uko sawa kabisa wako magaidi wa kisiasa mfano aliyekuwa anaitwa Carlos the Jackal.Bahati mbaya sana nchi za magharibi ugaidi unaunasibisha na uislam.Nchi hata ya Marekani au Wingereza na wengine wanafanya ugaidi.Nitoe mfano CIA wanapofanikisha mipango ya raisi wa nchi flani auwawe au apinduliwe ule ni ugaidi.
Patrice Lumumba alivyouwawa kwa ushirikiano wa CIA na Ubelgiji ule ni ugaidi.
Marekani ni moja ya nchi yenye madhambi makubwa mno duniani lakini inapenda kulazimisha nchi zingine kukubali sheria ya Ugaidi.
Najisikia fahari sana kwa mara ya kwanza kupata comment kwa mtu mmoja almaarufu sana anaitwa FaizaFoxy.
Mti mzuri ndio unapigwa mawe ndio umaarufu wake uko hapo
Ahsante sana.
Labda niongezee tu kuna mahali nimesoma sasa hivi kuwa kifo cha Samora Machel Africa Kusini Makaburu walihusika na CIA ya Marekani.Ndege yake ilivyoanguka polisi wa Makaburi walikuja masaa kadhaa baadae sana ila kilochowaleta ni kuangalia je Samora amekufa au laa.Baada ya hapo walichukua nyaraka zake zote alizokuwa nazo kutoka kwenye mkutano Zambia.
Je hatuwezi sema Marekani ni magaidi?