Njia pekee ya kuiokoa CHADEMA ni Lissu kumuunga mkono Mbowe baada ya uchaguzi wao

Kwanini yeye Mbowe asipishe?
 
mbowe hawezi kushinda huu uchaguzi tupo hapa utakuja kuniambia
 
Mimi bado najiuliza mantiki ya approach ya Tundu Lissu. Kuna mtu mmoja alitoa mfano wa wanandoa, kwamba akichofanya Lissu ni sawa wanandoa wawe na mgogoro na mmoja wao achukue shuka wanalolalia, na kwenda varabarani na kusema "jamani oneni haya madoa, halafu ndiyo mnasema huyu mume/mke, kweli?" Of course, wapita njia wakiona watacheka, na kusema "ah! Nilidhani huyu ni mke/mume, kumbe hamna kitu?" Sasa je, wapita njia watalifua hilo shuka? Binafsi naamini Lissu angeweza ku'deal' na allegations za rushwa ndani ya chama chake Kwa kutumia approach tofauti, na still ange'achieve' matokeo tarajiwa. Kwenye moja ya hotuba za Lissu alisema Kwa vile SSH alikuwa makamu wa Magufuli, hawezi kujitenganisha na utawala wa bosi wake. Lakini akija kwenye chama chao, yeye anajitenganisha na uongozi wa Chadema as if hakuwa kiongozi. Hapa napata shida kuamini kuwa makamu wa mwenyekiti Chadema ni sawa na kutokuwa na makamu kabisa! How is this possible? Iko wapi collective responsibility? Yaani kwamba mafanikio ya Chadema ni ya wote, na matatizo ya Chadema ni ya Mbowe? Hapa nashindwa kuelewa kabisa!
 
Kwanini yeye Mbowe asipishe?
Kwa nini apishe, wakati Kwa mujibu wa katiba yao ana haki ya kugombea? Mimi ningeona shida iwapo Mbowe angekuja na hoja mfano ya kuondoa ukomo wa madaraka kwenye Katiba yao. Hapo ndipo tungeweza kusema "ana uchu wa madaraka". Lakini katiba yao haina kipengele cha ukomo wa madaraka, na hapakuwa na mchakato wowote wa kuuweka hadi sasa, isipokuwa mapendekezo aliyokuja nayo Lissu kama moja ya mambo atajayoshughulikia akiwa mwenyekiti. Sasa kosa la Mbowe ni nini hapa? Amekiuka Katiba ya chama au amefanya jinsi katiba yao inavyosema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…