Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Kaa mbali na marafiki zako walevi.

Fanya ibada mara kwa mara kila siku.

Tembea na biblia/quran portable mfukoni

Mpe mshahara wako wote mke/mzazi wako akae nao hawe anakupa kidogo kidogo na kwa sababu muhimu.

Fanya mazoezi kila siku.

Kila la kheri , chagua kati ya ushauri niliokupa hapo juu ambao unaona utaweza mudu. Unaweza kuchagua zaidi ya moja.
 
Ni rahisi kuacha pombe kwa mtu yoyote kama you are just a social drinker, issue iko serious kama umeshakua alcoholic. Kama huna addiction ya alcohol jaribu kuangalia alternative activities za kufanya kwa muda ambao unautumia kunywa pombe, kwa mfano kama kila jioni unapita container ukitoka job- nenda home straight, tafuta kijibustani au kishamba uwe unalima, join kwaya kama u mkristu au timu ya mpira uwe unapitia kufanya mazoezi, tafuta kidemu ambacho hakinywi muwe mnajifungia ndani mnafanya michezo mingine, mnawatch movie na kunywa juice ya ukwaju, kama jumapili unaamkia kwenye supu-uwe unaamkia church, avoid company, etc. Its easy..

Kama umeshatumbukia kwenye alcoholism issue inakua more complex na ningeshauri utafute ushauri wa kitaalamu, hapa ukiacha ghafla unaweza kufa, unatakiwa u cut down intake ya pombe slowly na sio ghafla..ie kama ulikua unapiga bia 10, jaribu kupiga 7 leo, kesho 5, keshokutwa 4, etc. Na pia unaweza ku substitute pombe yenye high alcohol percentage kwa yenye ndogo, lets say unakunywa whisky sasa, hamia kwenye bia au kama unapiga bingwa anza kunywa kilimanjaro, etc....Its a slow process na inachukua muda.
 
kwa kweli kama we ni mnywaji sana ukiacha ghafla utapata withdrawal reactions ambazo zinaweza sababisha kifo kama mdau alivyosema hapo juu. cha muhimu ni kutafuta mtaalamu anayeweza kukuanzishia dawa ya kuacha pombe iitwayo disulfiram na nyinginezo ambazo ataona zinakufaa. pia unaweza kujiunga kwenye kundi liitwalo alcoholics anymous. hili liko international na lina saidia watu kuacha pombe (unaweza kuanza kwa kugoogle kulihusu). pia tafuta kitu mbadala wa kunywa kama vile kujifunza kitu fulani (muziki). pia epuka marafiki wanywaji kama wadau walivyosema hapo juu. BTW mi nataka kwenda kunywa saa hizi kama vipi twende zetu!?.
 
Hongera sana. Pombe ina hasara zaidi mwilini kuliko faida. Na unaweza kuacha, my nephew has more than 17 years toka aache jumla jumla.
Kwanza jiaminishe kwa nini ni muhimu kuacha pombe. Focus kwenye sababu za kiimani, kiafya na kisosholojia (pombe inaharibu mahusiano jamani, mnaokunywa more than three beers a day i am sorry kuwaamvia mnadhraulika kwa wake zenu. Painful truth, unless mmeoa pampula wenzenu mkifika home mnakoromeana tu).

Challenge kubwa utapata kwa walevi wenzio wa zamani. Ukijiaminisha una sababu za kitosha then utawakabili. Hata ukishindwa ukarudi nyuma its ok, amka uanze upya na utaweza. Haifanikiwi kwa siku moja tu, jipe muda. Kila la kheri
Jamani king'asti umeongea jamani yani umesema kweli namchukia mume wng wakati mwingie kwasababu yapombe tu anasifa nyingi nzuri tatizo pombe na zinamfanya anakuo mvivu kitandani. Akilewa hajijui hajitambui akiamka hajistukii wala yani kama kalala na dume mwenzie yani bure kabisa ila mambo mengine aaaaah yupo fresh ila pombe ananiuzi jamani alafu ndio hana mpango wa kuacha
 
Unataka kuacha pombe?Fanya hivi:
1.Jikubali kwamba wewe ni mlevi.
2.Punguza/acha taratibu
3.Kunywa asali 1 tsp siku 28.
 
Hapo namba 2.Kwani siwezi kuacha ghafla? Na vipi asali hiyo bwana wewe inahusianaje na kuacha pombo?
 
Upo msemo unaotumika kwamba ‘pombe ni noma’. Hiyo ina maana pana, ikiwemo kwamba madhara yanayotokana na kilevi hicho ni hatari kwa binadamu.

Kwa maana hiyo, njia pekee ya kuepukana na hatari hizo, ni kaucha kunywa pombe, jambo linaloaminika kuwa gumu miongoni mwa wanywaji wake.

Hilo linadhihirika pia kwa ushuhuda wa John Mathayo (36) mkazi wa Boma Ng’ombe mkoani Kilimanjaro, anayesema alifanikiwa kuacha kunywa pombe baada ya kutumbukia chooni, ikiwa ni matokeo ya kulewa `chakali’.

“Niliacha pombe baada ya kutumbukia kwenye shimo la choo, nikiwa nimelewa sijitambui,” anasema na kuongeza kuwa katika maisha yake, hatalisahau tukio hilo.

Mathayo ambaye hakubahatika kwenda shule, anasema kabla ya kuishi Boma Ng’ombe, alikuwa akiishi na wazazi wake kijiji cha Kilingi, wakijishughulisha na kibarua cha kulima mashambani.

Anasema kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 19, na kwamba aliambatana na wazazi wake walipokuwa wanakwenda kulima.

“Kwa mfano, shamba la heka moja tulikuwa tukilima watu watatu, gharama yake ilikuwa ni makubaliano kati ya mwenye shamba na baba, wakati mwingine ilikuwa ni Shilingi 20,000 au 15,000,” anasema.

Anasema baada ya kumaliza kulima na kukabidhiwa fedha, baba yake alikuwa akimpatia kiasi kidogo cha fedha alichokitumia kwa ajili ya kununua pombe.

“Baba alikuwa akinipa kati ya Shilingi 1000 na 1,500, yaani nilikuwa nikipewa fedha hizi akili yangu yote ilikuwa ikiwaza pombe tu, sio kitu kingine,” anasema na kuongeza kuwa:

“Hata ninapokuwa shambani, kuna ule muda ambao wakulima wanapumzika kwa kunywa maji na chakula, binafsi ninapotoka nyumbani nilikuwa ninahakikisha natoka na dumu dogo ambalo ndani yake kunakuwa na pombe ya kienyeji aina chang’aa au dadii,” anasema.

Anasimulia kuwa, kitendo cha kunywa pombe hizo mara kwa mara, kilimsababishia kufikia hatua akawa hachagui aina ya pombe kwa ajili ya kunywa.

Anasema wakati mwingine ilifikia hatua alikuwa analala porini kutokana na kulewa sana.

“Nakumbuka siku moja mzee mmoja alikuja nyumbani kuzungumza na baba kuhusu kumlimia shamba lake la nusu heka, kutokana na baba kuwa na kazi ya mtu mwingine, nilikubaliana na mzee huyo kumlimia kwa Shilingi. 8,000 basi nikaanza kazi,” anasimulia.

Mathayo anasema, baada ya siku mbili alikuwa amemaliza kulima hivyo alipokabidhiwa fedha alienda ‘klabuni’ sehemu wanayouza pombe za kienyeji.

“Nilianza kunywa mbege saa tisa alasiri, ilipoisha nikachanywa changaa, kwenye saa moja usiku nikaanza safari ya kurudi nyumbani, huwezi kuamini nilijikuta kwenye msitu wa West Kilimanjaro katika shimo,” anasema na kuongeza:

“Mashimo hayo yanachimbwa kwa ajili ya kutega nguruwe pori, kipindi hicho mvua ilikuwa imenyesha hivyo maji yalikuwa yamejaa kwenye shimo nililokuwa nimelala,” anasema.”

Anasema kwa bahati nzuri, shimo hilo halikuwa refu sana hivyo asubuhi alijikuta kichwa kikiwa nje (ya shimo) wakati kiwiliwili kikiwa ndani.

Anafafanua kuwa, pamoja na adha hiyo aliyoipata siku hiyo, lakini hakuacha pombe na kwamba aliongeza ulevi.

Hata hivyo, Mathayo anasema tukio jingine linalohusiana na pombe ni baada kutoka kunywa pombe akiwa njiani kuelekea nyumbani, akipita kwenye moja ya pori, alikutana na mnyama ambaye hakumjua ni wa aina gani.

“Huwezi kuamini, siku hiyo nilikimbia mwendo mrefu wakati awali nilipotoka klabuni, nilikuwa nayumba naenda mbele na kurudi nyuma, nilipofika eneo la wazi, yule mnyama alirudi nyuma na kutokomea msituni,” anasimulia.

Anasema baada ya kurudi nyumbani alimsimulia mama yake, ambaye kila siku alikuwa akimshauri aache pombe kwa kuwa zinamzeesha wakati umri wake bado mdogo.

“Mama alikuwa anakasirika sana anaponiona ninarudi nyumbani nikiwa nimelewa sijielewi, kitendo hicho kilimuuma zaidi pale ninapolala nje, baba alikuwa anakunywa ingawa hakunifikia mimi,” anasema.

Anasema akiwa na umri wa miaka 24, siku moja baada ya kufanya kazi za kila siku, akarudi nyumbani kama kawaida yake akiwa amelewa, alitumbukia kwenye shimo la choo ambalo lilikuwa limefunikwa juu kwa magogo.

Anasema mgogo hayo yalikuwa yameoza kutokana na mvua za mara kwa mara, zinazonyesha hivyo alipokanyaga lilivunjika na kuingia nalo ndani ya shimo.

Anasema shimo hilo ambalo ni mali ya mzee mmoja aliyemtaja kwa jina la Mushi, kutokana na kuwa na mchanganyiko wa maji na kinyesi, alikunywa maji hayo machafu.

“Nilikuwa nazama na kuibuka juu, nilikunywa maji bahati nzuri ilikuwa ni saa 12 jioni hivyo nilipopika kelele za kuomba msaada walijitokeza watu kunisaidia, niliokolewa nikiwa sifai, walinitapisha na kunimwagia maji,” anasema na kuongeza:

“Kutokana na kuzoeleka kijijini hapo baadhi walinisema na kunitaka niache tabia ya ulevi kwani majanga ninayokutana nayo ni moja ya mafundisho, mzee mmoja aliniambia nikiendelea na ulevi janga la mwisho ni kifo,” anasema.

Anaeleza kuwa, baada ya kupata huduma ya kwanza na kurudishwa nyumbani, siku iliyofuata hakutamani kwenda kilabuni zaidi alishinda siku nzima ndani bila kula chochote.

Mathayo anasimulia kuwa, katika hali isiyo ya kawaida alijikuta wiki nzima baada ya tukio hilo, alikaa bila kunywa pombe wala kuwa na kiu nayo.

“Huwezi amini nilikuwa nafanya kazi ndogo ndogo nyumbani kisha nalala, ulipita mwezi bila kurusha mguu kilabuni, walevi wenzangu nilikuwa nakutana nao mtaani asubuhi walikuwa wananishangaa lakini binafsi pia nilikuwa najishangaa kwa yote yaliyotokea juu yangu,” anasema.

Anasema baada ya mwaka mmoja alihamia Boma Ng’ombe kutafuta maisha ambapo huko alikuwa akijishughulisha na uchimbaji mchanga na kuuza kazi ambayo anaendelea nayo hadi sasa.

Amewahasa vijana wenzake wenye tabia kama aliyokuwa nayo awali, kuacha kwani amegundua kuwa ulevi hauna faida zaidi ya kufa.

Msomaji kama una ‘Sintasahau’ itume kupitia simu ya mkononi 0714318553 ama barua pepe; romdav1@yahuu.com. Hairuhusiwi ‘ku-beep’.










CHANZO: NIPASHE

 
Kwani lazima kila anywaye alewe? Nadhani pombe si mbaya bali matumizi yake.Hata vyakula kama vile sukari, mafuta wanga na vingine vingi vikizidishwa au kutumika vibaya vina madhara. Hivyo huyo jamaa asilaumu pombe bali ukosefu wake wa hekima.
 
Kwani lazima kila anywaye alewe? Nadhani pombe si mbaya bali matumizi yake.Hata vyakula kama vile sukari, mafuta wanga na vingine vingi vikizidishwa au kutumika vibaya vina madhara. Hivyo huyo jamaa asilaumu pombe bali ukosefu wake wa hekima.

umesema vyema mkuu.

aristotle alishawahi kuelezea virtue na kusema kila kitu ukizidisha kina madhara na ukipunguza sana kina madhara pia kiasi ndicho kinachohitajika
 
Ulevi ni raha au karaha! Tueleze faida uayopata ukilewa
cwezi jua raha unayo pata wewe au karaha unayo ipata maana me raha ninayo pata inanipeleka ulimwengu mwingine tofauti kabisa na kufanya nifike mahali ambapo ctegemei kufika kama cjalewa so kila m2 na anacho jivunia
 
kichwa chake ni kibovu tu, asisingizie pombe. Pombe ilibarikiwa tangu harusi ya Kana na Mwenyezi mungu akaiona ni njema.
 
Wadau/wakuu wa jamvi nisaidien katika hili nataman sana kuacha pombe lakini nashindwa nifanyaje? Na je kuna dawa maalum ya kutumia ambayo inaweza nsaidia?(mi ni nywaj wa kama bia 7 na kuendelea kwa siku wakat mwingine had nazima kabisa)

-------------------------
Nakupongeza kwa uamuzi wako uliouchukua wa kuomba ushauri wa kutaka kuacha kunywa POMBE! Ni watu wachache sana wanaweza kufanya kama wewe! Kwa kupitia JF unaweza ukapata members wazuri na wabaya watakaokupa ushauri wa kila aina.

Mimi binafsi nilikuwa mlevi wa kupindukia! Kila nikijaribu kuacha kunywa nilikuwa nashindwa kutokana na ushawishi wa rafiki zangu! Siku moja nikiwa naendesha gari huku nikiwa nimelewa nilipata ajari mbaya sana. Namshukuru Mungu sikufa wala kiungo cha mwili wangu kukatika. Lakini nina makovu mwilini kama kumbukumbu!

Msukumo unaoupata moyoni mwako kuwa uache pombe, hata mimi nilikuwa naupata na kupuuzia! Hebu fikiria ni pesa ngapi umepoteza kwa kunywa pombe? Ni faida gani umeipata kwa kunywa pombe? Amua mwenyewe sasa toka moyoni kuwa pombe sikutaki tena pamoja na wafuasi wako na Mungu atakusaidia. Usisubiri yakupate yaliyonipata mimi na walevi wengine.

ushauri wangu umekaa kiroho. Sijui imani yako? Ila kwa maelezo yako naona ni 'kitu cha pekee' huo unywaji wako.
Hivyo anza kutazama TV EMMANUEL na utajikuta tatizo limekutoka. Kuna wengi wanashuhudia jinsi walivyoondokana na kunywa pombe kupindukia na kuvuta sigara kupindukia. Kila la heri.

Sina ushauri rasmi nnaoweza kukupa ila nna uhakika kitendo cha kutambua kua unatakiwa kuacha ni hatua moja itakayokufikisha kuacha kabisa. Walevi wengi hawawezi kuacha pombe simply bcoz hawataki kukubali kama ulevi ni tatizo.
 
Tatizo walevi wakiambiwa kwenda kwa wataalamu wa akili wanaona wanadhalilishwa.

Lakini ukweli upo hapo, nenda kwa wataalam wa ushauri wa kuancha pombe.
Hata kama ukipewa dawa ya kuacha leo, bila kufuata ushauri waweza pata repalse baadae.
 
Back
Top Bottom