Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

jamani mtu ameniambia ni m-pm ili anisaidie kuhusu hili yeye ni mtaalam asa sielewi namna ya kufanya, naomba kuelekezwa.
 
Jaribu kutumia soft drink kila unapohisi kutumia pombe kama soda ,juice nk na jaribu kuwa company ambayo hawatumi pombe! inaweza ikakusaidia
 
Kwa kweli ndugu zangu EMT, HANDBOY NA PAULO mmenipa ushauri wa maana sana ambao umenifanya nione kama ndo nimeshaacha kabisa, nawashukuruni sana wakubwa na naahidi kuyatekeleza yote nliyoelezwa.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Yesu Kristo ndio pekee wakukuondoa kwenye hilo tatixo ulilonalo. Hongera kwa kutambua kama unapotea.
Profesa mmoja UDSM alipata ajari akawa ana internal breeding wakashindwa kumfanyia operation sababu anastaxia (Dawa ya kuondoa maumivu) ilikuwa haikubali sababu ya Pombe, mpaka akafariki. Hongera kwa kugundua mapema. Nakushauri umpokee Yesu awe bwana na Mwokoxi wa maisha yako.
 
  • Thanks
Reactions: len
mwanangu kiukweli kuacha pombe kabisa hilo swala hakunaga otherwise ungekua una miaka hata miwili tangia uanze, lakini cha msingi unawezapunguza sana kwa kuepuka makundi ya drinkers, invest more in doing exercise, pia punguza kiwango kama ni beer 10 anza kunywa hata 5 tu there we go.....mfano hai mimi hapa nilikosa kuvaa joho chuo coz nililala polisi coz of ulevi.......but siku hizi nimepunguza sana kwa wiki mbili natupia beer 2 tuuuu kwaajiri ya afya basi................
 
dawa ya kuacha pombe ni kinyonga,
una mchukua kinyonga unamkausha , then unamsaga , ule unga wake unaweka kwenye bia ya mtu unaetaka aache pombe ,
akinywa tu , hajikugusa tena pombe .

we have do this million times,it always work
Mkuu@paty Kinyonga hana sumu lakini mkuu?
 
haya tunasubiri majibu zaidi maana naona hajatupatia nini cha kufanya mimi nina watu wengi sana tena ndugu wananikela sana kwa unywaji wao wakupindukia ninatamani sana kupata dawa ili niwaokoe katika ndimbwi hili la ulevi
 
Unasema uongo wewe Maziwa ya nguruwe sio Dawa ya kuacha kunywa Pombe. dawa ya kuacha Pombe tafuta Mama anaye nyonyesha akutilie kwenye pombe yako maziwa yake kidogo tu utaacha kabisa kunywa Pombe fanya hivyo unipe FeedBack

Mkuu Mzizi ubishani wako umekuwa wa kienyeji zaidi. Kama Metacelfin inatibu Malaria haimaanishi kuwa Fansider haitibu. Huyu aliyesema maziwa ya nguruwe yeye anayajua hayo kama ambavyo wewe unajua maziwa ya binadamu. Ningeona ubishi wako una mashiko kama ungeniambia uliyajaribu maziwa ya nguruwe na hayakusaidia lkn sio tu kwa kuja mbio na neno MUONGO.

Kila mtu kuna anachoamini, kwa mfano mimi ningeona solution ya huyo mpwa msumbufu ni kuvunjiwa yai moja la kuku katikati ya masaburi yake na tangu hapo hatorudia tena kulewa chakari. Maoni yangu yaheshimike pia.
 
both pombe na nguruwe ni haramu ktk uislam

Huu ndio upotoshaji. Kwanza napinga vikali kuwa pombe ni haram kwa Uislamu. Soma Sura 47:15 na
Suras 83:22,25.

La pili,nguruwe si haram kwa uislamu. Kilicho haram ni kula nyama yake.
 
Huu ndio upotoshaji. Kwanza napinga vikali kuwa pombe ni haram kwa Uislamu. Soma Sura 47:15 na
Suras 83:22,25.

La pili,nguruwe si haram kwa uislamu. Kilicho haram ni kula nyama yake.
Mkuu@Mwana Mtoka Pabaya Unajuwa kile unachokisema lakini? Umetowa aya za Quran unajuwa lakini maana yake? Nakusaidia kidogo maana nimeona umetowa aya lakini hujuw i unachokisema aya uliyotowa hii hapa ( Soma Sura 47:15) 15. Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao?

Nakupa Tafsiri ya aya hiyo hii hapa:

15. Sifa ya Pepowalio ahidiwa wachamngu ni kama hivi: ndani yake imo mito ya maji yasiyo chafuka, na mito ya maziwa yasiyo haribika utamu wake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa na takataka zote. Na humo

watakuwa na kila namna ya matunda, na msamaha mkubwa kutokana na Mola wao Mlezi.
Je! Sifa za Pepo ya hawa ni kama sifa itayo kuwa ni malipo ya mwenye kudumu milele Motoni, na akanyweshwa maji yaliyo tokota ya kukata matumbo?

Aya hii tukufu inataka tuzingatie kuwa maji yaliyo vunda, yaliyo tuama, yenye kutaghayari, ni maji yenye madhara. Na Aya hii tukufu imesema hayo kabla ya kuvumbuliwa darubini za kutazamia vijidudu (Microscope) kwa makarne ya

miaka, ndipo ilipo juulikana kuwa maji yaliyo tuama yaliyo taghayari yanakuwamo ndani yake mamilioni ya vijidudu vyenye madhara ya kuwasibu watu na wanyama kwa namna mbali mbali ya magonjwa.

Na ukatowa aya nyingine hii hapa naweka.


(Suras 83:22,25)
22. Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema.
23. Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.
24. Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,
25. Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri,

Tafsiri yake ni hii hapa

22,23. Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema za Peponi, juu ya viti vya enzi, wakiziangalia neema na ukarimu alio wakirimu Mwenyezi Mungu.


24. Utaona katika nyuso zao uchangamfu na mng'aro wa neema.


25,26. Wakinyweshwa kinywaji safi kilicho hifadhiwa; kuhifadhiwa huko hakukuzidisha ila uzuri wake. Na kupata neema hizo, basi, na washindanie wanao shindana.

Haya wapi paliporuhusiwa pombe kuwa ni halali kwenye aya hizo? mbona unasema maneno ya uongo? aya zinazungumzia Watu watakao ingia Peponi watakavyoishi sio watu wa duniani. mbona unapotosha watu kwa

kusema kuwa waislam hawajaharamishwa Pombe? Unatafsiri aya za Quran kwa kutumia kichwa chako ? Wewe unafikiri Quran sawa sawa na biblia yenu yenye mikono ya watu? kasome vizuri Quran upate kuelewa

vizuri Quran inazungumza wakati tulikuwa nao yaani tunavyoishi duniani na wakati ujao yaani baada ya wewe na mimi kufa yaani jinsi watuı watakavyoishi huko peponi watakuwa wanakunywa nini na kula nini? mkuu soma qurani upate kuielewa usilete aya kwa faida yako late aya uikosoe Quran kama unaweza.

 
Ajaribu disulfiram kama ataipata ni dawa nzuri itamsaidia
 
Back
Top Bottom