Mtazamo wa kisasa
Utafiti fulani katika baadhi ya nchi umedai kuwa vifo vinavyosababishwa na sababu zozote zile vinaweza kufikia viwango vya baina ya 16 hadi 28% kwa uchache miongoni mwa wanywaji wa wastani (vinywaji 1-2 kwa siku) ikilinganishwa na ile miongoni mwa wanaojiepusha na unywaji kabisa. Mmwandishi wa habari Roni Caryn Rabin wa New York Times anasema kwamba takwimu za utafiti huu zina makosa
Upeo wa kiasi kinachopendekezwa
Habari zaidi:
Recommended maximum intake of alcoholic beverages
Nchi mbalimbali hupendekeza kiasi tofauti cha upeo wa kunywewa . Kwa nchi nyingi kiasi cha upeo kwa wanaume ni 210g-140g kwa wiki. Kwa wanawake, kiasi ni 84g-140g kwa wiki. Nchi nyingi hupendekeza kutumiwa kwa pombe kabisa wakati ujauzito ama kunyonyesha.
Vifo vinavyohusiana na Pombe
Matumizi ya pombe kupita kiasi ni mojawapo ya sababu zinazoweza kuzuilikaambayo husababisha vifo vingi kote duniani. Utafiti mmoja unahusisha pombe na kila kifo 1 katika 25 kote duniani na kwamba 5% ya miaka wanayoishi watu na ulemavu hutokana na matumizi ya pombe.
Nchi hukusanya takwimu kuhusu wanaofariki kwa ajili ya pombe. Huku baadhi ya takwimu zikihusiana na athari za muda mfupi kama vile ajali, nyingi huhusiana na athari za muda mrefu wa kutumia pombe.
Urusi
"Matumizi ya pombe kupita kiasi nchini Urusi, hasa kmiongoni mwa wanaume, katika miaka ya hivi karibuni imesababisha zaidi ya nusu ya vifo katika umri wa miaka 15-54
Uingereza
Vifo vinavyohusiana na pombe nchini Uingereza ni huainishwa kwa kutumia Uainisho wa Kimataifa wa Magonjwa, Toleo la Kumi (ICD-10). ICD-10 hujumuisha:
- Matatizo ya akili na tabia kutokana na matumizi ya pombe - ICD-10 F10
- Kuzorota kwa mfumo wa neva kutokana na pombe - ICD-10 G31.2
- Polineuropathi ya pombe - ICD-10 G62.1
- Kadiomiopathi ya pombe - ICD-10 I42.6
- Gastriti ya Pombe - ICD-10 K29.2
- Ugonjwa wa ini wa pombe - ICD-10 K70
- Hepatitis sugu , isiyoainishwa mahali kwingine kokote - ICD-10 K73
- Fibrosi na sairosi ya ini - ICD-10 K74 (bila kujumuisha K74.5 K74.3-Sairosi ya biliari)
- Ugonjwa sugu wa kongosho kutokana na pombe - ICD-10 K86.0
- Sumu itumikayo kiajali kutokana na mkumbano na pombe - ICD-10 X45
- Sumu itumikayo na mtu binafsi kimaksudi kutokana na mkumbano na pombe - ICD-10 X65
- Sumu kutokana matumizi na kukumbana na pombe, bila kusudi wazi - Y15 ICD-10
Mashirika ya takwimu ya Uingereza yanaripoti kwamba "Kulikuwa na vifo 8,724 vinavyouhusiana na pombe katika mwaka 2007, chini zaidi kuliko 2006, lakini zaidi ya mara mbili ya 4,144 iliyorekodiwa katika mwaka 1991. Kiwango cha vifo kuhusiana na pombe kilikuwa 13.3 ya watu kwa kila watu 100,000 mwaka 2007, ikilinganishwa na idadi ya watu 100,000 6.9 kwa mwaka 1991."
Nchini Skotlandi, NHS inakisio kwamba katika mwaka 2003 kifi cha kia mtu mmoja katika 20 waliofariki inaweza kuhusishwa na pombe.
Utafiti wa 2009 uligundua kuwa watu 9,000 hufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na pombe kila mwaka, mara tatu ya idadi ya miaka 25 ya hapo awali.
Marekani
Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji Magonjwa kinaripoti kuwa, "Kutoka 2001-2005, kulikuwa na takribani vifo 79,000 kila mwaka zinazotokana na matumizi ya pombe kupita kiasi. Kwa hakika, matumizi ya pombe kupita kiasi ni ya 3 katika sababu zinazoambatana na mitindo ya kimaisha kwa kusababisha vifo kwa watu nchini Marekani kila mwaka". Utafiti mmoja wa 1993 ulikadiria vifo vya waliofariki Marekani kupitia pombe kuwa 100,000.
Vifo kwa ujumla
Utafiti uliotazamiwa wa miaka 23 wa madaktari wa kiume 12,000 Waingereza
Ufalme wa Muunganowenye umri wa miaka 48-78, waligundua kuwa vifo kwa jumla vilikuwa vya chini sana kwa makundi yaliyokunywa chini ya "vipimo" 2 (Vipimo vya Uingereza = 8 g) kwa siku zaidi ya ilivyokuwa katika makundi ya wasiokunywa pombe. Zaidi ya vipimo 2 kwa siku ilihusishwa na ongezeko la hatari ya vifo. Pombe iliwakilishwa 5% ya vifo katika sampuli ya madaktari.
Mfumo wa mishipa ya moyo
Makala kuu ya: Alcohol and cardiovascular disease
Uchambuzi-mpevu wa tafiti 34 uligundua upungufu wa hatari ya vifo kutokana na ugonjwa wa moyo kwa wanaume ambao hutumia vinywaji 2-4 kwa siku na wanawake ambao hutumia 1-2 kwa siku. Uchambuzi-mpevu wa jaribio usioratibiwa uligundua
kwamba matumizi ya pombe kwa kiasi cha wastani hupunguza kiwango cha seramu ya fibrinojeni, protini ambayo husaidia mchakato wa kugandisha na kukuza viwango vya ongezeko la ukuajib wa aina ya plasminojeni ya tishu,kimeng'enya ambayo husaidia kuyeyusha mgandamano. Kiwango cha seramu ya protini C-tendaji(CRP)ya kuvimba na kiashiria cha hatari ya CHD, ni
cha chini kwa watu ambao hunywa kiasi wastani kuliko wale wasiokunywa pombe kabisa; hivyo basi inaonyesha kuwa matumizi ya pombe kwa kiasi cha wastani inaweza kuwa na athari zinazozuia kuvimba. Mbali na matokeo yake kwa akili, pombe ina athari dhidi ya mgandamano, yenye matokeo sawa na warfarini. Zaidi ya hayo, ugonjwa wa moyo ni wa kiasi cha chini kwa wanywao kwa wastani kuliko watumiaji chai
Licha ya ushahidi wa kiepidemiolojia, baadhi ya watu wanakosoa wazo la kupendekeza pombe kuwa na faida za kiafya. Daktari katika Shirika la Afya Duniani alisema kuwa kupendekeza matumizi ya pombe wastani kwa faida za kiafya ni "ya ujinga na hatari."
Kumekuwa hakuna majaribio yaliyoratibiwa na kudhibitiwa kuonyesha faida za pombe kwa moyo . Kutokana na hatari ya kutumia vibaya, utegemezi, athari mbaya, pombe haifai kamwe kupendekezwa kwa faida za moyo. Badala yake, chakula bora, mazoezi na kama inapohitajika matumizi ya dawa ndizo tiba zinazopendekezwa kwa kutunza moyo. Imesemwa kuwa faida za kiafya za pombe ni swala la kujadiliwa na huenda lilitiliwa chumvi na wadau wa sekta ya pombe. Pombe inafaa kuchukuliwa kama dawa-lewevu ya burudani ambayo ina uwezo wa kuzua athari kali na mbaya kwa afya na haipaswi kutangazwa kwa utunzaji wa moyo.
Ugonjwa wa pembeni wa mishipa (PAD)
"Matumizi wastani ya pombe inaonekana kupunguza hatari ya PAD katika wanaume walio na afya". "Katika utafiti huu mkubwa uliohusu raia, matumizi wastani ya pombe yalionyesha uhusiano wa kupungua kuhusiana na ugonjwa wa pembeni wa mishipa miongoni mwa wanawake, waliplinganishwa na wanaume. Mkolezo wa mabaki kutokana na sigara huenda uliweza kuwa kuathiri matokeo. Miongoni mwa wasiovuta sigara, uhusiano wa kinyume ulionekana kati ya matumizi ya pombe na ugonjwa wa pembeni wa mishipa katika wanaume na wanawake."
Uzibifu wa muda (IC)
Utafiti uligundua kwamba matumizi wastani ya pombe yalikuwa na athari ya kinga dhidi ya uzibifu wa muda. Hatari ya chini zidi ilionekana katika wanaume waliotumia na vinywaji 1 hadi 2 kwa siku na kwa wanawake ambao wanaotumia kinywaji nusu hadi 1 kwa siku.
Mshtuko wa moyo na kiharusi
Unywaji pombe wa kiasi cha wastani umeonekana kuwasaidia wale ambao wamekumbwa na mshtuko wa moyo kuendelea kuishi. Hata hivyo, matumizi ya pombe kupita kiasi husababisha ongezeko la hatari ya kupata ugonjwa wa moyo. Durusu ya maandishi iligundua kuwa unywaji pombe kwa kiasi nusu ulitoa kiwango bora zidi cha ulinzi kwa moyo. Hata hivyo, walibainisha kuwa kwa sasa hapajakuwa na majaribio yaliyoratibiwa kuthibitisha ushahidi ambao unaonyesha jukumu la vipimo vidogo vya pombe kukinga kwa dhidi ya mshtuko wa moyo Hata hivyo, matumizi wastani ya pombe huhusishwa na shinikizo la damu. Pana ongezeko la hatari ya kwa hipatrigliseridemia, kadiomiopathi presha,, na
kiharusi iwapo vinywaji 3 au zaidi vya pombe vitatumiwa kwa siku.
Ikilinganishwa na kuacha pombe, unywaji wa kiasi wastani huhusishwa na ongezeko la hatari ya
kiharusi. Unywaji wa kiasi cha chini hauna faida yeyote kwa kuzuia kiharusi
Kadiomiopathi
Kiasi kikubwa cha pombe kinaweza kusababisha kadiomiopathiya pombe, inayojulikana kama " dalili za moyo wa likizo." Kadiomiopathi ya pombe hujitokeza kwa namna ambayo kimatibabu ya hufanana na kadiomiopathi iliyopanuka idiopathi,
inayoshirikisha hipartrofi ya misuli ya moyo ambayo inaweza kusababisha aina fulani ya arithmia ya moyo. Tofauti hizi zisizo za kawaida za umeme, zinazowakilisha katika EKG, mara nyingi hutofautiana kwa hali, lakini huwa kutoka mabadiliko mbalimbali ya vipindi vya muda vya PR, QRS, au QT hadi vipindi na matukio paroxsysmal ya tachycardia ventricular. Pathofisiolojia (sababu za
kuugua mwilini) ya kadiomiopathi ya pombe haijatambuliwa kikamilifu, lakini baadhi ya nadharia huelezea kuhusu ongezeko la utoaji wa epinefrini na norepinefrini, ongezeko la utendaji, au ongezeko la kiwango cha asidi huria za mafuta zisizo na plazma ya kama taratibu inayowezekana.
Magonjwa ya damu
Walevi wanaweza kuwa na upungufu wa damu kutokana na sababu kadhaa, pia wanaweza kupata thrombositopenia kutokana na athari ya sumu ya megakariositi, au kutokana na hipesplen