mwanamabadiliko
JF-Expert Member
- Oct 30, 2010
- 938
- 1,540
Ethiopia waligoma kuzuia safari China, Kuna cases 104 mwafrica 1 amekufa, Congo pia.
Marekani wameshazuia, sisi haya mambo ya urafiki tuacheni, naiomba serikali nipo chini ya miguu yake wazuie safari zote, huu ugonjwa Ni mbaya.
Corona ikija kutuua au kuua ndugu zetu CCM haitapona, nasema haitapona, chukueni hatua tuokoe kizazi chetu.
---

Kama mpaka muda huu napoandika mada hii,ndege kutoka mataifa kama China,Italy,Iran,Marekani na kwingineko ambako ugonjwa huu umesambaa bado zinaingia nchini,huu kwangu ni uzembe na ugonjwa huu ukiingia nchini, basi serikali ndio ya kulaumiwa.
Waziri wa Afya chukua hatua(toa ushauri ndege zisiingie kutoka mataifa hayo) na kama unakutana na vikwazo, ni bora ukajiuzulu vinginevyo tutakutaka uwajibike ugonjwa huu ukiingia nchini.
Hili pia linamuhusu waziri mwenye dhamana na maswala ya uchukuzi kwani liko chini yake.
Mkichukua hatua sasa na ugonjwa bado ukaingia,hatuwezi kuwalaumu ila si kwa kuacha hali hii ya kuruhusu mindege iingie alafu eti tunazuia mbio za mwenge.
Tuache kupambana na Coronavirus kwa style ya kupambana na Mbu wa Malaria ambapo tunaacha milango wazi alafu tunapambana na mbu hao kwenye vyumba vya kulala.