Njia rahisi ya kufikia Sudan Kusini ni ipi?

Njia rahisi ya kufikia Sudan Kusini ni ipi?

Ningependa baada ya janga hili la Korona nizamie zangu Sudan Kusini
Nafikaje huko?
Usalama ukoje?
Uimara wa sarafu yao ukoje?
Fursa za biashara zipoje?
Natanguliza shukranii
Pitia Uganda kunaendeka kwa bus
Usalama bado haujatengemaa
Fursa zipo za kutosha tatizo rushwa iko juu
Kuna ubaguzi wa makabila

Jr[emoji769]
 
Nenda Sudan kaskazini iliyokuwa ikiongozwa na Omar al-Bashir hasa jimbo la Darfur kama unaujuzi kidogo wa Veta fursa nje nje!
 
Okay...unatoka tz unaenda kampala...pale utapata mabasi mengi tu yanayoenda juba..
Usalama upo around juba...na maisha kule ni mapambano hasa itakubidi uwe aggresive kidogo....
Utakuta beautiful black ladies wanaojua kupenda...ukitaka experience kaishi adjumann kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwanza pole maana nimeona wengi wamekupa matango pori, sudan kusini hususani juba mji mkuu maisha ya kawaida sn na biashara zao wengi wanakuja kuhemea kampala, ukifika kampala wasudan ni wengi mnoooooo, usalama upo wa kutosha tu cha msingi usipeleke ujuaji sn wa kibongo kwenye nchi za watu kuhusu pesa jamaa wanatumia dola sn so pesa yao ipo juu sana, biashara za kufanya sudan kama utakua na msingi basi ni vyakula na vyombo vya ndani ni dili sn mkuu . wish you all the best

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiende kichwakichwa kule, anzia Uganda kwanza upate uzoefu..Fursa zipo ila itategemea na wewe mwenyewe usugu wako, Vijana wengi sana Kenya na Uganda wametajirika kwa dili za Magendo..

Narudia tena usiende kichwa kichwa, tafutia uzoefu ukiwa Uganda nenda kiani kachungulie uusome mchezo..
 
Back
Top Bottom