mimi mbona sizeeki, inategemea na immunity yako pamoja na genetic , wengine hata dozi ya malaria hatujawahi kunywa tangu utoto na hatutumii vyandarua vyenu.kuna uwezekano wa kuzuia isianzishe nyingine
jamani pombe inazeesha haraka sana!
mimi mbona sizeeki, inategemea na immunity yako pamoja na genetic , wengine hata dozi ya malaria hatujawahi kunywa tangu utoto.
huwezi kujua kwa haraka,punguza unywaji kidogo hata uwezo wa kufikiri utaongezeka kidogo
Yoshua Bin Sira: 31:25-31, 40:2025) Usijionyeshe kuwa hodari wa kunywa kileo (pombe), yaani mvinyo,Imewaangamiza wengi.26) Tanuru hujaribu kazi ya mhunzi, na mvinyo mioyo ya watu, katika ugomvi wa wenye kiburi.27) Kwa wanadamu mvinyo ni kama maji ya uzima, ukinywa kwa kiasi. Je, anao uzima gani mtu asiye na mvinyo? Nayo imeumbwa ili kuwafurahisha wanadamu.28) Mvinyo ni furaha ya moyo na changamko ya roho, ikinywewa kwa wakati wake na ya kutosha.29) Lakini kunywa mno ni uchungu wa roho, na fedheha, na ugomvi.30) Kileo humzidishia mpumbavu mitego ya kumletea hasara; hupunguza nguvu, na zaidi huleta jeraha.31) Usimkaripie jirani yako kwenye karamu ya mvinyo, wala usimdhihaki anapocheka, wala usimwambie neno la shutumu, wala usimnyenye kwa kutaka alipe deni.40:20 - Kunywa mvinyo na kuimba kunachangamsha moyo, na upendano wa rafiki hupita yote.Zaburi 104:15Na divai imfurahishe mtu moyo wake; aungaze uso wake kwa mafuta, na mkate umburudishe mtu roho yake.Mhuburi 10:19Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, na divai huyafurahisha maisha, na fedha huleta jawabu la mambo yote.1timotheo 5:23 Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.
thank you
ni pm unihubirie nijaribu kupunguza lol -- ila naona uchungu kuachaaa!!!
monday to monday. na usiniulize why, sababu mimi simo kwenye payroll.
dada Rose saa zingine bar haziepukiki,unaweza kuhitaji kitu,ushauri au biashara mtu akakwambia tukutane bar fulani,na pia kuna watu wanaenda bar kuongea,kucheza pool na siku hizi hata vikao vya harusi hufanyika bar.Nilicheka sana siku moja jamaa aliingia bar na paketi ya maziwa mabaunsa wakamtoa nje eti anaharibu biashara.soma kwa uangalifu!
unywaji pombe uliopitiliza unaweza kusababisha matatizo makubwa katika ini <liver> lako!
bora kunywa beer chache kuliko kunywa vinywaji vikali kama konyagi,brand,whiskey,
jaribu kukwepa majumuiko ya unywaji pombe
shughulika sana na majumuiko yasiyo na uhusiano na unywaji pombe
punguza siku za kunywa pombe kwa week
jitahidi kutokwenda bar kila wakati
inawezekana kujenga taifa lisilo la walevi!!!
nimefanyia kazi na inawezekana kabisa!
kila la heri!
Dawa ni kuacha kununua tu.
Chukuwa Pombe unayotumia kwa mfano kama ni Bia au Konyagi nenda nayo makaburini kaiweke juu ya Kaburi lolote lile ilale siku moja kisha kesho yake nenda huko Makaburini ulipoiweka hiyo pombe kaifunguwe na unywe basi ndio itakuwa dawa hutakunywa tena hiyo pombe inshallah.Wandugu natafuta dawa ya kuacha pombe jamani. Nisaidieni kila nikikumbuka ze pombe naamishia ofisi kaunta. Yaani ndugu nateseka sana. Halafu nikisha kunywa nahamasika sana na mchezo wa ule wakati watoto wamelala. Nifanyeje jamani?