Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Aisee Mlachake, ukiipata hiyo dawa naomba uniPM nami niijaribu.

Mi nimejaribu kuacha na nimeshindwa kabisa.

Ngoja nikazimue kwanza.




Asprin hiyo dawa ukiipata usiache kuni pm uniambie maana hili ji janga la jamii
 
Bwana Yesu alisema njooni ninyi nyote mnaoelemewa na mizigo... pia alisema njoo mnywe maji ya uzima na kila anywaye chemichemi ya uzima itabubujika daima hatakuwa tena na kiu. mwamini Bwana Yesu akuokoe na akujaze Roho Mtakatifu. Bibilia inasema tusilewe kwa mvinyo tena maana una ufisadi bali tujazwe Roho kwa maana zama hizi ni za uovu.
 
Chukuwa Pombe unayotumia kwa mfano kama ni Bia au Konyagi nenda nayo makaburini kaiweke juu ya Kaburi lolote lile ilale siku moja kisha kesho yake nenda huko Makaburini ulipoiweka hiyo pombe kaifunguwe na unywe basi ndio itakuwa dawa hutakunywa tena hiyo pombe inshallah.
mmh!..hii kali sasa!tutaacha kunywa kweli?
 
huwez kuacha ghafla kama ulikuwa unakunywa nyingi,anza kupunguza idad na kuepukana na kampani ya unywaji.cyo kaz rahs lakn ukiamua unaweza!
 
Kwa aina ya pombe unayotumia ukiweza kuwa maskini utaacha pombe, tunakuombea uwe maskini
 
Wandugu natafuta dawa ya kuacha pombe jamani. Nisaidieni kila nikikumbuka ze pombe naamishia ofisi kaunta. Yaani ndugu nateseka sana. Halafu nikisha kunywa nahamasika sana na mchezo wa ule wakati watoto wamelala. Nifanyeje jamani?

Mdororo wa uchumi ukikutembelea utaacha tu, wala huhitaji dawa ukkishiwa hata soda itakua anasa kwako!
 
We fanya hivi kesho asubuhi ukifika ofisini mfate boss ofisini kwake afu mtukane afu si atakuachisha kazi ukishaacha si utadhorora kiuchumi ukishadhorora kiuchumi si utakosa hela ya kunywa hatimae utaachakunywa
 
Ndugu zangu nisaidieni kitaalam!!! naumia kila nimwonapo ndugu yangu akiwa amelewa kupindukia kufikia kiasi cha kukokotwa na kusaidiwa kurudishwa nyumbani. Je kuna namna yoyote ya kuweza kumsaidia mtu huyu kitabibu??????
 
Ndugu zangu nisaidieni kitaalam!!! naumia kila nimwonapo ndugu yangu akiwa amelewa kupindukia kufikia kiasi cha kukokotwa na kusaidiwa kurudishwa nyumbani. Je kuna namna yoyote ya kuweza kumsaidia mtu huyu kitabibu??????
Mshauri arudi Kanisani au Msikitini..nadhani ana pepo la pombe!!
 
Ndugu zangu nisaidieni kitaalam!!! naumia kila nimwonapo ndugu yangu akiwa amelewa kupindukia kufikia kiasi cha kukokotwa na kusaidiwa kurudishwa nyumbani. Je kuna namna yoyote ya kuweza kumsaidia mtu huyu kitabibu??????

Ipo...lakini sio kwamba anapewa dawa fulani basi anaacha kunywa pombe kabisaa! Unywaji pombe kupindukia mara nyingi huwa na psychological component, utabibu utakuja katika kuaddress hiyo psychological component. Muhimbili kitengo cha maginjwa ya akili (sina maana ndugu yako ni chizi, maana watu wengi wakisikia hiki kitengo basi wanakwazika kwa kuona wanadhaniwa machizi) wanatoa huduma ya ushauri nasaha kwa watu wenye matatizo ya addiction (pombe na madawa ya kulevya), nadhani wanaweza msaidia akipata kuhudhuria hizo sessions.

Naongezea maombi pia japo kuna mtu ameshauri tayari hapo juu!
 
Anahitaji ushauri nasaha tu - Ulevi hauna dawa ya vidonge wala ya maji - Ulevi ni ugonjwa unaohusiana na msogamano wa mawazo wa namna moja au nyingine...

Kama ni rafiki yako wa karibu, jaribu kumdadisi kuhusiana na maisha yake ya:-
- kifamilia
- kikazi
- kimahusiano
- na hata kiafya

Kati ya hayo kuna moja au mawili yanayomwelemea na anaamua kuwa mlevi ili ku-conceal defeat!
 
ok kweli pombe kunawatu wanazama vimbaya sana hata kusahau nini cha kufanya
 
mimi nina tatizo la kunywa pombe kupita kiasi, nimejaribu katika vipindi kadhaa kuacha lakini inakua kwa muda mfupi tu, siipendi hali hii natamani nisinywe tena katika maisha yangu imeniharibia mambo mengi sana ktk maisha yangu mpaka nakosa amani.
 
Watafute alcoholics anonymous ni kundi la watu wanaokutana na kupeana strategy za kuacha ulevi wa kupindukia.
 
Ni uamuzi tu, mimi nina mwezi sasa nimeacha na nilikuwa mlevi kupindukia. Pombe ni mbaya sana, mimi pia mambo yangu mengi yalisimama kwasababu ya pombe. AMUA mkuu inawezekana.
 
pole sana punguza badala ya kunywa pombe kumi kunyawa tano siku nyingine 2 mdogo mdogo utaacha
 
amua tu pia badili mwenendo badala ya baa nenda kwenye nyumba za Mungu, soma sana vitabu, magazeti nk.
 
Back
Top Bottom