Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Jamani naombeni mnishauri nimsaidiaje mume wangu aache ulevi maana ht maendeleo ye2 yanakuja taratibu sn kwsbb kipato chake anamaliza bar.
Kabla ya kutaka kumuachisha ulevi jiulize mambo yafuatayo...
1;Je ameanza ulevi kabla hamjaoana?
2;Je ameanza ulevi baada ya kuoana?
Kama jibu ni namba moja basi utakuwa ulikubaliana nae na sasa unataka kukimbia kivuli chako
Kama namba mbili ni jibu sahihi mkalishe chini umuulize kama ana matatizo kazini au mahali popote kwenye shughuli zake,kagua kama wewe na yeye mnamawasiliano ya kuridhisha maana miongoni mwa hayo kunaweza kuwa kuna tatizo,mara nyingi wengi wanapopata matatizo kazini,kwenye ndoa au mambo mengine yanayofanana na hayo hukimbilia kwenye ulevi wakidhani ni dawa kumbe wanajimaliza zaidi....
Note:
Kuacha tabia yoyote ile ni mtu mwenyewe na huwa halazimishwi au kuachishwa,unachopaswa kufanya ni kumshauri aache na sio kumlazimisha aache....
Pole na usijali hayo ni ya kawaida tu ......!!