Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Mie ni mnywaji wa pombe huwa napenda japo sio mara kwa mara ila nikinywa nakunywa kweli jambo linalomkera mke wangu na mama yangu nataka kuacha nashindwa kwani nikikaa wiki sijaonja naona kama mgonjwa. Hivyo kama kuna mtu anajua dawa aniambie.
Dawa ninayo, tukubaliane kuwa tafta pesa ya kret la bia unywe hadi uflot, mimi ntachonga dili na watu wa mochwari hasa mshana jr, ntampa hata 20 elf na ntakupeleka na gari kama mfu ili uchanganywe na wafu. Utakapopata ufahamu na kuamka ujikute uko ktkt ya maiti, huo mshtuko utakufanya usinywe tena
 
Hakuna dawa ya pombe ni dhamira yako mwenyewe tu ukiamua unaacha ni sawa na tabia ya wizi ukiamua tu na mtangulize Mungu hashindwi jambo.
 
... Strong minds make bold decisions, kaa na mkeo mwambie by end of the week mimi pombe baasi, na hakikisha unasimamia maamuzi hayo. Kama jambo dogo kama hilo huwezi kufanya maamuzi na kuyasimamia vipi kwa mambo mazito kama kumu
 
Pombe kuachana nayo labda 2020 Mkuu, kabla ya hapo endelea kusoma namba tu.
 
Mkuu;
Okoka!! Huwezi amini, hakuna dawa duniani bali kwa Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye hai. Ukimpokea, akawa Bwana na Mwokozi wa maisha yako. That very minute, atakubadilisha uwe huru na hiyo dhiki yako. Wenzio tunayekuambia haya, tulikuwa zaidi yako, lakini leo, tumemwona akitubadilisha. Nakushauri; Mpokee huyu Yesu Kristo
 
kuna chalii alikunywa akazima na ilikuwa kawaida yake kuzima, jamaa wakamvunjia yai, aliposhtuka akajua kafumuliwa malinda, jamaa hata baada ya kuujua ukweli hajanywa pombe tena, dawa ndo hiyo
 
Tafuta dawa inaitwa metronidazole kunywa tembe 4 nusu saa kabla hujanywa pombe,
 
Chukua kidonge kinaitwa Disulfiram changanya na pombe unywe.. Fanya hivyo siku tatu mfululizo

Then ulete mrejesho
 
Uache kunywa ili iweje??? Mtu mwenyewe unakunywa kwa wiki mara 1.
Na hiyo pombe hutaweza kuacha kamwe kwa sababu huachi kwa kutaka wewe bali mama yako na mkeo.
Acha kwa maamuzi yako sio kwa kupangiwa na mwanamke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…