Salaam wakuu,weekend imeshatoboka tayari! Nipo hapa Rombo View ~ Sinza nang'ata Castle Lite baridi taaratibu huku nikisubiri kongoro na ndizi mchemsho kidogo. Nipo na mwanaJF mwenzangu.
Nimefikiria njia fulani za kuacha ulevi nikaona tushare pamoja ili tupunguze risks za kiafya na kifedha pia. Zifuatazo ni aina kuu za ulevi hapa duniani (hasa Tanzania):-
1. Uasherati /Uzinzi/Umalaya/Uchepukaji
2. Kunywa pombe (beer, wine, whisky, spirit,na mengine ya huko mtaani kwako)
3. Usengenyaji/ umbea/Unafiki
4. Kuangalia mpira, kucheza bao, kamali, karata na kunywa kahawa vijiweni
5. Kutamani kisichokuwa chako na usichoweza kukipata au kukinunua.
6. Kuvuta sigara, bangi, shisha nk
7. Kula mirungi nk
Sasa basi, mambo yote haya yamekuwa yakichangia ama kumkwaza mwenzi wako (bosi wako, rafiki zako), kukupotezea muda ambao ungeweza kufanya kazi kwa bidii, kukupotezea pesa, kukudhoofisha/kukuchosha kimwili nk.
Ili uepukane na haya yote, fanya yafuatayo:-
1. Minimiza idadi ya makundi ya Whatsap, ikiwezekana yafute yote
2. Ukitoka kazini, nyooka nyumbani kama mshale
3. Epuka makundi ya walevi wa aina nilizozitaja hapo juu
4. Penda kutumia muda mwingi kukaa na familia yako
5. Jitahidi upende kujifunza au kujua vitu vipya muda wote
6.Jitahidi kuwa busy na kazi au mradi wako mwingine baada ya masaa ya kazi.Mradi unaokuingizia pesa
7. Jitahidi kuivumilia kiu inayotokana na vilevi nilivyovisema hapo juu,kwani haufi
Asanteni sana.
Karibuni Rombo View Sinza,hapa Dsm.