Ni hiari yao, lakini watanzania sio wajinga kama walivyotaka tufikirie kuwa kweye zile vurugu serikali ndiyo iliyokosea.
Watanzania wanamuona Samia kama Mama Shupavu aliyesitisha uangamizaji wa miundombinu ya taifa na mali za watu. Mama Samia leo hii angelaumiwa sana kupita kiasi kama angeshindwa kuilinda nchi nchi isiungue, hakuna ambae angemwelewa. Watanzania wengi mpaka leo hawajui malengo ya chadema yalikuwa kuharibu nini na nini kwa kiwango gani, hasa baada ya kuona wameunguza vituo vya polisi, ofisi za serikali, vituo vya mwendokasi, ATM, TRA, petrol stations, mahakama, mabaa, maduka ya watu na wizi wa kila aina. Watanzania bado wanajiuliza maswali kama ingekuwaje kama vituo vyote vya polisi, vituo vyote vya mwendokasi, ofisi zote za serikali na TRA zote, shule na hospitali za serikalli nchini vingeunguzwa. Hali yetu ya kiuchumi, huduma za kijamii, uslama na kisiasa vingekuwaje.
Je, hata kama chadema kingeingia madarakani ndiyo ingejenga ofisi nyingine, vituo vya polisi vingine, TRA nyingine, mahakama, shule, hospitali na barabara nyingine kwa fedha ipi kutoka wapi?
Ukweli chadema wamewakosea watanzania. Dhambi hii itawatafuna sana na haiwezi kufutika kwa kusema na kuandika sana mitandaoni; wametukosoa. Mama samia ni mmoja tu, na miundombinu mingine nae aliikuta tu na ataiacha; huwezi kuchoma mali za watanzania wote kwa kisingizio cha Mama Samia. Watanzania sio mazuzu wa kiasi hicho, hwatabaki salama. haiwezekani.