Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Wana JF mimi nimeshawahi kuwa ni mshiriki mzuri wa meditation na yoga (kwa wale waoelewa najua wanalielewa)..nimefanya hivyo kwa muda wa miaka mitatu na maisha niliyaenjoy sana enzi hizo nipo na marehemu munga tehnan kwa wanaomjua...

Ila kuna matatizo nikayapata kazini nikashindwa ku handle ile situation kama mnavyojua kuchoshwa kazi kunavyokula mind kwa hyo nikajikuta nimeingia kwny matumizi ya pombe(kitu ambacho sikuwahi kutumia mpk nimemaliza chuo unkizingatia nimesoma boys o level na A level)

Mpka leo ni miaka minne na kazi nilishapata nyingine kila nikijaribu kuacha nashindwa na ninataman sana maisha ya meditation niyarudie sababu nimegundua ndo maisha ya fur aha pekee...wadau msaada wenu.
 
Fanya utaratibu uokoke na ujiunge na jamii ya waliokoka. Yesu atakuweka huru na yote yasiyofaa na utapata raha na amani milele.
 
Fanya utaratibu uokoke na ujiunge na jamii ya waliokoka.Yesu atakuweka huru na yote yasiyofaa na utapata raha na amani milele.

Hakuna binu nyinine unayojua tofouti na hyo imani yako ya yesu.
 
acha kazi hii itapelekea kukosa hela ya kununulia pombe
 
Hakuna binu nyinine unayojua tofouti na hyo imani yako ya yesu.

Unaweza jaribu mbinu nyingine zote,endapo zikishindwa chukua hii niliyokushauri, Kwani ni suluhisho la issue zote zisizofaa na zilizoshindikana.

Wala huhitaji kuweka juhudi yoyote ili kuacha pombe na mambo mengine yasiyofaa.Ukiamua tu kuambatana na Yesu,mambo yote yanakuwa shwari kabisa. Nami nilikuwa hivyo, lakini sasa niko poa.

Lakini nasema tena jaribu njia nyingine pia, zikishindikana karibu nitakuelekeza zaidi.
 
Okoka, mpe Yesu maisha yako utashangaa kiu ya pombe itakavyotoweka. Mungu akubariki.
 
Mimi ntakuwa tofauti sana na ushaur wa watu wengine ushaur wang ni Owa mwanamke unayempenda sana sana ukimuona amekasirika sbb ya pombe utajisikia vibaya na inaweza saidia
 
dawa ya kuacha pombe ni kuikataa kutoka moyon basi...hata kuanzia sasa sema sintokunywa tenda mpaka ipite miaka 3
 
Easy sana,,wewe ni kukuwekea maziwa nguruwe mara baada ya kunywaya utapike utumbo.
 
HUo ni usaliti wa wazi ulipigwa chini kazi ikakusaidia. Umepata kazi nyengine unataka kuiacha acha uzandiki kula gambe
 
dawa ya kuacha pombe ni kuikataa kutoka moyon basi...hata kuanzia sasa sema sintokunywa tenda mpaka ipite miaka 3

This is the best advice kama unataka kuacha pombe. Nilikua mnywaji mzuri sana. Naamua naacha miezi sita, mwezi name hata wiki. Ila najikuta narudia kisa nimepatwa na majanga au nataka kunywa ili niwe karibu na mtu Fulani.

Kwasasa nimeamua tena kuacha na Leo ni siku ya 20. Sina hamu na pombe na nahisi kuichukia sana. Naomba Mungu aniweke katika hali Hui for the rest of my life.

Pombe ni pepo. MTU anaweza kukuomba 5k lakini ukamnyima lakini ukaingia bar mhudumu au rafiki akaomba bia ukanunua hata kumi.

Unakuta mtu hana hata kiatu kavaa ndala lakini yupo grocery anapiga monde.

Amua acha pombe. Ulevi ni ujinga. Kwanini MTU ufanye kitu ambacho hakina faida kwako ila ni hasara tu.

Tafakari. Chukua hatua
 
pole sana kwa hilo,hakika mpk ulipo upo ktk hatua nzuri ya tiba,kwanza umeshatambua tatizo,pili umetamani kuacha,tatu unatamani kurudia meditation ya yoga,nne umejihisi huwezi kuacha pombw
soln:fanya maamuzi yafuatayo,anza kupunguza pombe taratibi from hero to zero,pili epuka mazingira na company zinazokupeleka kwenye pombe,tatu tenga muda wa meditation ya yoga taratib hata nusu saa kwa siku huku ukiendelea kuongeza muda mpk utakapoloea kabisa hakika utatoka zero to hero upande huu huku kule ukipotezea,kuwa tiyari fanya maamuzi sasa,maisha ni mipango na kupanga ni kuchagua kila la kheri mkuu
 
Okoka, hata mimi nilikuwa nakunywa pombe hadi iliniharibia maisha lakini nilipookoka mwaka 2005 sijawahi kufikiri kama kuna kitu kinaitwa pombe hapa duniani, pia heshima yangu imerudi.
 
Kunywa kisha kaanguke njiani mtaani kwenye uchochoro alafu iwe usiku alafu utaacha pombe mwenyewe kesho yake.

Mh mjomba hiyo ni majanga sasa kwa nini niache kwa fedheha!!?alafu nipigwe picha na global....!!
 

Asante sana the don kwa ushauri wako...yani inanisumbua sana sababu kila nikiamka ni mjuto tu ya kutumia pesa zaidi na nilivyopanga,kukosana na watu ninaowaheshimu,kukosana na mwezi wangu kwa kumjibu vibaya nikiwa nimelewa pia zaidi ya yote I miss meditation!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…