ndayilagije
JF-Expert Member
- Nov 7, 2016
- 7,491
- 8,304
[emoji125][emoji125][emoji125]We taja vizuri Pombe yup???
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji125][emoji125][emoji125]We taja vizuri Pombe yup???
Unywaji wa pombe na ulevi ni vitu virility tofauti kama vile Mbingu na Nchi*Heshima kwa walevi wote*
Hawa jamaa wana sifa zote nzuri na mbaya moja tuu ya ulevi.
1. *Wanajitoa sana*
Hawa jamaa wanatoa sana sadaka na rambirambi. Angalia hata kwenye magrupu yenu ya watsapp na fb. Utaniambia.
2. *Si mabahili*
Hawa jamaa wanajitoa sana kwa kila kitu. Na huwa hawapendi ku bargain. Yaani mwambie inahitajika 10,000 atakupa bila kuuliza ya nini?
3. *Sio waoga wa kufanya maendeleo*
Hapa angalia idadi ya walevi walio na magari na nyumba. Afu angalia waso kunywa pombe wana nini?, wamepanga au wanajenga?
4. *Wana peana mawazo kuntu wakiwa bar*
Hawa jamaa wanapo nunuliana pombe huwa wanapeana michongo ambayo asiye mnywaji wa pombe hawezi ipata.
5. *Ndoa zao zinadumu muda mrefu*
Hawashindi nyumbani muda mrefu inawafanya ndoa zao zidumu, kwakuwa hawana muda wa kukaa na kuanza kugombana na mke wake, wala kujadili upuuzi.
*Jitahidini kunywa pombe kwa maendeleo yako na ya Taifa*
*Kama si mlevi jitahidi kufuata kanuni za walevi hapo juu, najua itakuwa ngumu*
Kwakweli najivunia kuwa MLEVI
Pole sana Jombaa mimi nikiwa na 50,000 mfukoni nilikua naogopa kuingia bar. Yaani bila 100,000 siingii barPombe inatia hasara sana mkuu,mie nilikuwa natoka na laki moja na nikikutana na kampani yangu ndani ya masaa matatu kilo imeisha nilikuwa natembea na card mfukoni ilifikia mahala beer zikinoga nampa mtu kadi na password anaenda kuchukua pesa mie niko baa tunakula beer,kuna siku nilimuagiza Rafiki yangu akaenda akachota na yeye za kwake niliumia sana,kifupi tungi inahasara kubwa kuliko faida,nashukuru mungu alinisadia kupitia Rafiki yangu mmoja ambaye tulipokuwa tukitoka kazini ananigada na kunishawishi kwenda kucheza darts badala ya kwenda kwenye zile kampani za hatari mwisho wa siku nashukuru nilifanikiwa kuacha pombe.
Kaka uko sahihi na inaelekea umenielewa vyema. Kwa mfanya biashara kunywa pombe kwake kuna faida tofauti na waajiriwa. Sisi waajiriwa tunatumia kwasababu tunajua mwisho wa mwezi tutaingiza. Mfanyabiashara anakunywa akiwa na uhakika mambo yanaenda vizuri na huwezi kula mtajiMkuu ukisema pombe inatia hasara nakushangaa sana nimejenga si chin ya nyumba tatu,na biashara kibao na usafiri upo ni akil tu yako na maisha yako unategemea kunywa pombe kwa laki tatu yako ya mshahara [emoji40] [emoji40] [emoji40] [emoji40] so sad
Honey Faith naomba niseme nilikua kama wewe tena zaidi ya wewe, Nikitoka ofisini Brake ya kwanza Bar au Grocery, Mhudumu akiniona tu hakuna swali anakuja na Heineken Baridiiiiii. Weekend kuanzia ijumaa ndio naogea kabisa yaani kurudi nyumbani ni saa tisa kama sio saa kumi alfajiri.Hata kama hali ni ngumu weekend bila vi heineken sijisikii vizuri kabisa
Honey Faith naomba niseme nilikua kama wewe tena zaidi ya wewe, Nikitoka ofisini Brake ya kwanza Bar au Grocery, Mhudumu akiniona tu hakuna swali anakuja na Heineken Baridiiiiii. Weekend kuanzia ijumaa ndio naogea kabisa yaani kurudi nyumbani ni saa tisa kama sio saa kumi alfajiri.
Sometimes nikiona nimelewa sana naingia kwenye gari nalala huku gari nimefunga vioo vyote, nikiamka nimelowa mwili mzima Jasho, Najua hii ni hatari sana lakini nashukuru Mungu nipo hai na kwasasa nimejitambua
Kama kweli una uwezo wa ku control pombe na kunywa weekends kwa weekends ni jambo jema na unywaji wa aina hiyo ni burudani ya kutosha na inakuondolea stress kama zipo.
Lakini kama ndio unywaji wa daily kama mimi mpaka sometimes kazini unashindwa kwenda jua Pombe sio rafiki wa maisha yako
Unywaji wako ulivuka mipaka. Bora uliacha, lakini kwa sisi ambao tunakunywa bia 3 au mbili, wacha tujiachie
Yaan niache kunywa pombe na safari ndogo ndo izo zimetoka na mabalimi atayanywa nani?[emoji44][emoji44]
Utakubalije wakati ww sio mlevi?Huwa tunajidanganya sana eti Bar tunabadilishana mawazo yenye tija!! hili sikubaliani nalo kabisa kabisa ni utetezi wa kitetea pombe ambayo haina faida
Kwa nini maji ya Kilimanjaro na coke.Ni Kazi kubwa sana Binadamu kubadili tabia,
Ulevi ni tabia ya mtu na Ulevi una hasara nyingi tukubali au Tukatae.
Mfano.
kama unakunywa Bia Tatu kila siku weekends unakunywa tano ina maana unakunywa Bia 25 kwa wiki, Na nyie wa maofisini mnaknywaga windhock na Heineken that means ni Tshs. 3000 kwa bia.
Kwea mwezi ni 100 Beers at minimum kwa mfano hii 300,000 kila mwezi ungekua unanunua hisa za CRDB leo ungekua na hisa ngapi?
Ni mambo mangapi umefanya kwaajili ya ulevi yakakusabishia hasara?
Ukiajiangalia kwenye kioo huoni adhari za pombe usoni mwako?
Ni dini ipi inarhusu ulevi?
Muda unaotumia kulewa ungekua unasoma vitabu leo IQ yako ingekuwa tofauti kabisa!!!
Ni mara ngapi pombe imekupeleka kwenye mchepuko.
Ni mara ngapi unatoka Mbezi unaenda kunywa Tabata? hiyo gharama ya usafiri unaipigiaga mahesabu.
Hatua ya kwanza kuacha kunywa ni kuyawaza hayo hapo juu na mengine, ukishachukua hatua sasa naacha au napumzika jiwekee malengo.
Anza mazoezi, jioni unapotoka kibaruani fanya jogging! uchoshe mwili, ukienda kuangalia mpira bar agiza chupa yako kubwa ya maji ya kilimanjaro, au coka na maji mdodo mdogo unazoea.
Hali ni ngumu wazee, tupunguze matumizi yasiyo ya lazima
Yaani namalizia ya nne ndio nakutana na huu uzi, waiter leta mbili...
Ntasoma comments nyingine kesho..