikiana kwa pamoja tutatimiza ndoto za walio wengi .
Tatu: Serikali na Sera zake.
Serikali yapaswa kuhakikisha kutimia kwa ndoto za walio wengi kwa ushirikiano kutoka katika jamii na kuweka Sera rafiki zaidi , wazazi na mtu nwenyewe, kutengeneza mazingira rafiki katika kutimia kwa ndoto hizo, kutambua mchango chanya kwa watakao timiza ndoto zao.
*Ishi ndani ya ndoto yako.
Yakupasa kuishi ukilinda na kusimamia matakwa yako juu ya kutimia kwa ndoto yako kwani uko ndiko iliko amani na utulivu wa moyo wako, kwa mfano ikiwa una ndoto za kuwa mwanajeshi hivyo basi ya kupasa kuishi tangu ukiwa mdogo katika misingi ya kuwa mwanajeshi kwa kutojichora maandishi mwilini mwako, kutojiingiza katika matendo ya kialifu ,nakadhalika ili kutimiza ndoto yako.
*Elimu kuelekea ndoto yako.
Ni wajibu wa mzazi au mlezi katika kuitambua,kumuelimisha na kumfafanulia njia bora na sahihi zaidi kijana wake kuelekea kutimia kwa ndoto yake ili aweze kupata elimu staiki na kutimiza ndoto, kwa mfano unataka kuwa tabibu hivyo basi unapaswa kuipenda na kujitoa katika masomo ya sayansi kwani ndio njia sahihi kuelekea kutimia kwa ndoto yako.
*Kujitoa na juhudi zako katika safari ya ndoto zako.
Yakupasa kuweka juhudi jadidi na yakinifu kwani kuna wakati utapitia changamoto na misukosuko ya hapa na pale katika kuelekea ndoto zako, kikubwa kuto kata tamaa na kuonyesha msimamo wako zaidi tena kwa vitendo na sio maneno tu ,kwani ata waswahili usema "maneno tupu hayavunji mfupa ".
*Mwisho usimsahau Mungu katika safari ya ndoto zako kwani yeye ndie mpaji wa vyote tuvitakavyo na tuvipendavyo katika maisha yetu.
Kumbuka na uishemu kila hatua yako kuelekea ndoto zako kwani inathamani na ni muhimu katika safari yako, NDOTO YAKO NDIO FURAHA YAKO ya maisha yako yote hapa duniani, tulizo la nafsi na maendeleo ,Hivyo basi USICHEZE NA NDOTO YA MWENZAKO kama usivyopenda kuchezewa ya kwako na pia penda na furahia ukishiliki katika kutimiza ndoto ya mtu hivyo itakuwa rahisi kutimiza ya kwako.
Ahsante .

Upvote
2