Ni Kazi kubwa sana Binadamu kubadili tabia,
Ulevi ni tabia ya mtu na Ulevi una hasara nyingi tukubali au Tukatae.
Mfano.
kama unakunywa Bia Tatu kila siku weekends unakunywa tano ina maana unakunywa Bia 25 kwa wiki, Na nyie wa maofisini mnaknywaga windhock na Heineken that means ni Tshs. 3000 kwa bia.
Kwea mwezi ni 100 Beers at minimum kwa mfano hii 300,000 kila mwezi ungekua unanunua hisa za CRDB leo ungekua na hisa ngapi?
Ni mambo mangapi umefanya kwaajili ya ulevi yakakusabishia hasara?
Ukiajiangalia kwenye kioo huoni adhari za pombe usoni mwako?
Ni dini ipi inarhusu ulevi?
Muda unaotumia kulewa ungekua unasoma vitabu leo IQ yako ingekuwa tofauti kabisa!!!
Ni mara ngapi pombe imekupeleka kwenye mchepuko.
Ni mara ngapi unatoka Mbezi unaenda kunywa Tabata? hiyo gharama ya usafiri unaipigiaga mahesabu.
Hatua ya kwanza kuacha kunywa ni kuyawaza hayo hapo juu na mengine, ukishachukua hatua sasa naacha au napumzika jiwekee malengo.
Anza mazoezi, jioni unapotoka kibaruani fanya jogging! uchoshe mwili, ukienda kuangalia mpira bar agiza chupa yako kubwa ya maji ya kilimanjaro, au coka na maji mdodo mdogo unazoea.
Hali ni ngumu wazee, tupunguze matumizi yasiyo ya lazima