Kazi ya ****** ni kutoa uchafu lakini ukisha tanuka ****** unavujisha akili na ndicho kinacho kusumbuaWatanzania sio wajinga, wanajua kuwa chadema ndio waliharibu mali, maisha na utaratibu wao mzima siku ya na baada ya uchaguzi. Wananchi sio wajinga wa kushindwa kujua kwamba no reforms no election ya chadema ndio chanzo cha wapendwa wao kufa, kuumia na mali zao kuharibiwa. Watanzania wa leo wanafahamu kuwa mali iliyoharibiwa haikuwa ya Samia wala CCM bali ni mali yao watanzania inayowafaa watanzania na iliyotokana na kodi na nguvu zao.
Watanzania leo hii wanaziita vurugu zile kwa jina "vurugu za chadema". Mfano, niliwasikia wananchi wa Gongolamboto wanaohangaika kutafuta wapi ofisi zao za serikali za mtaa na Kata zilihamishiwa kwa sasa baada ya kuchomwa pale gongolamboto wakisema "baada ya vurugu za chadema ofisi za kata na kanda 5 zilihamishiwa Chanika kwenye kona ya Kigogo fresh". Kule Mbagala baada ya usafiri wa mwendokasi kusimama muda mfupi tu baada ya kuanza walikuwa wanalia na vurugu za chadema kurejesha adha ya usafiri Mbagala.
Chadema hata watoe maelezo gani kutaka kujitenga na zile vurugu wananchi hawatawaelewa kabisa. Wanajua chadema waliharibu mali zao, imeharibu ajira zao, imeharibu huduma zao na iliharibu mazoea yao.
Kwa watanzania, chadema sio ile tena wanayoifahamu bali watu hatari kwao. Hebu wajaribu kuitisha mkutano wa hadhara leo ili waone mwiitikio wa wananchi, hasa pale ambapo polisi watasema mkutano hauna kibali.
Hata nchi na taasisi za kimataifa zinajua kuwa chadema ndio waliofanya vurugu zile. Taasisi na jumuiya za kimataifa zina taarifa kamili kuwa chadema walichoma mali za umma na za wawekezaji binafsi utamaduni ambao hata wao hawakubaliani nao pia kwakuwa nchi hizo zinawekeza tanzania pia pamoja na watu wao. Hivyo, utamaduni wa kuiba na kuchoma mali za wawekezaji wanaona utakuja kuwagharimu hata wao wenyewe. Jumuiya na taasisi za kimataifa zinazo taarifa kamili kuwa waandamaji waliua askari wanaolinda watu na mali zao utamadunia ambao hata wao hawaukubali kwakuwa hata wao wana mali na watu wao ambao wanahitaji kulindwa na walinzi hao. Ndiyo maana malalamiko yao hayapewi attention ya kutosha, kwakuwa chadema wamefanya vitendo vya kigaidi achacho sio tu kinawaathili wenyeji lakini hata wageni pia.
Dunia nzima sasa hivi inakumbatia dialogue (kiti na meza) sio mapigano.
Chadema waombe radhi wananchi kwa kile kilichotokea la sivyo, hawana njia nyingine.