Oxlade-Chamberlain
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 8,635
- 2,205
uko nako unaenda kumuua bora ukawa mlevi wa pombe kuliko wa zinaaHamia zinaa
Hamia zinaa
Jamani king'asti umeongea jamani yani umesema kweli namchukia mume wng wakati mwingie kwasababu yapombe tu anasifa nyingi nzuri tatizo pombe na zinamfanya anakuo mvivu kitandani. Akilewa hajijui hajitambui akiamka hajistukii wala yani kama kalala na dume mwenzie yani bure kabisa ila mambo mengine aaaaah yupo fresh ila pombe ananiuzi jamani alafu ndio hana mpango wa kuachaHongera sana. Pombe ina hasara zaidi mwilini kuliko faida. Na unaweza kuacha, my nephew has more than 17 years toka aache jumla jumla.
Kwanza jiaminishe kwa nini ni muhimu kuacha pombe. Focus kwenye sababu za kiimani, kiafya na kisosholojia (pombe inaharibu mahusiano jamani, mnaokunywa more than three beers a day i am sorry kuwaamvia mnadhraulika kwa wake zenu. Painful truth, unless mmeoa pampula wenzenu mkifika home mnakoromeana tu).
Challenge kubwa utapata kwa walevi wenzio wa zamani. Ukijiaminisha una sababu za kitosha then utawakabili. Hata ukishindwa ukarudi nyuma its ok, amka uanze upya na utaweza. Haifanikiwi kwa siku moja tu, jipe muda. Kila la kheri
Kwani lazima kila anywaye alewe? Nadhani pombe si mbaya bali matumizi yake.Hata vyakula kama vile sukari, mafuta wanga na vingine vingi vikizidishwa au kutumika vibaya vina madhara. Hivyo huyo jamaa asilaumu pombe bali ukosefu wake wa hekima.
sasa raha ya pombe nini kama sio kulewaKwani lazima kila anywaye alewe? Nadhani pombe si mbaya bali matumizi yake.Hata vyakula kama vile sukari, mafuta wanga na vingine vingi vikizidishwa au kutumika vibaya vina madhara. Hivyo huyo jamaa asilaumu pombe bali ukosefu wake wa hekima.
sasa raha ya pombe nini kama sio kulewa
cwezi jua raha unayo pata wewe au karaha unayo ipata maana me raha ninayo pata inanipeleka ulimwengu mwingine tofauti kabisa na kufanya nifike mahali ambapo ctegemei kufika kama cjalewa so kila m2 na anacho jivuniaUlevi ni raha au karaha! Tueleze faida uayopata ukilewa
Ulevi ni raha au karaha! Tueleze faida uayopata ukilewa
Nakupongeza kwa uamuzi wako uliouchukua wa kuomba ushauri wa kutaka kuacha kunywa POMBE! Ni watu wachache sana wanaweza kufanya kama wewe! Kwa kupitia JF unaweza ukapata members wazuri na wabaya watakaokupa ushauri wa kila aina.
Mimi binafsi nilikuwa mlevi wa kupindukia! Kila nikijaribu kuacha kunywa nilikuwa nashindwa kutokana na ushawishi wa rafiki zangu! Siku moja nikiwa naendesha gari huku nikiwa nimelewa nilipata ajari mbaya sana. Namshukuru Mungu sikufa wala kiungo cha mwili wangu kukatika. Lakini nina makovu mwilini kama kumbukumbu!
Msukumo unaoupata moyoni mwako kuwa uache pombe, hata mimi nilikuwa naupata na kupuuzia! Hebu fikiria ni pesa ngapi umepoteza kwa kunywa pombe? Ni faida gani umeipata kwa kunywa pombe? Amua mwenyewe sasa toka moyoni kuwa pombe sikutaki tena pamoja na wafuasi wako na Mungu atakusaidia. Usisubiri yakupate yaliyonipata mimi na walevi wengine.
ushauri wangu umekaa kiroho. Sijui imani yako? Ila kwa maelezo yako naona ni 'kitu cha pekee' huo unywaji wako.
Hivyo anza kutazama TV EMMANUEL na utajikuta tatizo limekutoka. Kuna wengi wanashuhudia jinsi walivyoondokana na kunywa pombe kupindukia na kuvuta sigara kupindukia. Kila la heri.
Sina ushauri rasmi nnaoweza kukupa ila nna uhakika kitendo cha kutambua kua unatakiwa kuacha ni hatua moja itakayokufikisha kuacha kabisa. Walevi wengi hawawezi kuacha pombe simply bcoz hawataki kukubali kama ulevi ni tatizo.