Njia ya Kibiti kwenda kwenye laana ya Cabo Delgado

Njia ya Kibiti kwenda kwenye laana ya Cabo Delgado

Vita kuu ya kuuchafua Uislamu duniani ni DISINFORMATION.

Mwandishi wa makala hii analipa huu upupu alioumwaga. Hajaanza leo. Na analipwa na watendaji wa wasio waaminifu, wavuta bangi.

Ndio maana nimeuuliza mwanzoni tu.

Huu ujumbe wa makala unaolenga kuufungamanisha uislam na ugaidi.

Je, HIVI MAGAIDI WENYEWE NDIO WANAOJIFUNGAMANISHA NA UISLAM au WAANDISHI NDIO WANAOFUNGAMANISHA UGAIDI NA UISLAM?

Tuseme nchi hii kuna ugaidi wa kutengenezwa. False Flag Terror.

Tatizo la nchi la nchi yetu ni ubaguzi wa kidini tu hakuna cha ugaidi wa Waislam na Uislam.

......ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya.


Nitaweka threat inayojitegemea waraka wa waislam kwa serikali ukiitahadharisha serikali iache kuwalea waandishi wote wa kikundi hichi kinachofadhiliwa kuuchafua uislam.

Kama serikali haina mkono wake tunahitaji wamtafute azori ili atueleze ukweli wa mambo
Hupaswi kuwa chukia watu kwa kukuita mwizi Kama kweli wewe ni mwizi

Unacho takiwa ni kuacha uizi nakubadilika kabisa ili usiitwe mwizi

Tabia ni jina la kuzaliwa nalo na huwezi kuwa zuia watu wasi kuite jina lako

Uislamu utabaki uislamu tu kama utakuwa ukiji husisha na uislamu tu

Lakini utaitwa uislamu ugaidi Kama utajihusisha na ugaidi

Ushauri wangu kwa ndugu zangu waislamu

Nikwamba Kama waislamu hatuvutiwi na maneno machafu juu ya dini yetu kujihusisha na ugaidi

basi tuna paswa kuwa mstali wa mbele kwa kuwa tafuta na kuwa vumbua

na hata kuwa kabidhi magaidi mikononi mwa tawala au mamlaka ambazo tuna fanyia huduma zetu za kiroho baasi

Kwani hakuna ibaada pasipo amani

Hakuna uchumi pasipo amani


Hakuna maisha wala njia ya pepo.pasipo.amani

Tubadilike ndugu zangu hili Lina tuhusu na halikwepeki
 
Hupaswi kuwa chukia watu kwa kukuita mwizi Kama kweli wewe ni mwizi

Unacho takiwa ni kuacha uizi nakubadilika kabisa ili usiitwe mwizi

Tabia ni jina la kuzaliwa nalo na huwezi kuwa zuia watu wasikuiye jina lako
What if mwizi ni huyo anaekuita wewe mwizi lkn unapokwenda kuiba anadondosha kwa makusudi kitambulisho bandia Chenye jina na picha yangu.

Nani anastahili kukemewa na asipoacha kuchukiwa.
 
Na wanaamini katika JIHAD
Waislamu wengi ni wavivu hawataki kufanya kazi Wana penda easy money angalia hata mikoa ambayo dini hii Ina tawala

Maisha magumu, jitu Zima linaishi kwa baba na mama,mitoto ya kiume inaolewa

huko ndiko kunako ongoza kwa ushoga na ufuska

Yote ni kwasababu ya uvivu kukaa vibarazani badara ya kufanya kazi una kutas Toto la kiume Lina mwita mwana ume mwenzie shosti"

Huko ndiko uliko zaliwa uchawa

leo baba levo eti ni mtoto wa diamond inaingia hakilini kweli?

Sasa mtu Kama mwijaku/baba levo akipewa mil.40 aingize bom kalia Koo ana shindwaje?

Waislamu niwa vivu
Nenda tanga, Zanzibar,pwani na morogoro,ujionee ugumu wa maisha wanao upitia na uvivu jinsi ulivyo watawala

Kisha jiulize gaidi likitangaza dau tupo salama kweli?

mwislamu nirahisi kushawishika kuwa gaidi la kuaminika kupitia uvivu wake na misingi ya dini yake kuhusu maisha ya kesho/maisha baada ya kifo
 
What if mwizi ni huyo anaekuita wewe mwizi lkn unapokwenda kuiba anadondosha kwa makusudi kitambulisho bandia Chenye jina na picha yangu.

Nani anastahili kukemewa na asipoacha kuchukiwa.
Ina tegemeana ulisha wai kulipoti kwa Nani kupoteza kitambulisho chako?.

na baadae uka lipoti kukipata kupitia Nani au njia gani?

hapo ndipo tuta kapo anzia kwenye kujilidhisha kuhusu wewe juu ya kitambulisho chako na picha yako kupatikana eneo la tukio

Kisha tutajua ume bambi kiwa au need wewe mwenyewe
 
Oyaaa sio kila comment u reply kaza mtoto wa kiume.
Mie nimeishi huko na ndugu yangu alishavamiwa wenzie wakauliwa ila yeye walimsamehe walipomuona ana msahafu ila mateso walimpa kama kumpiga bapa za panga kumvua nguo kumgaragaza chini wenzie walichinjwa na rafiki mzungu kaacha mashamba yake Montepues sababu ya hao na marafiki wa Mozambican wanalalamika hawana raha nikasoma Uzi kujua chanzo haswa mpaka kufikia hapo aliposema ana muondelezo ndipo nikamwambia natamani ingekuwa movie ni download nisi subiri muendelezo mpaka mwisho.
sasa hayo maelezo ya ndugu yako yanahusiana nini na swali
 
𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 𝐧𝐚 𝐦𝐚𝐠𝐚𝐢𝐝𝐢 𝐲𝐚 𝐀𝐧𝐬𝐚𝐫 𝐚𝐥-𝐬𝐮𝐧𝐧𝐚.

- 𝐍𝐣𝐢𝐚 𝐲𝐚 𝐊𝐢𝐛𝐢𝐭𝐢 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐝𝐚 𝐤𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞 𝐥𝐚𝐚𝐧𝐚 𝐲𝐚 𝐂𝐚𝐛𝐨 𝐃𝐞𝐥𝐠𝐚𝐝𝐨.

- 𝐖𝐚𝐭𝐮 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐨𝐤𝐨𝐭𝐚 𝐦𝐢𝐢𝐥𝐢 𝐧𝐚 𝐯𝐢𝐜𝐡𝐰𝐚 𝐯𝐲𝐚𝐤𝐞 𝐩𝐞𝐦𝐛𝐞𝐧𝐢.

𝐒𝐄𝐇𝐄𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝟬𝟭:

Tarehe 20 mwezi huu wa tano, waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga taifa, Dkt. Stergomena Tax analiambia bunge kuwa hali ya usalama katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji bado haitabiriki.

View attachment 3003798

Kwa maneno machache bado hali si shwari na sababu ni uwepo wa kikundi cha kigaidi cha Ansar Al-Sunna ambacho kinafanya mashambulizi huko nchini Msumbiji, jimbo la Cabo Delgado linalopakana na mipaka ya kusini mwa Tanzania.

Hivyo ni bayana, kama kikundi hiki bado kinahema, basi hatuna uhakika wa usalama wetu huko mpakani. Waulize wakazi wa vijiji vya mpakani, Kitaya na Michenjele, huko halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara juu ya USIKU ule.

Usiku huo wa tarehe 14/10/2020, giza halikuja mpweke kwenye ardhi yao bali liliambatana na wageni wasiowatarajia.

Ikiwa ni majira ya saa moja, wanatahamaki wamo katikati ya mashambulizi ya kundi kubwa la watu wenye silaha za moto.

View attachment 3003799

Watu wanakimbia huku na kule wakipiga mayowe ya hofu. Wavamizi wanachoma nyumba, magari, zahanati na pia ofisi ya kata.

Sekeseke la zaidi ya nusu saa. Kifo ama uhai.

Hali kuja kutulia, watu wanatoka walikojificha na walikokimbilia, wanakuja kuokota miili ya wenzao waliopigwa risasi na wengine waliochinjwa kama kuku.

Lakini mbaya, wanabaini wapendwa wengine hawapo. Wamebebwa wakaongozana na 'mabwana' wale kurudi huko walikotokea. Wengi wao wakiwa mabinti wa makadirio ya miaka 14 mpaka 20.

(pichani ni mwanaume aliyepoteza mke na mtoto wake wa kwanza)

View attachment 3003801


Baada ya wiki moja kupita, siku ya Alhamis tarehe 22 Oktoba, ndo' aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi (IGP) Simon Nyakoro Sirro anasimama mbele ya vyombo vya habari na kusema tukio lile lilifanywa na magaidi waliovuka mpaka kutoka nchini Msumbiji.

View attachment 3003822

Magaidi hao walikuwa 300 kwa idadi na wamefanya uhalifu ikiwemo mauaji. Baadhi wakakimbia na wengine wakakamatwa wanaendelea na mahojiano. Anasema lengo ni kupata mtandao wote wa magaidi.

Mtandao ulioanzia kule MKIRU (Mkuranga, Kibiti & Rufiji).

Kwa mujibu wa kamanda Sirro, wale Ansar al-sunna waliopo Msumbiji leo hii jimbo la Cabo Delgado, ambao ndo' wanamfanya waziri Stergomena Tax kusema kuwa usalama hautabiriki mpakani mwetu na Msumbiji, mtandao wao ulianzia hapa nchini mkoa wa Pwani.

Ila ni kweli Pwani tu? Kuna mahusiano gani na kwanini tena jimbo la Cabo Delgado mpaka leo hii? Mbinu za hawa magaidi ni zipi? Jeshi la SADC na Rwanda wamefikia wapi? Hali ya sasa ipoje na Rwanda ananufaikaje na mgogoro huu?

Ikumbukwe ripoti ya hivi karibuni, tarehe 17 Aprili 2024, kutoka gazeti la serikali ya Msumbiji, 'Boletim da Republica' imetolewa orodha ya watu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kushirikiana na kikundi hiki cha ugaidi, miongoni mwao wametajwa watanzania wawili; bwana Ally Yusuf Liwangwa (47) kutoka Dar es Salaam na bi. Safina Maulana (36) kutoka Mtwara.

View attachment 3003806

Sasa turudi kwenye siku ile ya tarehe 5, Oktoba 2017. Siku ya kwanza kabisa risasi kurushwa hewani kwa jina la Ansar al-sunna.

Siku hiyo katika mji wa pwani - Mocimboa de Praia - jimbo la Cabo Delgado, mambo yanabadilika ghafla katikati ya usiku na alfajiri.

View attachment 3003807

Kuanzia saa saba ya usiku, kundi la watu wanaokadiriwa thelathini kwa idadi wakiwa na silaha za moto na baridi, wanavamia mji huu wakilenga vituo vya wanausalama.

Mpaka kufikia saa kumi alfajiri, vituo vitatu ambavyo ni Mocimboa district police, kituo kidogo eneo la Awasse na kituo cha polisi cha maliasili na mazingira vinaripoti kushambuliwa na kutokea majibizano ya risasi.

View attachment 3003808
View attachment 3003814

Msemaji wa jeshi la Polisi, kamanda Inacio Dina (pichani), anawaambia waandishi wa habari mashambulizi hayo yamepelekea vifo vya maafisa polisi wawili na wavamizi watatu lakini ripoti zinasema watu 14 walifariki na pia vituo viliripoti kupotelewa na silaha.

View attachment 3003811

Wavamizi hao walikuwa wanazungumza lugha ya Kireno, Kiswahili na Kimwani. Hiki Kimwani ni lugha ya watu wa pwani ya eneo hili.

Kamanda anasema pia wamefanikiwa kuwakamata wavamizi kadhaa na hao watasaidia kupata taarifa zaidi ya wavamizi wenzao.

Kamanda anapoulizwa kuhusu mafungamano ya wavamizi hao na waislamu wenye itikadi kali mathalani Al-shabab wa kule Somalia, anasema ni mapema sana kusema hivyo. Watu hao kutumia 'local languages' za hapa Msumbiji kunamaanisha ni watu waliokulia hapahapa.

View attachment 3003815

Na hili linatukumbusha miezi sita nyuma ambapo redio ya taifa, Radio Mozambique, iliripoti kukamatwa kwa wanaume watatu wanotuhumiwa kuwa na 'connection' na Al-shabab.

Wanaume hao walikuwa wanawakataza watu kwenda vituo vya afya vya serikali na pia kuwapeleka watoto wao shule.

View attachment 3003816

Lakini baadae walikuja kuthibitika hawana mahusiano yoyote na Al-shabab ya Somalia japo wakaazi walikuwa wanawaita jina hilo, hivyo wakaishia kushikiliwa kwasababu ya kusababisha mashaka ya usalama.

Kamanda Inacio anawaondoa hofu wananchi akisema kikosi maalum cha kupambana na ugaidi kipo kazini na hivyo hali ya usalama itakomaa hivi punde.

Lakini tofauti kabisa na anachosema, huu ndo' unakuwa mwanzo rasmi wa mfululizo wa mashambulizi na mauaji katika jimbo la Cabo Delgado mpaka kuja kuvuka mpaka wa Tanzania.

View attachment 3003818

Kabla ya mwezi Oktoba kuisha, 'mabwana' wanamjibu kamanda kwa mashambulizi mawili katika kijiji cha Maluku na karibu na kijiji cha Columbe.

Mwezi unaofuata (Novemba) tarehe 29 wanavamia vijiji vya Mitumbate na Maculo. Wanaharibu kanisa na pia wanachinja watu wawili.

View attachment 3003819

Tarehe 13 January 2018 wanaingia mji wa Palma na kumwaga risasi sokoni na kwenye ofisi ya serikali. Watu watano wanakufa.

Tarehe 12 March, wanavamia kijiji cha Chitolo na kuchoma nyumba hamsini pia wanaua wakazi. Na kwa siku tatu mfululizo 20, 21 na 22 mwezi Aprili wanavamia vijiji kadha wa kadha wakiua na kuteka watu.

View attachment 3003823

Ni mwezi unaofuata, Umoja wa Afrika (AU) unathibitisha ripoti ya gazeti la Afrika Kusini iliyosema kuna wapambanaji wa Islamic State wamekwishaingia ndani ya Msumbiji, ripoti ambayo serikali ya Msumbiji ilikuwa inapingana nayo hapo awali.
View attachment 3003826
Na kilichofuatia baada ya hapo, ndo' hali ikawa mbaya zaidi. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huo 2019, watu zaidi ya arobaini na sita wakaripotiwa kuuawa kwa risasi na kuchinjwa kama kuku ikiwemo watoto wadogo.

View attachment 3003824

Achilia mbali nyumba lukuki ziliishia kuchomwa moto, watu kujeruhiwa na wengine kutekwa.

Si polisi, si jeshi la Msumbiji (FDS) wote wako hoi.

Mabwana hawa waliwavua nguo, kila mtu akaona uchi wao. Namna walivyo duni kwenye vifaa na mafunzo, na namna walivyo 'corrupt'.

View attachment 3003828

Wananchi wanasema mara kadhaa wameshuhudia wanajeshi wakikimbia eneo lao la ulinzi muda mfupi kabla ya eneo hilo kushambuliwa na magaidi. Wengine wanaiba mitumbwi ya wananchi ili wakimbie kujinusuru.

Kwa kaliba hii, mashambulizi yanazidi kutiririka, magaidi wakiamua wachinje ama wakatekate kama kuni (dismembering).

Zoezi hilo linaenda mpaka mwishoni mwa mwaka 2019 ambako serikali ya Msumbiji inakiri kuhitaji msaada, wamezidiwa.

Kwa kupitia FDS wanawekeana mkataba na jeshi la mamluki (mercenary) Wagner Group la nchini Urusi, na kwa mara ya kwanza kabisa mapema ya mwezi Oktoba mwaka 2019, mashambulizi ya kwanza ya FDS wakishirikiana na Wagner Group yanashika hatamu na yanaleta mafanikio.

View attachment 3003830
Wanawakimbizia magaidi huko misituni na wanafanikiwa kukamata watu makumi kwa makumi walokuwa wanasafiri kutoka jimbo la Nampula kwenda kuongeza nguvu ya magaidi huko jimbo la Cabo Delgado.

Lakini nguvu hii ya soda haikuchukua hata mwezi. Magaidi wanajibu kwa mtindo wa mashambulizi ya kushtukiza (ambushing) na FDS wanapoteza wanajeshi ishirini huku Wagner wakipoteza wanajeshi saba.

Mwezi wa kumi na moja, FDS wanapoteza tena wanajeshi kadhaa huku Wagner wakipoteza wanajeshi watano.

View attachment 3003832

Kipigo hiki kinapelekea pande hizi mbili, FDS na Wagner Group, kuingia kwenye mgogoro. FDS wanailaumu Wagner kutokuwaheshimu maafisa wao na huku Wagner wanalaumu jeshi la FDS pamoja na raia kuwa 'undiscplined'.

Hivyo oparesheni inafeli.

Wagner wanaondoka zao na katika ombwe hili, mkuu wa jeshi la Polisi, kamanda Bernadino Rafael, anaona afanye jambo upesi ili kujiimarisha kiusalama.

Anawasiliana na bwana Lionel Dyck, mkurugenzi wa jeshi binafsi toka nchini Afrika Kusini, Dyck Advisory Group (DAG), ambayo inahusika na utoaji wa vifaa na wataalamu wa mapambano ya kivita.

View attachment 3003837

Wanaweka makubaliano ya kupatikana kwa helikopta sita za vita na pia msaada wa anga kuwakabili magaidi.

Kwa muda huo 2020, hapo Msumbiji kulikuwa na helikopta moja tu ya combat, Russian-built MI-8, tena waliyopewa kama msaada na Rais Putin mwaka 2017.

View attachment 3003840

DAG wanaanza oparesheni yao April, 2020, wakikatiza anga la Msumbiji kupambana pembeni ya wanausalama.

View attachment 3003855

Lakini misheni yao ikiwa imebakiwa na wiki mbili tu kumalizika, linatokea shambulizi la mji wa Palma.

Shambulizi kubwa la kigaidi kupata kutokea katika ukanda huu wa kusini mwa Afrika.

Watu takribani 1,200 - 1,400 wanauawa ndani ya siku moja. Maiti zinazagaa barabarani. Mamia ya watu, ikiwemo watoto, wanaokotwa wakiwa hawana vichwa.

View attachment 3003862

Shambulizi hizi linashtua jumuiya mataifa ya kusini mwa Afrika (SADC), na sasa linaazimia kufanya kitu upesi kabla hatujaipoteza nchi ya Msumbiji mazima.

View attachment 3003933

Na Rwanda naye habaki nyuma. Anaingiza miguu yake eneo hili akidai kuisaidia Msumbiji kupambana na ugaidi ni njia mojawapo ya kujihakikishia usalama wake kama nchi.

View attachment 3003866

Lakini hana interests zingine hapa?

Kama hapana, je vile vikao vyake na raisi wa Msumbiji, Felipe Nyusi, pembeni ya mkurugenzi wa TotalEnergies, bwana Patrick Pouyanné, vinatoa ujumbe gani?


Ikumbukwe shambulizi hili la mji Palma lilitokea karibu na mradi mkubwa wa dola 'mabilioni' ulio chini ya kampuni ya kifaransa ya TotalEnergies na kupelekea kampuni hiyo kufunga shughuli zake kwa muda usiojulikana.

View attachment 3003938

Lakini yote kwa yote, Msumbiji imefikaje hapa? Intelijensia yake ililala wapi? Hawa magaidi ni kina nani na wanataka nini hapa Cabo Delgado?

Kuna mahusiano gani na mambo ya MKIRU (Mkuranga, Kibiti na Rufiji)?

Habari inaanzia kule Mombasa, Kenya, miaka 12 ilopita...

𝐓𝐔𝐍𝐆𝐎𝐉𝐄 𝐒𝐄𝐇𝐄𝐌𝐔 𝐘𝐀 𝟬𝟮:
Uchambuzi uliotukuka.
 
Hakuna cha ugaidi wala nini nchi hii sema alikuwa na chuki tu kama makafiri wengine wote dhidi ya Waislamu na ndiyo walioenda kuuliwa na wale wengine wachache waliohoji juu ya mauaji hao wakapotezwa.
Tatizo la nchi la nchi yetu ni ubaguzi wa kidini tu hakuna cha ugaidi wala nini,kuna msemo unasema ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya.
Gaidi katika 1 na 2. Hamna nafasi ndani ya nchi hii, kafanyieni upuuzi wenu Msumbiji na Somalia
 
Hao DAG wa south Africa na wao ni Private Military Company (PMC).
Mwaka 2020 June 27 hadi 29 yalitokea mapigano makali kati ya Jeshi la Msumbiji wakisaidiwa na hao DAG, magaidi waliteka na kuua katika mji wa Mocimboa da Praia uliopo jimbo la Cabo Delgado.

Wagner walipokuja na kusema jeshi la Msumbiji nidhamu hakuna na hawajajipanga walikuwa hawajakosea.

Magaidi waliwazidi nguvu Jeshi la Msumbiji, June 27 magaidi walitembeza kichapo heavy ambapo askari wa Msumbiji walianza kutoroka wengine wakijichanganya na raia, hali imekuwa ngumu ilifikia kipindi askari jeshi wanavua gwanda na kujichanganya na raia, Magaidi walikosa upinzani.
Baadhi ya askari walikimbilia majengo ya bank lakini walimalizwa na kundi hilo.

Ndipo hao DAG wakaingia mzigoni wakiwa na helicopters 3 angani na kuanza msako, mashambulizi yalikuwa yanatokea angani, kazi ilikuwa ni kutofautisha raia na magaidi.

Kuna kipindi magaidi walijichanganya na raia kitu kilichopelelea helicopters za DAG kushambulia kundi na kupelekea wananchi wengi kufa.

Baada ya moto kuwa mkali ilibidi hao jihadists wakimbilie hospital kudhani moto kutoka angani ungewaacha, lakini DAG walipeleka moto huko huko hospital kupelekea wagonjwa na wananchi kufariki, helicopter 3 zinazunguka mji, jamaa walimwaga moto mwingi sana huku jeshi Msumbiji wakifanya operation ndogo ardhini.

Inasemekana DAG walipeleka moto hadi Al Shabaab kwa jina lingine wanojulikana wakaamua muingia maporini , lakini moto huakuwaacha nyuma wakafuatwa huko jamaa wakapeleka moto, huko msituni kulikuwa na raia wamekimbia na Al Shabaab wapo humo na mateka, kuna imaam mmoja aliyekuwa mateka chini ya Al Shabaab alifariki msituni.

Mji ulikuwa hautamaniki ni kama Gaza, baadhi ya wakazi walikimbia kuelekea visiwa vya karibu kwa kutumia boat huku wengine wakikimbilia vijiji vya karibu kuponya uhai.

Wanakijiji walipokuja kurudi Macimboa ilikuwa ni maiti zimetapakaa mji mzima.

Kwa moto DAG waliupeleka, ilipelekea Amnesty International kuingilia kati kwamba DAG wamefanya uhalifu wa kivita kwa kuua raia wasiokuwa na hatia huku DAG wakisema si si kweli wao walikuwa wakilenga magaidi walipo.

Jeshi la serikali ya Msumbiji pia ilisemekana kufanya uhalifu kabla ya Al Shabaab hao kufika kwenye huo mji wa Mocimboa, ilisemekana walitesa wananchi, kuua na ubakaji kitu kilichopelelea baadhi ya wananchi kujiunga na Al Shabaab hao hivyo kupelekea kuwazidi nguvu Jeshi la Msumbiji kwenye hio battle ya June 27.

Baadae Jihadists hao walikuja tena kuuchukua huo mji wa Mocimboa da Praia mwezi august mwaka huo huo wakikizidi jeshi la Msumbiji nguvu.

Hapa DAG hawakuingilia kati kutokana na kile kilichokua ni mashtaka kutoka Amnesty International.

Sasa hapo ndipo unielezee hao DAG ambao ni moja ya PMCs walienda kufanya nini..
Pale wanaenda kupambana na kutoa mafunzo. usifikiri wanakwenda kutoa mafunzo pekee.

Nikitafalari haya mashirika kama Amnesty yapo kutimiza maslahi ya wakubwa. Hio kazi wangeachiwa DAG kwa huo moto wao, Hao w@$3ng3 wangeshasambaa.
Mpaka hapo napata picha hayo magaidi ya Msumbiji ni project ya Europeans/USA
 
msumbiji ni nchi basi. ni kikundi cha wahuni na watunga shanga. hamna nchi pale ni takataka jeshi lao kama la wakata viuno drc
Mkuu nakubaliana na wewe nimesafiri mara kadhaa kwenda Msumbiji kwanza Serikali ipo Maputo tu huko kwenye majimbo hakuna kitu hali ni duni sana. Wanajeshi wao ni waoga kupita maelezo tuliwafundisha mbinu za medani za kutosha ila kwenye uwanja wa vita wanakimbia au kuuza ramani kwa waasi. Wanajeshi wa nchi nyengine hawataki kushirikana nao kwa sababu wanauza sana kambi. Nakubaliana na wewe Msumbiji sio nchi ni genge lililoachwa na Wareno ili kuzua taharuki.
 
Oyaaa sio kila comment u reply kaza mtoto wa kiume.
Mie nimeishi huko na ndugu yangu alishavamiwa wenzie wakauliwa ila yeye walimsamehe walipomuona ana msahafu ila mateso walimpa kama kumpiga bapa za panga kumvua nguo kumgaragaza chini wenzie walichinjwa na rafiki mzungu kaacha mashamba yake Montepues sababu ya hao na marafiki wa Mozambican wanalalamika hawana raha nikasoma Uzi kujua chanzo haswa mpaka kufikia hapo aliposema ana muondelezo ndipo nikamwambia natamani ingekuwa movie ni download nisi subiri muendelezo mpaka mwisho.
Ningereply kila comment ina maana nusu ya posts kwenye huu uzi zingekua zangu.

Anyway Sorry for your loss mtoto wa kiume.
 
Je, HIVI MAGAIDI NDIO WANAOJIFUNGAMANISHA NA UISLAM au WAANDISHI NDIO WANAOFUNGAMANISHA UGAIDI NA UISLAM?


Tuweke ushahidi ktk kulijadili hii conspiracy.

Kwani aina hii ya uandishi kama kwamba mwandishi alikuwepo wakati maturiko yakitokea yananipa mashaka kuwa hii ni script kama script nyingine za Hollywood za kuupata matope Uislam.

Tujiulize kwanini mwandishi mmoja (nzori kama sijakosea) aliyetaka kutuletea ukweli wa ugaidi kwa kibiti alipotezwa akiwa ktk mikono ya watu salama.
Una
Inasemekana Azory alikamatwa na watu wasiojulikana.

Wasiojilikana kila mmoja wetu unafahamu ni kina nani.

Akapotezwa sasa wanakuja waandishi na kuhadithia habari za mkwiru kana kwamba wamezifanyia uchunguzi ambazo azory hakipata fursa hiyo na kupotezwa.

Ndio maana nimeulizea mada hii yenye lengo la kuunasibisha uislam na ugaidi.

Je, HIVI MAGAIDI WENYEWE NDIO WANAOJIFUNGAMANISHA NA UISLAM au WAANDISHI NDIO WANAOFUNGAMANISHA UGAIDI NA UISLAM?
Unamjua mwandishi?
 
Ina tegemeana ulisha wai kulipoti kwa Nani kupoteza kitambulisho chako?.

na baadae uka lipoti kukipata kupitia Nani au njia gani?

hapo ndipo tuta kapo anzia kwenye kujilidhisha kuhusu wewe juu ya kitambulisho chako na picha yako kupatikana eneo la tukio

Kisha tutajua ume bambi kiwa au need wewe mwenyewe
Fikiria tukio la kigaidi la hili karibuni. Kijana kakamakwa na watu waliojitambulisha usalama. Wakamchukua hadi kituo maarufu cha polisi oystebay na kumpeleka eneo la gereji. Wakamtesa. Wakasafiri nae hadi arusha, wakaenda kumputa porini katavi. Wasamaria wema wakamwona na kutoa msaada. Manusura akahadithia yote. Baada ya kuhadithia asubuhi wanajitokeza jeshi la polisi na kusema wanawatafuta waliomteka mtuhumiwa. Hadi leo hawajamuona.

Ndio maana tunauliza what if mwizi ni yule ataewarangazia umma x ni mwizi.

In my opinion tz kama si duniani, hakuna ugaidi wa waislam bali ni False Flag.

Kupitia propaganda 85% ya watu huwa fool

But time will tell u can fool some people some time. But u can't fool all the people all the time.

My friend uko tayari contaminated na propadanda za wahuni waliojificha ndani ya taasisi za serikali
 
Fikiria tukio la kigaidi la hili karibuni. Kijana kakamakwa na watu waliojitambulisha usalama. Wakamchukua hadi kituo maarufu cha polisi oystebay na kumpeleka eneo la gereji. Wakamtesa. Wakasafiri nae hadi arusha, wakaenda kumputa porini katavi. Wasamaria wema wakamwona na kutoa msaada. Manusura akahadithia yote. Baada ya kuhadithia asubuhi wanajitokeza jeshi la polisi na kusema wanawatafuta waliomteka mtuhumiwa. Hadi leo hawajamuona.

Ndio maana tunauliza what if mwizi ni yule ataewarangazia umma x ni mwizi.

In my opinion tz kama si duniani, hakuna ugaidi wa waislam bali ni False Flag.

Kupitia propaganda 85% ya watu huwa fool

But time will tell u can fool some people some time. But u can't fool all the people all the time.

My friend uko tayari contaminated na propadanda za wahuni waliojificha ndani ya taasisi za serikali
Yule mtu aliji husisha nasiasa/Deep politics ways can isay

kitu ambacho ni hatali
wakati huo huo Hana Kinga

so Waka mkamata kisiasa wakamfanya walivyo jiskia na wakataka kumpoteza kisiasa

na Hata alipo bahatika kuwa hai baada ya kuya eleza aliyo yapitia nakuomba msaada

wameamua kumsaidia kisiasa

Na kuhusu wahuni iam not sure Kama wapo lakini Hata mhuni ukimuuliza kwanini Ana fanya uhuni

atakwambia sababu ambazo utazielewa

So siwa chukulii Kama niwahuni Ila naweza kuwaona Kama niwatu ambao walikuwa kazini na wanalipwa kwa kazi hiyo

Sasa unadhani Kuna kazi au malipo yasiyo na faida?

Ninacho zungumzia hapa nikwamba si geni hili la uislam kuhusishwa na ugaidi

Lakini je! waislamu wanafanya juhudi gani kuu tenganisha uislam na ugaidi?

Binafsi sioni juhudi hizo ziki fanyika na Hilo huenda tafsiri ake ikawa inatuhusu coz we don't care about

that's why nimezungumza hivyo no more

so sorry Kama nitakuwa nime eleweka vibaya mkuu
 
Yule mtu aliji husisha nasiasa/Deep politics ways can isay

kitu ambacho ni hatali
wakati huo huo Hana Kinga

so Waka mkamata kisiasa wakamfanya walivyo jiskia na wakataka kumpoteza kisiasa

na Hata alipo bahatika kuwa hai baada ya kuya eleza aliyo yapitia nakuomba msaada

wameamua kumsaidia kisiasa

Na kuhusu wahuni iam not sure Kama wapo lakini Hata mhuni ukimuuliza kwanini Ana fanya uhuni

atakwambia sababu ambazo utazielewa

So siwa chukulii Kama niwahuni Ila naweza kuwaona Kama niwatu ambao walikuwa kazini na wanalipwa kwa kazi hiyo

Sasa unadhani Kuna kazi au malipo yasiyo na faida?

Ninacho zungumzia hapa nikwamba si geni hili la uislam kuhusishwa na ugaidi

Lakini je! waislamu wanafanya juhudi gani kuu tenganisha uislam na ugaidi?

Binafsi sioni juhudi hizo ziki fanyika na Hilo huenda tafsiri ake ikawa inatuhusu coz we don't care about

that's why nimezungumza hivyo no more

so sorry Kama nitakuwa nime eleweka vibaya mkuu
Kwa hiyo katiba inaruhusu ukijiingaza ktk siasa za kukosoa serikali adhabu ni kuwawa na watu wasiojulikana.

Kitendo alichifanyiwa na wasiojilikana, lkn walipeleka katakana oystebay ni cha kigaidi.

Tujiulize, kwanini huyu muathirika hakuwataja mashekhe, jiulize pamoja na mashekhe kukaa muda mrefu gerezani mwisho wa siku serikali inawaachia huru kwa kusema hawaoni sababu ya kuendelea na kesi hiyo.

Haki ya kuwahusisha inatoka wapi. Kwann tuone kuna ulazima wa kufanya juhudi wakati kimsingi tz wenye uelewa wanaielewa kuwa maumivu wanayoyapitia waislam ni kwasababu wana maoni tofauti na watendaji wa serikali wenye uwezo mdogo wa kutafsiri mambo waliobahatika kuwa ndani ya serikali.

Na ni kawaida kuwa viongozi wenye uwezo mdogo wa kufikiri kutengeneza wafuasi wenye uwezo mdogo wa kufikiri.

But they can't fool smart tz christian neither us.
 
Hawa wanamgambo kwa tukio walilolifanya huko kitaya mkoani mtwara, ilikuwa ni kete ya kuwatafuta popote walipo duniani na kuwatokomeza

Ilikuwa ni dharu kubwa sana kwa nchi yetu. Jeshi lilfanya kazi yake, ila halikwenda zaidi. Ulikuwa muda wa kuwafuta kabisa duniai na kulipa jeshi heshima yake.
 
Back
Top Bottom