Silivian
Member
- Nov 13, 2022
- 64
- 103
Hiki ni kitendo rahisi sana cha kunasa hisia za mwanamke yeyote yule na kuchukua moyo wake pasipo yeye kujua.
"Mpigie simu mara kwa mara kama sehemu ya kumjulia hali tu uone kama hatajaa mwenyewe."
Hii mara nyingi huwa inafanya kazi kama mwanamke atakuwa single au yupo kwenye mahusiano yaliyotelekezwa au kususisiwa na mwanaume aliyenaye.
Unapojaribu kumpigia simu jaribu kuwa "Gentleman" kwa kuongea "Maneno" fulani hivi ya kuonyesha unajali.
Sio tu kwa wanawake, mtu yeyote anayejaliwa kwa kupigiwa simu au kutumiwa ujumbe mfupi huwa anajihisi kuthaminiwa.
Hisia za kuthaminiwa zitamfanya mwanamke aanze kukuingiza moyoni pale unapomkumbuka kwa kumpigia simu mara kwa mara pale inapobidi.
Mahusiano hujengwa kwa mawasiliano ,na mahusiano huvunjwa pia kwa mawasiliano.
Kumbuka kuwa, "anayejali huwa anakujulia hali. asiyejali huwa hana habari."
Nimekupa mfano hapo juu hata kwa rafiki yako wa jinsia yako anapokujulia hali huwa kuna ka hisia fulani hivi unakapata.
Basi hako hako ka hisia huwa atakapata mwanamke utakayeanza kumjali kwa kumpigia simu au kumtumia ujumbe mfupi wa maneno.
Wasichana wengi wamejikuta wakiingia "Hubani" kwa kuendelea kuchati au kuongea na wanaume ambao mwanzoni waliwakatalia, lakini kupitia kupigiwa simu za kujuliwa hali walijikuta wakihisi wanapendwa na kujikuta wakikabidhi mioyo yao bila choyo.
Hili zoezi ni kweli linafanya kazi kwa 90%, na ndio mzizi namba moja wa kuziteka hisia za mtu yeyote yule.
Kumpigia simu mwanamke na kumwambia maneno "Mazuri" na "Matamu" itafanya ubongo wake ufungulie kemikali ziitwazo "Dopamine" zinazotengeneza hisia za furaha.
Baada ya hapo mwanamke atakuwa anapenda kupigiwa simu au kutumiwa sms na wewe ili tu aipate hiyo furaha kwa sababu atakuwa tayari kakuzoea wewe kama mtu pekee unayempatia furaha inayoleta amani ya moyo wake.
Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app