Njia pekee ya kuzuia CORONA Tanzania Ni kuzuia watu kuingia na kutoka nchini

Njia pekee ya kuzuia CORONA Tanzania Ni kuzuia watu kuingia na kutoka nchini

Ikitokea Basi Ccm watajitetea kwamba wao hawajaleta CORONA na hawatahangaika kutibu wagonjwa wa corona.
 
Joto linaathiri muda wa kuishi wa kirusi hichi kikiwa nje ya mwili wabinadamu lakini siyo kwa kiasi kikubwa sana. Kibaya zaidi mtu unaweza kuwa navyo lakini asionyeshe dalili na akavisambaza pia.

Kwa kifupi, nimeelewa kuna aina mbili ya hivi virusi. Aina ya kwanza ikikupata unapata dalili za mafua na homa, koo kuuma lakini ukatibu kama mafua mengine ukapona. Aina ya pili ndio mbaya sana ambayo ina develop pneumonia, mapafu yanajaa maji inabidi mtu awekewe vifaa vya kupumua na kutoa maji mpaka apone. Hivyo vifaa mara nyingi vinapatikana hopitali kubwa, hasa vyumba vya ICU. Tanzania tunavyo vya kutosha kuhudumia mlipuko ukitokea?

Maji masafi na sabuni ndio wawe rafiki zetu wa kudumu kwa sasa.

Laiti serikali ingehakikisha stendi zote za vyombo vya usafiri, malango ya kuingilia sokoni, maeneo ya mikusanyiko yote, nk. kuwe na maji na sabuni. Watu walazimishwe kunawa mikono kabla ya kuingia na baada ya kutoka kwenye maeneo haya na vyombo vyote vya usafiri.

Kuna uzi humu unatoa updates za Virusi na maambukizi ya Corona au COVID-19:
Fahamu kinachojiri kuhusiana na kirusi cha Corona (Coronavirus)
Ha mkuu hilo angalizo lako gumu sana. Kari

Nadhani hiyo namba 2 ndio inawaliza wazungu. Ila Mungu apishe mbali tutaanza kuogopana.
 
Jamani unaambiwa wanakuja huku kutibiwa kule wagonjwa wengi wanashindwa kupata huduma wanakufa
 
Kwa upande wangu naona hii ndo njia pekee inayoweza kuiepusha Tanzania dhidi ya ungonjwa hatari wa Korona.

Lakini Kama tunaendelea kujidanganya kwamba Serikali imejipanga sijui kuwafanyanyia vipimo wageni wanaoingia kutoka mataifa mbalimbali yakiwemo Yale ambayo yameathirika Sana kwa ugonjwa huu Kama vile China, Basi tunapotoka na Ni suala la muda tu Corona itatua nchini.

Pale Serikali itakaposhituka na kuanza kuzuia wageni kuingia na watu kutoka itakuwa tayari imechelewa.

Kama Serikali ina Nia thabiti ya kuzuia ugonjwa wa Corona Basi huu ndo ulikuwa muda mwafaka kwani wote tunafahamu kuwa Tanzania Hakuna Corona hivyo ili Corona iingie Tanzania Basi italetwa kutoka mataifa mengine.

Angalia video hapa chini kufahamu Serikali wanavyojidanganya
 
Attachments

  • 88009172_2551659521604876_1019766857565285344_n.mp4
    1.6 MB
Bahati mbaya hata mada zinazohusu Corona na serikali, moderator wanazihamishia Jukwaa tofauti
 
Kama mpaka muda huu napoandika mada hii,ndege kutoka mataifa kama China,Italy,Iran,Marekani na kwingineko ambako ugonjwa huu umesambaa bado zinaingia nchini,huu kwangu ni uzembe na ugonjwa huu ukiingia nchini, basi serikali ndio ya kulaumiwa.

Waziri wa Afya chukua hatua(toa ushauri ndege zisiingie kutoka mataifa hayo) na kama unakutana na vikwazo, ni bora ukajiuzulu vinginevyo tutakutaka uwajibike ugonjwa huu ukiingia nchini.

Hili pia linamuhusu waziri mwenye dhamana na maswala ya uchukuzi kwani liko chini yake.

Mkichukua hatua sasa na ugonjwa bado ukaingia,hatuwezi kuwalaumu ila si kwa kuacha hali hii ya kuruhusu mindege iingie alafu eti tunazuia mbio za mwenge.

Tuache kupambana na Coronavirus kwa style ya kupambana na Mbu wa Malaria ambapo tunaacha milango wazi alafu tunapambana na mbu hao kwenye vyumba vya kulala.
 
Back
Top Bottom