Njia ya kumuachisha mtoto kunyonya kidole

backtobasics

Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
26
Reaction score
40
Wana JF,

Ni njia gani isiyo na madhara ya kumfanya mtoto aache kunyonya vidole, ana miezi 7 sasa ila naona kwa kasi anayoenda nayo yaani hadi usingizini yeye yuko navyo tu...

Sitamani afike umri mpaka anaanza shule awe ananyonya na pia nasikia vinaharibu dental formula hivyo nawezaje kumsaidia?

===
Ufuatiliaji wa JamiiCheck

 
Mkuu achana nayo hiyo mdogo wangu ana miaka 30 kwa sasa na ana nyonya!

Nilikua kaacha siku moja nadhani ni pasaka hii tukalala kitanda kimoja kule kijijini kwa wazee nikasikia kama mtu anafyonza kitu kumuangalia ananyonya madole.

Nadhani hawaachi dogo karithi kwa babu mdogo upande wa baba na yeye hadi anakufa alikuwa akijisahau anatia dole mdomono dole lile hadi lilikuwa lishabadilika
 
duuuh😂😂 !!!hii hatari sasa huyu mtoto wa kiume si ni noma sana
 
Kama anatmebea unamvalisha kaptula bwanga kiunoni attention inahamia kuzuia kaptula isidondoke.
Tafuta mwenzake wa kucheza naye kukimbizanakimbizana kunafanya asaahau kunyonya kidole
 
Mwanaume unalala na dume lenzako kitanda kimoja? Maajabu
 
Hii ni janga mimi kuna mtoto wa mdogo wangu ana miaka sita ananyonya mno na ni kweli zinaharibu dental formula
 
Muache unampa mateso makubwa hivyo vitu ni automatically

Mtoto kunyonya kidole ni tabia ya kawaida ambayo mara nyingi huanza tangu akiwa tumboni au punde tu baada ya kuzaliwa. Hizi hapa ni sababu kuu zinazomfanya mtoto afanye hivyo:

Kujituliza na Kujifariji:
Hii ndiyo sababu kuu. Mtoto hutumia kidole kama njia ya kujipoza anapokuwa na wasiwasi, anapochoka, au anapotaka kulala. Kulingana na maelezo ya wataalamu katika Gazeti la Mwananchi, kunyonya kidole huwasaidia watoto kujisikia salama na wenye furaha.

Asili ya Kunyonya (Sucking Instinct): Watoto huzaliwa wakiwa na hamu ya asili ya kunyonya kwa ajili ya kupata chakula. Wakati mwingine, hata kama ameshiba, ile hamu ya kunyonya bado inakuwepo, hivyo hutumia kidole kuitosheleza.

Njaa:
Mara nyingine mtoto anaweza kuanza kunyonya kidole ikiwa hajapata maziwa ya kutosha au anahisi njaa na anasubiri kulishwa.

Kuondoa Upweke:
Mtoto anaweza kunyonya kidole anapojihisi mkiwa au mpweke kama njia ya kujiliwaza mwenyewe.

Kukua kwa Meno:
Wakati meno yanapoanza kuchomoza, fizi huwasha au kuuma, hivyo mtoto huweka kidole mdomoni ili kupunguza muwasho huo.Wataalamu wengi wanashauri usimlazimishe mtoto kuacha tabia hii akiwa na umri wa chini ya miaka 4, kwani watoto wengi huacha wenyewe kadiri wanavyokua na kuanza kupata njia nyingine za kujiliwaza.
 
Nimewahi kuona njia nyingi wanatumia wazazi na walezi.Kuna zingine sikuzipenda kama vile kupiga,kuwawekea pilipili na hata vitisho vingi.Jaribu kuwa unamvalisha gloves za nguo zisizoumiza ili akiweka kidole mdomoni kisishawishi kukinyonya.
 
Hili siyo tatizo. Ataacha mwenyewe hasa akianza shule. Usihangaike. Kna watu tuna watoto walinyonya vidole .... yaani kila mtoto wangu alinyonyalakini waliaacha wenyewe.
 
Endelea kusema ukatili mpaka mtoto awe na magego na meno yaliyoparanganyika.
Kumbuka kuwa meno ya utotoni hung'oka mtoto akifikia umri kati ya miaka 5-8. Hivyo hiyo dental formula itajipanga upya kama kawaida.
Mimi nilikuwa na tabia ya kutafuna peni wakati wa kujisomea hasa maswali magumu ya pure maths kipindi nabukua usiku wa manane. Lakini leo hii sifanyi hivyo.

Mtoto ataacha mwenyewe kadri umri unavyokuwa mkubwa.
 
Mwanaume unalala na dume lenzako kitanda kimoja? Maajabu
Asee wacha namimi nikushangae ...ebu nambie kosa la kulala na mwanaume mwenzio kitanda kimoja?

Ujue bro sio kila mtu ana element za ushoga kama wewe na jamii inayokuzunguka la wengine hatuko hivyo.

Ebu nambie tofauti na ushoga ulio kujaa kwenye ubongo wako Kuna tatizo Gani kulala na mdogo wako wa kiume kitanda kimoja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…