Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Salam,

Nimeona nianze kwa kukiri udhaifu wangu kwenye pombe, kwa kweli naipenda na nimekuwa mdhaifu sana kwenye hii kitu. Naweza kusema sijafikia kiwango cha kujiita mraibu lakini it is too much. Yaani kila siku ni lazima nipate chupa zisizopungua tatu za virikuu.

Zinanimaliza kiuchumi, zinaninyima muda wa kukaa na familia, na zinaniletea mibalaa tu. Ajali za kijinga, ugomvi na mengine ya hovyo.

Kwa akili yangu naona nimeshindwa kabisa kuacha ulabu...... Kama kuna dawa waungwana tusaidiane.

Pombe, pumbavu zako pombe.
Chukia matokeo na hasara zake utajikuta umeacha
 
Hujaamua kuacha eroo.
It begins with you. Hamna jns, huez acha mara 1, unapunguza mdgmdg ndani ya mwez unaipotezea, unaeza ukawa unakunywa labda chai jion.
Fanya kwa moyo wote.
 
Mangi flani hivi unazingua babu hamna kitu mtu ukiamua huwezi acha.mm nilikuwa napenda watoto wa kike htr nilikuwa nawabadilisha sio mchezo wife akagundua hakuniambia akaanza kuwa mnyonge furaha yake ikapungua kabisa nikawa nikimuuliza hataki kuniambia ni kulia tu kuna siku akaniambia unapenda sana wanawake wa nje.aisee niliumia nikapiga chini wote yani sasa hivi Nina mwezi wa 5 sijatoka nje ya mke wangu kwa hiyo hkn kisichowezekana
 
Ukiwa huna majukumu mazito ya kimaisha.... Hakika kama ni mlevi ni vigumu kuacha.
 
Ukiwa huna majukumu mazito ya kimaisha.... Hakika kama ni mlevi ni vigumu kuacha.
Unajua kuna target za kibinadamu..... Mara nyingi zile kubwa zikishafikiwa watu tunakuwa na tabia ya ku relax. Labda niset target nyingine.
 
Kuna jamaa yangu ni mangi flan kama wewe yeye alikua anagonga kitu cha Charles Glass yaaani ilikua ikija mezani inatoa jasho anaiangalia then anasema "Dah hii kitu ni tamu aisee.." Uzuri wa huyu jamaa yangu sijawahi muona akiyumba wala ugomvi na alikua komba mzuri tu.. Ila nilikutana nae akadai amepunguza kidogo..
 
Mwambie mtu akuwekee maziwa ya nguruwe anayenyonyesha kwenye pombe utakayokunywa ukishindwa nenda kanisani kuombewa
Yani akishindwa maziwa Ya nguruwe sidhani kama ataweza njia nyingine
Maziwa ya nguruwe hayashindwi pombe...ila akirudia ataumwa vibaya sana.
 
Jamani tuacheni utani, hivi kweli nikiwaza kale ka bia kabariiiidiii kanavyoshuka kwenye koromeo, naweza kuacha kweli?!! Mangi kilaji usiache aisee!!
 
simple like that,chukua mavi ya mwendawazimu yakiwa mabichi Mix na supu ya kunguru,kunywa Mara mbili kwa siku,muda WA siku tatu,Lazima upone Mangi
 
Nami naomba msaada nikipata tu mawazo, njia pekee ya kutoa mawazo ni kunywa
 
Kwa kosa la kuitukana hutokaa uiache fanya yafuatayo
1.epuka kupita sehemu zinazouza vilevi
2.jitahidi kuwakwepa marafiki walevi
3.tafuta shughuli ya kuku keep busy all the tym
 
Salam,

Nimeona nianze kwa kukiri udhaifu wangu kwenye pombe, kwa kweli naipenda na nimekuwa mdhaifu sana kwenye hii kitu. Naweza kusema sijafikia kiwango cha kujiita mraibu lakini it is too much. Yaani kila siku ni lazima nipate chupa zisizopungua tatu za virikuu.

Zinanimaliza kiuchumi, zinaninyima muda wa kukaa na familia, na zinaniletea mibalaa tu. Ajali za kijinga, ugomvi na mengine ya hovyo.

Kwa akili yangu naona nimeshindwa kabisa kuacha ulabu...... Kama kuna dawa waungwana tusaidiane.

Pombe, pumbavu zako pombe.
kuacha pombe ni kukimbia kuripa kodi binafs sikushaur
 
Salam,

Nimeona nianze kwa kukiri udhaifu wangu kwenye pombe, kwa kweli naipenda na nimekuwa mdhaifu sana kwenye hii kitu. Naweza kusema sijafikia kiwango cha kujiita mraibu lakini it is too much. Yaani kila siku ni lazima nipate chupa zisizopungua tatu za virikuu.

Zinanimaliza kiuchumi, zinaninyima muda wa kukaa na familia, na zinaniletea mibalaa tu. Ajali za kijinga, ugomvi na mengine ya hovyo.

Kwa akili yangu naona nimeshindwa kabisa kuacha ulabu...... Kama kuna dawa waungwana tusaidiane.

Pombe, pumbavu zako pombe.
ukitaka hiki kitabu nitafute.

NA DAWA ZA KUSAIDIA KUACHA POMBE
Watu wengi wamefanikiwa kuacha pombe kwa juhudi zao wenyewe na wengine kupitia msaada wa wataalamu mbalimbali. Kuna watu wanaojiunga ili kusaidiana katika kuacha pombe. moja ya kikundi maarufu ambacho kimeenea duniani kinaitwa alcoholics anonymous (AA). Katika kikundi hiki watu wanaotaka kuacha pombe hukutana na kubadilishana uzoefu na mbinu za kuacha pombe. kuacha pombe linaweza kuwa jambo gumu hivyo inashauriwa kulifanya taratibu. Unaanza kwa kupunguza kiasi unachokunywa taratibu mpaka unafikia kuacha kabisa. Usikatishwe tamaa ukiona unarudi nyuma mara kwa mara kwani ni jambo la kawaida katika kuacha tabia au zoea lolote lile. Ukishindwa kuacha basi unaweza kupunguza kwani unywaji kiasi huwa hauna madhara isipokuwa ukiwa mjamzito au ukishauriwa na mtalaamu wa afya. Zifuatazo ni mbinu mbalimbali ambazo zinatumika kupunguza au kuacha kabisa unywaji wa pombe. 1. tafuta kinywaji mbadala wa pombe kama vile chai au kahawa.
38
2.tafuta vitu mbadala vya kufanya kwa wakati ambao unakuwa unakunywa pombe kama vile kusoma vitabu, kuangalia filamu, kushiriki katika michezo au mazoezi. 3.tumia pesa ambazo unaziokoa kutoka kwenye pombe kwa kujiburudisha kama vile kula vizuri au kununua vifaa vya nyumbani. Hii itakusaidia sana katika kuona umuhimu wa kuacha pombe. 4.jiwekee mkakati kabla ya kwenda kunywa kuhusu kiasi utakachoenda kunywa na pesa utakayotumia. Usibebe pesa zaidi ya uliyopanga kutumia. 5. tumia glasi ndogo wakati wa kunywa na tumia vinywaji vyenye nguvu ndogo. Utafiti unaonyesha watu hunywa zaidi wakitumia glasi kubwa kuliko wakitumia glasi ndogo. 6.kunywa maji kabla hujaanza kunywa pombe. na unavyokuwa unakunywa pombe hakikisha unakuwa na maji ya kunywa karibu na uyatumie mara kwa mara. 7.jaribu kuepuka vishawishi vya kunywa. Watu wengi huwa tunashawishika kunywa kwenye mazingira fulani au tukiwa na watu fulani. Unachotakiwa ni kugundua ni vishawishi vipi hukufanya unywe na uanze kuviepuka.
8.kuwa na msimamo. Watu wengi ambao hujaribu kuacha pombe hukutana na wakati mgumu wanapopata ofa toka kwa marafiki. Njia sahihi ni kukataa bila kusitasita. Kusitasita kunaweza kukufanya uteteleke katika msimamo wako. Ni vizuri ukatafuta sababu ya kukataa ofa mapema kabla hata ya
39
kukutana na ofa. Mfano, unaweza ukasema sinywi au siongezi pombe nyingine kwa sababu nataka kupunguza uzito au sababu nyingine ambayo utakuwa umeitengeneza kama ulinzi wako. 9.epuka kunywa pombe ukiwa na kiu au njaa. Hii inapunguza kiasi cha pombe ambacho kitaingia kwenye damu hivyo utapunguza madhara yake. Pia inasaidia kupunguza kasi ya mtu kuwa mraibu/teja wa pombe. 10.hakikisha ndugu na marafiki wanajua kwamba umedhamiria kuacha pombe. hii itasaidia kupata msaada kutoka kwao pia hawatakuwa wanakushawishi sana unywe. Pia hili linaweza kukusaidia kupata marafiki wapya kwani changamoto mojawapo ya kuacha pombe ni kupoteza marafiki. 11. kama unakunywa kwa kutumia glasi hakikisha kinywaji kimeisha kabisa ndo uongeze tena. Hii itakusaidia kujua ni kiasi gani cha pombe ulichotumia. Kuna watu ambao mbinu hizo hapo juu zimeshindwa kabisa kuwasaidia kuacha pombe. msaada pekee ambao hubaki kwa watu hao ni kutumia dawa. Mara nyingi watu hawa ni wale ambao wanakuwa wametawaliwa sana na pombe na hupata madhara mara waachapo. Matibabu ya watu hawa hufuata hatua tatu muhimu.
1.hatua ya kwanza ni kutibu madhara yatokanayo na kuacha pombe. tumeshaona baadhi ya dawa zitumikazo kutibu madhara yatokanayo na kuacha pombe huko juu.
40
2.hatua ya pili ni kumsaidia mtu huyu kutotumia pombe. hatua hii ndio mara nyingi hutumia dawa. Tutaona dawa hizo hivi punde. Kumbuka kwamba dawa za kumsaidia mtu kutotumia pombe ni tofauti na zile za kutibu madhara yatokanayo na kuacha pombe. 3.hatua ya tatu ni kumsaidia mtu huyu asirudie tena kunywa pombe. Kuna dawa nyingi ambazo hutumika kusaidia watu kuacha pombe. baadhi ya dawa hizo ni kama disulfiram, fluoxetine ambayo kwa kawaida ni dawa ya sonona(depression). Dawa zingine ni pamoja na ondasentron, acamprosate, setraline na topiramate. Katika dawa zote disulfiram ndio imetokea kuwa maarufu sana na ndio tutakayo izungumzia sana katika kitabu hiki. Disulfiram ni dawa ambayo mtu akiitumia halafu akatumia pombe hupata madhara ambayo yatamfanya asitumie/asitamani pombe. ni kama vile kula yamini
 


Kwa wale wanaotumia sigara,bangi na madawa ya kulevya na wanahitaji KUACHA hii ndyo dawa mujarabu kwa



⚡wanywaji wa pombe

⚡Bhangi, sigara

⚡Mirungi , ugoro

⚡Na madawa mengine ya kulevya ukitaka KUACHA



Chukua dawa inayoitwa MURDA , chukua majani yake uyaanike yakauke





Kisha chukua majani hayo na uyasokote kama sigara kisha vuta msokoto huo nusu asubui na nusu yake jioni , yaani kutwa mara mbili



Dawa hiyo utayumia kwa siku tano tuu. Hakika hutotamani walakutimia tena vilevi vyako



Na dawa hii ilivyo mujarabu ukivuta mara ya kwanza tu hapo hapo jaribu kuvuta bhangi au sigara au kunywa Hakika utaona inakukera sanaa na ni mbaya



MAJANI HAYA YANAPATIKANA KATIKA MADUKA YA DAWA ASILI,KAMA UPO DAR NENDA KKOO UTAPATA.


Kwa ushauri na tiba wasiliana nasi

0653 532036 whatsapp
tibazetutz@gmail.com
 
Back
Top Bottom