Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Damn.....
Pole sana mkuu.
Mina pombeka ingawa sio kama wewe kiivyo aiseeee
Na kwa hii mida ulio weka hili bandiko kweli nashawishika kuamini kwamba tungi limekuharubu kabisa.
Maana mida hii ni usiku mnene ilipaswa uwe umelala fofofo lakini ona sasa usingizi umepata kwasababu ya stress
Ni sheedah mkuu, ni zaid ya popo
 
Ndo tatizo la vijana wa kibongo,mtu huna hata bajaji,nyumba,wala banda tu la kuku umehamishia kwe pombe! Alaf mwisho wa siku unatafuta mchawi oh nimerogwa mbona pesa hazikai! Mara lile loh.ndugu kama ulivyoanza kunywa na ndivyo uache kunywa.ukiona unashindwa tafuta mchuchu mmoja decent mwenye kujitambua na kujielewa mueleze shida yako kama utakubalika moyoni mwake mueleze tatzo lako naye atakusaidia.
 
Kunywa mkojo yako ya asubuhi kabisa,kidogo tu! Linganisha rangi ya mkojo na pombe.Then ukiiona tu mindset yako itakwambia usinywe mkojo. Ukishindwa OKOKA mojakwa moja.utakua na kiu ya Mungu zaidi.
 
Mshahara wako ukitoka nipe nikushikie. Na unipe ruhusa ya kukukong'ota mikonzi nikikubaini ulikopa pombe. Nitakufanyia hii free of charge.

Option B, njoo ulewe baa za kwetu. Siku ukivunjiwa yai wallah wabillah, hutakaa unywe pombe tena
 
Ndo tatizo la vijana wa kibongo,mtu huna hata bajaji,nyumba,wala banda tu la kuku umehamishia kwe pombe! Alaf mwisho wa siku unatafuta mchawi oh nimerogwa mbona pesa hazikai! Mara lile loh.ndugu kama ulivyoanza kunywa na ndivyo uache kunywa.ukiona unashindwa tafuta mchuchu mmoja decent mwenye kujitambua na kujielewa mueleze shida yako kama utakubalika moyoni mwake mueleze tatzo lako naye atakusaidia.
Usifikiri ni rahisi kiasi hicho. Mimi binafsi namuelewa.
 
Dogo unaweza sana ku control. Watu tumeanza kitambo na tunaenda nayo mdogomdogo. Tatizo company gani unayo na kutaka kuonyesha mbwembwe. Si unajiona handsome??? Sasa nikwambie nenda bar pke yako uwe na elf 10 tu kwa mfuko unywe bia zako 3 au 4 taratiiibu... Then muda utakuwa umeenda enda unarud hom. Hakikisha hata km bado unasikia kiu usiagize RUDI NYUMBANI. Fanya hivo walau mara 2 kwa wiki. Sasa angalia ni rafiki gan unaeweza kupeana company. Acha kutoka usiku. Acha kujiendekeza dogo. Huna pepo ni tabia ambayo unapaswa kuiacha kwa NGUVU. Dhamiria kwa nia kabisa kwa kuwa wewe ndo muhusika usianze kwa kutegemea eti watu wengine wakusaidie mf kuombewa. Kaa ndani kwako sali. Km mkristo chukua bible soma ukisikia usingizi lala. UKIAMUA UTAWEZA NA UTAZIDI KUWA HANDSOME kwa umri wako haujachelewa utapata mke na beautiful family. May God be with you
 
Wakuu naomba ku share na nyinyi hii tabia nahitaj msaada for real.

Mimi ni kijana wa miaka 27, na tabia hii ambayo sio ya kuiificha. Weekend hii nilikuwa naona mnamsema Kitwanga lakini Kuna vitwanga wengi JF na mitaani. Kilevi/beer natumia kupita maelezo. Maisha yangu yamekuwa ya kula bata viunga vya jiji la marahaba. salary yote inaishia kwenye vyupa

Nashindwa kuelewa tatizo ni nini, najaribu kuacha nashindwa. Nisipokunywa nakuwa very decent & smart young man. Lakin nikinywa tu nakuwa chakaramu.

Mbaya zaidi imenifanya nisiwe serious kabisa hata kwenye issues ambazo ni very critical. Na offisini nimeanza ku underperform.
Nimekuwa mtu wa mawazo sana Nisipokunywa. Kinachonishangaza ni kwamba mchana siwez kugusa beer. Lakini ikifika saa tatu usiku shetani ananishawishi naondoka kwangu kuelekea viwanja vya mbali. Huko
Nitapiga kamnyeso mpaka kumi za usiku nikirudi hoi. Pombe ni source of all evils trust me people.... Na mbaya zaidi inazeesha sana.

I wish to change, i wash to focus on life. I wish to have a beautiful family Lakin sijui nachomoka vipi. Naweza jizuia wiki Mbili lakini nikizipatia nafidia siku zote ambazo sijapata. This is not normal.

Maji haya ya Mzungu yamenikamata akili mpaka naona soon nitatumbuliwa jipu.
I was handsome mpaka namaliza chuo. Nilikuwa nikitembea wasupaaaa (babies) wanani admire. But currently nipo very rough hata kesho sijui nitavaa nini kwenda officin.
Sina savings, sina kiwanja, sina mchumba

Jina kubwa maendeleo zero..... Nilikuwa na aminika Lakin sasa hivi hakuna anae ni trust including my family members.
Nataka toroka kwenye hili pepo chafu. Kama Kuna sehemu ya maombi/tiba ya ki science ya uhakika please naombeni msaada. Na kama mpo young men wa type hii badilikeni kimea sio kitu kizuri.


Note. Hii excuse ya ku control it's not real. Pombe huwezi control, overtime itakuzidia tu.
unatakiwa kwenda kwenye makanisa ya wokovu, zungumza na pastor the whole story, sometimes ni evil forces destined to destroy your destiny..
After PRAYERS you will see changes, This is real!!
Paulo anasema ninachotamani kukitenda sikitendi, ila nisichotamani kukitenda ndio nakitenda, that is external forces
 
mkuu pole sana. Lakini kaa ukijua kila mtu ana majanga yake..mm nakushauri tafta mwanamke ambae hatumii hyo kitu atakurekebisha bt sio kuku achisha cz huwez acha utapunguza tuu.
 
unatakiwa kwenda kwenye makanisa ya wokovu, zungumza na pastor the whole story, sometimes ni evil forces destined to destroy your destiny..
After PRAYERS you will see changes, This is real!!
Paulo anasema ninachotamani kukitenda sikitendi, ila nisichotamani kukitenda ndio nakitenda, that is external forces
hamna kitu sipendi kama hizi strory
 
Pole kaka Kitwanga wa jf.
Lakini mie naamini kwamba kila tabia unayoweza kuianzisha unaweza ukaiacha pia. Kuna njia nyingi za kutumia.
1. Marafiki ulio nao kama ni walevi kuachana nao itakuwa suluhu na kama huwezi kuwaacha washauri muache pombe na mfokasi kwenye maendeleo. Wale ambao watachukia ushauri wako watakukimbia na utakuwa salama. Jaribu kutafuta marafiki wasiokunywa Pombe.
2. Kumcha bwana ni chanzo cha maarifa. Anza kusali kwa kumaanisha na Mungu ni mwaminifu atakuokoa toka shimoni.
3. Anza kupunguza kiasi bia moja uinywe kwa masaa hata sita hivi. Usinywe haraka haraka.
4. Kama una tabia ya kutafuta pesa zisizo halali achana nazo maana ndo zinakupa kiburi cha kutafuta pombe maana unakuwa hauna uchungu nazo.
5. Jitahidi kunywa vinywaji visivyo na kilevi kama vile Grand Malt ingawa ina radha ya kufanana na bia lakini hailevyi. Kwa ushauri zaidi soma Mithali 21:17.
Mungu akuongoze naamini utabadilika.
 
Pole sana mkuu,jaribu kuanza kujizuia kunywa katikati ya wiki,fanya mambo mengine ukitoka ofisini .Kunywa kidogo Ijumaa na jmosi .
 
Back
Top Bottom