Njia ya kupunguza msongamano wa magari na watu katika Majiji - Tanzania

Njia ya kupunguza msongamano wa magari na watu katika Majiji - Tanzania

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,446
Reaction score
1,645
Habari Tanzania !

Leo njoo tuwake kwa maneno makali hapa tuwaweke watu kazi juu juu.

Njia za kupunguza na kuondoa msongamano wa watu na vyombo vya moto ni kama ifuatavyo;

1. Tuwekeze kwenye usafiri wa umma. Iwe kuna utaratibu kuwa njia zenye makazi ya watu yaani ile (Density Population ); usafiri hapo utumike wa umma pekee.

2. Tuweke Transport Card; hii haikwepeki hapa. Tuweke utaratibu mzuri wa nauli rafiki; pia mwananchi/ abiria aweze kuwa na Kadi ya Usafiri hii kwa safari zake za hapa na pale.

3. Tuunde Shirika la Usafiri wa Umma (Pawe na kampuni za Usafiri wa Umma zisizidi 3 mpaka 5 tu); zisajiriwe kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Tuachane na maupumbavu yaliyopo leo hii.

4. Serikali iruhusu mtu/ watu/ kampuni binafsi zijenge barabara na kuweka tozo ya huduma kwa muda fulani wa faida na rejesho kwa muwekezaji kulingana na makubaliano na Serikali. Haya makubaliano na mikataba ipitie Bungeni.

5. Gereji zote za vyombo vya moto zisajiriwe ziwe za kitaasisi na sio kama ilivyo kwa sasa. Tunatupunga msongamano na mlundikano wa hivyo vyombo vya usafiri.

6. Siasa isijifiche kwenye usafiri wa Umma.

Karibu.
 
solution inatengewa bajeti bilioni 100, jinsi zitavyotandikwa inabaki bilioni 10 tu 😂 halafu baada ya miaka mitano hivyo hivyo
 
solution inatengewa bajeti bilioni 100, jinsi zitavyotandikwa inabaki bilioni 10 tu 😂 halafu baada ya miaka mitano hivyo hivyo
Wanipe mimi hizo Bilioni; tuwape barabara mtelezo.
 
Hiyo mil napewa kabisa au nacheck kwanza barabara 🤭😁
 
Hata tujenge barabara zote ziwe lami kwa tabia zetu sisi na mifumo mibovu misongamano haitakwisha.
Wenzetu ni kuwa kwa mfano barabara zinatumiwa na vyombo vya moto ambavyo wenyewe wanalipia kodi. Hakuna mtembea kwa miguu,baiskeli au guta anaruhisiwa mpaka maeneo ya kuvukia tu. Siyo tu inapunguza foleni bali pia hakuna mtu au baskeli na gari vikakutana kuleta ajali.
 
Hata tujenge barabara zote ziwe lami kwa tabia zetu sisi na mifumo mibovu misongamano haitakwisha.
Wenzetu ni kuwa kwa mfano barabara zinatumiwa na vyombo vya moto ambavyo wenyewe wanalipia kodi. Hakuna mtembea kwa miguu,baiskeli au guta anaruhisiwa mpaka maeneo ya kuvukia tu. Siyo tu inapunguza foleni bali pia hakuna mtu au baskeli na gari vikakutana kuleta ajali.
Wazo ni nzuri sana. Kikubwa wazingatie ushauri.
 
PENDEKEZO LA KUPUNGUZA FOLENI: iwe kama ifuatavyo:
Turekebishe muda wa kuingia kazini(Kama vile tulivyorekebisha msongamano wa abiria wakati wa siku za sikukuu kwa kuruhusu magari kusafiri saa 24,yaani usiku na mchana).
i.kampuni zinazofanya usafi barabarani(wafanye kazi usiku)
ii.Matengenezo ya barabara(Kazi ifanyike usiku).
iii.Baa zifanye kazi hadi saa 8(Hatua hii itawatuliza wanywaji wasilete foleni,kwani muda wa baa utakuwa umesogezwa mbele , na itasaidia wenye kunywa wachangie mapato,watakao kuwa wazembe kwa ulevi wachukuliwe hatua kwani wengi wanasubiri ajira).
iV.Baadhi ya Taasisi muda wa kuingia kazini uwe ni saa 3 asubuhi.
V.Baadhi ya Taasisi zipunguze masaa ya kazi kutoka saa 40 kwa wiki hadi saa 30 kwa wiki.
 
Njia ni moja tu, ni kupunguza idadi ya watu kwa kupima upya mji wenu wa dar es salaam kama wale jamaa wa ethiopia walivyofanya. PViwanja viwe vikubwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za magorofa yasiyo mengi kwenye eneo moja. Kwa mfano, magorofa yale ya samia pale kawe, ule si ujenzi mzuri kabisa, yamejaa sana pale.
 
Ila points zako nzuri. Wawekeze kwenye usafiri wa uma. Hizo mwendokasi ziwe za kutosha, safi nzuri full ACs hadi watu waache vigari vyao vya mikopo nyumbani.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Back
Top Bottom