Njia pekee, rahisi na ya uhakika ya kuingia JWTZ

[

Nimekuelewa ndugu, ni kweli kabisa.Maisha siyo jeshi tuu kuna vitu Vingi vizuri Vya kufanya na kuweza kufanikiwa hata kiuchumi.TATIZO NI KWAMBA, NINAPENDA SANA KUWA MWANAJESHI NDUGU YANGU, NA ROHO (NAFSI) INAUMIA KUTOKUWA HUKO MPAKA MDA HUU.Ni basi tuu sina refa huko, YANI KWA JINSI YOYOTE AMBAVYO JESHI LIPO, MIMI NINGESHAENDA ZAMANI SANA MAANA NI KITU KINATOKA ROHONI.

QUOTE="Aleyn, post: 27170321, member: 60004"]Mkuu, mimi naamini mtu waweza kwenda JWTZ

1. Una refa wa maana, watoto wa mjini wanaita mbuyu. Wengi wanadanganyana kuwa hata watoto wa wakubwa JWTZ/TISS/CCM wanaenda kuokota mayai ya kuku JKT, hiko kitu HAKUNA.
2. Pesa, ndani ya pesa hakuna kinachoshindikana chini ya jua. Nguvu ya pesa haifanyi kazi Mbinguni tu ila hapa duniani pesa haina mpinzani.
3. Una profession ambayo ni hot cake mfano Urubani, Udaktar n.k hawa nilishuhudia kabisa hawajaenda kulima JKT. Baadhi walienda JKT kuchukua namba tu ila hata miezi 2 hawamalizi.

Mbali na hapo Mkuu mimi sina ninachokijua kama waweza penya hapo kwenda JWTZ pasipo JKT ila Mkuu mimi ninaamini maisha sio lazima uwe JWTZ tu.

Niliyoyasema hapo juu nimeyasema kutokana na mimi mwenyewe kupambana saaana kuingia katika chombo ila kwenda JKT niliambiwa na Captain aliyekuwa anasimamia kuwa nisiende sababu sasa hivi kurudi nyumbani ni kitu cha kawaida sana sana kwa wasomi.

Ili kuthibitisha niliyosema, January mwaka huu 2018 walirudi vijana kutoka JKT si chini ya 4,000 na kuna thread ilianzishwa humu juu ya hili. Tazama walioenda kama Diploma/Degree holders wanafika hata 70 kati ya 3,000 walioenda kozi JWTZ.[/QUOTE]
 
Kwahiyo Mkuu kazi mbali na Jeshi huwezi kufanya?
 
Vijana wengi wanapenda Jeshi ila asilimia kubwa wanataka watumie jeshi kama sehemu ya ubishoo wao.

Natumaini miaka ijayo kupata vijana timamu kwa ajili ya hii kazi itakuwa ngumu sana hasa idara ya usalama wa taifa (Nitaanza kumpa mwanangu Masomo ya uraia mapema ajue uzalendo aje kulitumikia taifa)
 
k
kama mtu ana ubishoo anaenda kufanya bongo fleva (ubanaji pua), avae milege, anyoe viduku, auze sura n.k ? JESHINI NI KAZI TUU, HAKUNA UBISHOO KULE.
 
Kwahiyo Mkuu kazi mbali na Jeshi huwezi kufanya?
Naweza kufanya. Hata mda huu ninafanya kazi ambayo siyo jeshi lakini nahisi kuwa na deni kubwa la kuwa mjeshi wa JWTZ. Yani hii kazi ninaifanya tuu ili mradi, naweza kusema nipo physically tuu ila mawazo yooooooooote ! NI JESHINI.
 
Tafuta kazi ya maana ufanye kijana, kazi za uaskari ni kujiandalia umaskini wa milele tu.

Umaskini na utajiri havina tafsiri maalum, kimsingi ni kufanya kitu kinachokupa furaha maishani, Kuna watoto wa wafanya biashara wakubwa ila wamegoma kurithi hizo biashara na kujifanya vitu vinavyowapa furaha, hivyo acheni kupangia watu maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…