Njia pekee ya kuleta amani Kenya ni ku-deal na Odinga bila kudekezwa

Njia pekee ya kuleta amani Kenya ni ku-deal na Odinga bila kudekezwa

Haiwezekani kumgusa BABA nyie vichwa hali jojo pambaneni na ujinga yenu ya Tizi, mambo ya Kenya yetu tuachieni wenyewe.
We know our rights na kwa taarifa yako hakuna penye wanaeza mpeleka BABA na hakuna cell ya polisi yeyote anaweza lazwa hapa Nai
Jaluo Iko na maneno mingi
 
Mambo yao waachie wenyewe...

Watu tuna maslahi binafsi na kenya wewe unaleta utoto, mwezi wa nne tunaanza msimu wa mavuno ya mahindi unataka auziwe nani, wakati penye pesa ni kenya, mwezi ya sita tunaanza karanga ya malawi kwenda kenya tukuletee wewe uwe unakula? Mwezi wa nane hadi wa 11 tunakita kambi kanda ya kati kupeleka mashudu ya alizeti kenya unataka wewe ndio uwe unayala hayo mashudu, Kikiwaka kenya ASAS anayechukua vifungashio nairobi utamtengenezea wewe aweke maziwa yake? Kenya yenye amani ndio uchumi wa east africa hasa mazao, amani ya kenya ni muhimu
 
Unajidanganya kijana odinga sio tundu lisu na Kenya sio Tz.. unafikiri kwann anaitwa baba?wanasiasa wa kizazi hiki wamepita kwenye mikono yake.

Ana wale wafuasi ambao wapo tayari kwa lolote lile atakalosema,alafu pia Kenya ipo kikabila zaidi yaani ukimlamata au kumuua Kenya haitotawalika na utakua umepuliza kipyenga cha vita ya kikabila.

Ww unafikiri viongozi wa Kenya hawana akili kwa kutomshughulikia? Wana elewa haya yote
 
Professorial Rubbish
Nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za Kenya toka enzi na enzi,

Hata wakati wa uchaguzi mkuu I told them Sikumsapot kibaki 2007 nilimuunga Mkono Odinga,

2012 nilimuunga Mkono Uhuru, kutokana na Maono ya atakapoifikisha kenya

2017 Vile vile Nilimpa sapot Kenyatta.

Baada ya kuona kuwa Kirusi cha siasa za Kenya ni Odinga

Njia pekee ni Kumficha au Kutumia ile njia ya kutomkamata Mateka, Kenya itatawalika vema,

Matatizo ya Kenya si sababu ya Rutto bali ni Mambo ya Dunia nzima

#FichaOdingaWakenyaWawenaAmani

Britanicca
 
Huu ndio ukweli nyingine ni siasa tu hua tunafanya, dunia nzima maisha yamepanda sio kenya tu, wao walitakiwa kuibana serikali yao walau waone wanatokaje kwenye mkwamo huo wa uchumi,
Kipindi Ruto anamtukana Kenyatta hakujua ni Dunia nzima Kuna mfumuko wa bei?
 
Haya ndio mambo nilikuwa namkubali JPM kwa kuchora mstari wa kudili na waganga njaa wa kisiasa mtu akileta mchezo unatandika shaba tu
Yuko wapi Sasa huyo JPM? Ukijifanya mbabe Kuna wababe zaidi Yako!! Ruto akijaribu kumtia shaba Odinga nakwambia vita itakua kubwa kuliko 2007 na nchi itagawanyika pasu kwa pasu.

Kule siasa za ukabila sio kama huku, mfano Lissu alivopigwa risasi basi kule kenya Kanda ya kati yote JPM asingewahi kanyaga milele. Au ukimgusa Mbowe basi Kanda ya kaskazini inakua war zone!!

So huo upuuzi wa JPM inawezekana Tanzania tu ambao ni mang'ombe.
 
Dunia nzima mafuta yamepanda bei alafu ruto baada ya miezi 6 ashushe bei nchini Kenya.
Kama anajua Hilo mbona kapandisha bajeti ya magari kutoka TZS billion 16 Hadi TZS Billion 40?? Au kupanda bei anayeumia ni kwa maskini tu huku matumizi ya serikali yanazidi kupandishwa tu kwenye vitu vya anasa?
 
imkamate na kumfungulia mashtaka.
Sio rahisi kihivyo!! Ukimkamata uwe tayari kwa machafuko kuanzia Mombasa mpaka Busia au Taita Taveta Hadi Homa Bay kitu ambacho Ruto hawezi himili.

Odinga ni WA kuitwa mezani tu otherwise siku sio nyingi mtaanza sikia Al Shabaab wanavamia airports na viwanja vya Mpira.
 
Wakenya hua ni wajinga sana sana
Hapana sidhani kama ni wajinga mkuu, ndo matokeo ya uhuru uliopitiliza. Hakuna nchi iliyowahi kuendelea kwa kuendekeza hili neno ‘demokrasia’ kila mtu ataamka asubuhi anataka lake ndo lisikilizwe, ilishindikana wanaandamana.

Uhuru uwe na kiasi
 
Kipindi mukiendelea kuchangia mambo ya Kenya, nawakumbusha wanasimba kumpigia kura chama kama mchezaji bora wa wiki.
 
Mambo ya Kenya waachieni wakenya. Tushughulike na Tanzania yetu kwanza.
Kuna la kujifunza ndo maana tunaongea. Ndo tunapoelekea. Tanzania na sisi tuna kiongozi kama odinga. Anaeamini yeye ndo anapendwa na nchi nzima. Sijui nani huwa anawadanganya.

Kuna watu wakiachwa wafanye wanayoyataka taifa litachafuka
 
Ninyi ndo mnafikiria kwa kutumia sijui nini akina Mandela wamekaa gerezani hakuna kimetokea ! Hakuna mtu mkubwa kuliko Taifa lolote,

Njia za kumuondoa ni nyingi tu si za kishamba za kupigana risasi nyingine ni Siri za kambi kinafanyikaga nini

Britanicca
we nae kichwa maji
 
Watu mnavyosema eti mkimdhibiti raila mtaitawanya kenya sijui wajaluo watabweka sasa aachwe ili aendelee kusumbua?. Kwani shida za mfumuko wa bei zipo kenya pekee? so mnabariki anavyoendelea kutesa vijana kuwaingiza mtaani?

Kuna watu wana uchu wa madaraka aisee huyo mzee si apumzike ye anaamini akiwa rais ataipeleka wapi kenya
 
We una umia nni na siasa zake
 
Ulichoandika ni pumba mbona ruto alikua anamtuhumu uhuru kwenye kupanda kwa bei na huku dunia nzima bei ya vitu ilikua imepanda
 
Kuna la kujifunza ndo maana tunaongea. Ndo tunapoelekea. Tanzania na sisi tuna kiongozi kama odinga. Anaeamini yeye ndo anapendwa na nchi nzima. Sijui nani huwa anawadanganya.

Kuna watu wakiachwa wafanye wanayoyataka taifa litachafuka
Huwez fananisha siasa za Tanzania na kenya ni mbingu na ardhi,
Tanzania kukiwa na mtaji wa wajinga kenya kuna werevu wengi
 
Back
Top Bottom