PENDEKEZO LA KUPUNGUZA FOLENI: iwe kama ifuatavyo:
Turekebishe muda wa kuingia kazini(Kama vile tulivyorekebisha msongamano wa abiria wakati wa siku za sikukuu kwa kuruhusu magari kusafiri saa 24,yaani usiku na mchana).
i.kampuni zinazofanya usafi barabarani(wafanye kazi usiku)
ii.Matengenezo ya barabara(Kazi ifanyike usiku).
iii.Baa zifanye kazi hadi saa 8(Hatua hii itawatuliza wanywaji wasilete foleni,kwani muda wa baa utakuwa umesogezwa mbele , na itasaidia wenye kunywa wachangie mapato,watakao kuwa wazembe kwa ulevi wachukuliwe hatua kwani wengi wanasubiri ajira).
iV.Baadhi ya Taasisi muda wa kuingia kazini uwe ni saa 3 asubuhi.
V.Baadhi ya Taasisi zipunguze masaa ya kazi kutoka saa 40 kwa wiki hadi saa 30 kwa wiki.