Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Njia za kufuata ili kuachana na unywaji wa Pombe na Ulevi uliopitiliza

Uache halaafu Serikali itoe wapi fedha za kulipa watumishi wake?
 
Dawa ya kuacha pombe ni maziwa ya mama anaenyonyesha .Unachukua glass yenye pombe, unakamulia maziwa ya maza anaenyonyesha ila usikamulie mengi, kisha unamwacha mnywaji anakunywa huo mchanganyiko, pasipo yeye kujua kua kuna maziwa yamekamuliwa kwenye pombe yake. Akishakunywa atatapika saaana na hatakaa aonje pombe maisha yake yote.
 
Nikisikia maziwa ya binadamu ukiweka kwenye beer kushnei sasa sijui kuna reaction gan
 
Heshima kwenu brothers and sisters,

Naombeni ushauri jinsi ya kuacha kunywa bia as nimejitahid nimeshindwa,,, kila nikisema leo naacha najikuta naacha kunywa ndovu nahamia castle light, nikisema tena naacha unakuta natoka kwenye castle light nahamia windhoek,, nifanye nini ili niache maana kila siku nisipopata hata bia 4 usingiz hauji najihis kama mgonjwa.. Hii inakuaje? Maana juzi b mkubwa kaja kunivisit kwangu hadi akachoka as akifungua friji hakuna cha nyanya wala bilinganya ni castle tu zimejipanga hadi nikajisikia vibaya na hapa ndo kwanza 26,,,, nimebahatika kupata ki ajira after school but daily naona mshahara hautoshi but wenzangu wanapata mshahara mdogo na hawana marupurupu yoyote lakini unawatosheleza hii inakuaje,, nifanyeje niache bia mwenzenu

Nimeamua kuwa open as hapa hatujuani lakini tunashauriana mambo muhimu na najua wengi mna njia za kuacha bia..

mambo kama haya yananifanya nifurahie uamuzi wangu wa kutokujaribu kilevi chochote duniani. Kwa hili am proud of me
 
Heshima kwenu brothers and sisters,

Naombeni ushauri jinsi ya kuacha kunywa bia as nimejitahid nimeshindwa,,, kila nikisema leo naacha najikuta naacha kunywa ndovu nahamia castle light, nikisema tena naacha unakuta natoka kwenye castle light nahamia windhoek,, nifanye nini ili niache maana kila siku nisipopata hata bia 4 usingiz hauji najihis kama mgonjwa.. Hii inakuaje? Maana juzi b mkubwa kaja kunivisit kwangu hadi akachoka as akifungua friji hakuna cha nyanya wala bilinganya ni castle tu zimejipanga hadi nikajisikia vibaya na hapa ndo kwanza 26,,,, nimebahatika kupata ki ajira after school but daily naona mshahara hautoshi but wenzangu wanapata mshahara mdogo na hawana marupurupu yoyote lakini unawatosheleza hii inakuaje,, nifanyeje niache bia mwenzenu

Nimeamua kuwa open as hapa hatujuani lakini tunashauriana mambo muhimu na najua wengi mna njia za kuacha bia..

mkuu mbona unaisalit TBL wakati wanachana tunakuitaji
 
mambo kama haya yananifanya nifurahie uamuzi wangu wa kutokujaribu kilevi chochote duniani. Kwa hili am proud of me

Daah tuko timu moja..tuna haja ya kujipongeza.
 
Jamii forum dr kuna ndugu yangu anasumbuliwa na tatizo la ulevi wa pombe je ni kitu gani afanye kuacha hiyo kitu?

UNYWAJI WA POMBE KUPITA KIASI NA KUTAWALIWA NA POMBE
Kawaida watu huanza kunywa pombe kwa kiasi kidogo tu. Baada ya muda hujikuta wanaanza kunywa kupita kiasi na mwisho hujikuta wametawaliwa na pombe. lakini ikumbukwe kuwa si watu wote wanaoanza kunywa pombe watafikia kunywa kupita kiasi au kutawaliwa na pombe. Na pia ikumbukwe kuwa sio watu wote wanaokunywa pombe kupita kiasi wanakuwa wametawaliwa na pombe. kuna mambo mengi yanachangia watu kunywa kupita kiasi au kutawaliwa na pombe. utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50 ya unywaji kupita kiasi unasababishwa na kurithi na chini ya asilimia 15 inatokana na sababu za kimazingira. Utafiti mmoja ulionyesha kwamba watoto waliozaliwa na wazazi/mzazi walevi wana uwezekano mara mbili zaidi ya kuwa walevi kuliko wale ambao wazazi wao sio walevi. Pia watoto waliozaliwa na wazazi/mzazi walevi walikuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa walevi hata kama wamelelewa na walezi wasio walevi. Inasemekana kuna aina mbili za unywaji wa kurithi. Ya kwanza ni ile ambayo haina matatizo sana. Aina hii hujionyesha zaidi mtu anapokuwa mtu mzima na anaweza asiwe mlevi akilelewa katika mazingira yafaayo. Aina hii hutokea kwa wanawake na wanaume. Aina ya pili ni ile yenye matatizo sana na huanza mapema ujanani. Ni ngumu mazingira kumbadilisha mtu aliyerithi ulevi wa aina hii.
30
Aina hii hutokea kwa wanaume tu. Pia kuna baadhi ya watu hasa wajamii ya kiasia wamerithi kutopendwa na pombe. watu kama hawa wakinywa hata pombe kidogo hupata madhara na kukosa raha ambayo watu wengine huipata watumiapo pombe. Madhara hayo hujumuisha kichefuchefu na mapigo ya moyo kwenda mbio. Watu wa namna hii huwa ni vigumu kuwa wanywaji wa kupitiliza kiasi na wengi wao hawanywi kabisa.
Sababu zingine zinazoweza wafanya watu watumie pombe sana ni pamoja na msukumo wa marafiki, matatizo ya kifamilia na kiuchumi. Pia jinsi jamii inavyoichukulia pombe nayo ina changia sana. Mfano hapa Tanzania kuna baadhi ya makabila watu wanaanza kutumia pombe tokea wadogo. Jamii hizi huchukulia unywaji wa pombe kama kitu cha kawaida tu. Watu wa kutoka jamii hizo wana hatari ya kuwa wanywaji wa kupindukia. Sababu za kisaikolojia pia zinahusika. Mfano mtu anaweza kuwa anatumia pombe ili kutoa hasira au huzuni. Mtu huyu hasira ikimuisha au huzuni ikimtoka mara baada ya kutumia pombe kuna uwezekano mkubwa wa kutumia tena pombe hata akipata hasira/huzuni kidogo. Kitendo hiki kinaweza mfanya awe mlevi wa kupindukia. sababu nyingine ni magumu ya maisha. Watu waliopitia magumu ya maisha kama vile kukosa kazi, kubakwa, kunyanyaswa utotoni na mambo kama hayo wanauwezekano mkubwa wa kuwa wanywaji kupita kiasi. Magonjwa ya akili nayo yanachangia kwa kiasi kikubwa watu kutumia pombe kupita kiasi. Magonjwa kama sonona (ugonjwa wa huzuni na kuhisi upweke) au kuchanganyikiwa (schizophrenia) yanachangia sana unywaji wa pombe.
31
wagonjwa hawa mara nyingi hutumia pombe ili kupunguza madhara ya magonjwa yao. Mfano mtu mwenye sonona anaweza akajisikia upweke umemtoka na huzuni imemtoka baada ya kutumia pombe. kitendo hiki kitamfanya awe anatumia pombe mara kwa mara. Baada yaBaada ya kuona vitu vinavyosababisha unywaji wa kupindukia hebu tuone jinsi ya kumtambua mtu mwenye tatizo la unywaji wa pombe. Kama we ni mnywaji wa pombe hebu jaribu kujibu maswali yafuatayo: 1.je umewahi kufikiria kuacha pombe? (a). ndiyo (b). hapana 2. je umewahi chukizwa na watu kukusema/kukushutumu kuhusu unywaji wako wa pombe? (a). ndiyo (b). hapana 3. je umewahi sutwa na dhamira au kujutia unywaji wako wa pombe? (a). ndiyo (b). hapana 4. je umewahi kunywa pombe asubuhi ili kutoa hangover? (a). ndiyo (b). hapana
Kama umejibu ndiyo kwa maswali mawili au zaidi hapo juu basi ujue unywaji wako wa pombe una matatizo. Ujue unakunywa
32
kupita kiasi lakini sio lazima uwe umetawaliwa na pombe. watu wenye unywaji wenye matatizo/unywaji kupita kiasi wanakuwa na dalili zifuatazo. 1. huendelea kunywa hata kama unywaji wa pombe unasababisha mtu ashindwe kutimiza majukumu yake. Majukumu hayo yanaweza kuwa ya kifamilia, kikazi au kishule/chuo. Mtu anaweza asifike kazini au anachelewa kwa sababu ya unywaji wa pombe. 2. kuendelea kutumia pombe hata katika mazingira ya hatari. Mfano mtu anaweza kutumia pombe huku akijua anatakiwa kuendesha gari au kufanya kazi inayohitaji umakini mkubwa. 3. kuendelea kutumia pombe hata kama inamletea matatizo ya kisheria. Mfano mtu anaweza kupelekwa polisi kwa sababu ya ugomvi uliosababishwa na ulevi zaidi ya mara moja lakini asiache au kupunguza kunywa. 4. kuendelea na unywaji wa pombe hata kama unakuletea matatizo katika familia na jamii kwa ujumla.
Hapa tumeona watu ambao wanakunywa kupita kiasi. Watu wengi wakitoka katika hatua ya kunywa kupita kiasi huingia hatua ya kutawaliwa na pombe (utumwa wa pombe). watu hawa ni kana kwamba hawawezi kuishi bila pombe. mtu aliye tawaliwa sana na pombe kwakweli anaweza kufa iwapo akiikosa kwa muda mrefu. Watu hawa huhitaji uangalizi wa karibu wa daktari pindi wanapotaka kuacha pombe. kuna aina kuu nne za kutawaliwa na pombe.
33
1. aina ya kwanza ni ile mtu kuwa na hamu kubwa sana ya pombe. mtu anakuwa anatamani pombe kiasi kwamba anakuwa anashindwa kufanya majukumu mengine bila kuipata. Mtu wa aina hii atafanya juu chini kuhakikisha anapata pombe. 2. aina ya pili ya kutawaliwa na pombe ni kushindwa kujizuia. Watu wa aina hii wakishaanza kunywa ni vigumu kuacha mpaka wawe wamezima au wameishiwa hela. Hii inaweza pelekea kusababisha kifo. Sababu kadri unavyokunywa sana ndio unajisahau kwamba unapitiliza kipimo. Watu wengi wa aina hii hufa kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi na kushindwa kupumua. 3. aina ya tatu ni ile hali ya pombe kutawala mwili. Hapa ni kwamba mwili wa mtu hauwezi kufanya kazi kama kawaida bila pombe. mtu akikosa pombe anakuwa kama anaumwa. Dalili ambazo humtokea mtu wa aina hii akikosa pombe ni pamoja na: kichefuchefu, kutoka jasho kwa wingi, kutetemeka na kutototulia ( kuwa na mawenge). Watu wa aina hii ndio huhitaji uangalizi wa karibu zaidi wa daktari pindi wanapotaka kuacha pombe. 4. aina ya nne ni ile hali ambayo mtu anakua sugu wa pombe. mtu wa aina hii huwa anahitaji kiasi kikubwa zaidi cha pombe ili kulewa kadri siku zinavyoenda. Baada ya kuona aina zakutawaliwa na pombe hebu sasa tuone sifa/dalili anazoonyesha mtu aliyetawaliwa na pombe.Watu wengi wamefanikiwa kuacha pombe kwa juhudi zao wenyewe na wengine kupitia msaada wa wataalamu mbalimbali. Kuna watu wanaojiunga ili kusaidiana katika kuacha pombe. moja ya kikundi maarufu ambacho kimeenea duniani kinaitwa alcoholics anonymous (AA). Katika kikundi hiki watu wanaotaka kuacha pombe hukutana na kubadilishana uzoefu na mbinu za kuacha pombe. kuacha pombe linaweza kuwa jambo gumu hivyo inashauriwa kulifanya taratibu. Unaanza kwa kupunguza kiasi unachokunywa taratibu mpaka unafikia kuacha kabisa. Usikatishwe tamaa ukiona unarudi nyuma mara kwa mara kwani ni jambo la kawaida katika kuacha tabia au zoea lolote lile. Ukishindwa kuacha basi unaweza kupunguza kwani unywaji kiasi huwa hauna madhara isipokuwa ukiwa mjamzito au ukishauriwa na mtalaamu wa afya. Zifuatazo ni mbinu mbalimbali ambazo zinatumika kupunguza au kuacha kabisa unywaji wa pombe. 1. tafuta kinywaji mbadala wa pombe kama vile chai au kahawa.
34
2.tafuta vitu mbadala vya kufanya kwa wakati ambao unakuwa unakunywa pombe kama vile kusoma vitabu, kuangalia filamu, kushiriki katika michezo au mazoezi. 3.tumia pesa ambazo unaziokoa kutoka kwenye pombe kwa kujiburudisha kama vile kula vizuri au kununua vifaa vya nyumbani. Hii itakusaidia sana katika kuona umuhimu wa kuacha pombe. 4.jiwekee mkakati kabla ya kwenda kunywa kuhusu kiasi utakachoenda kunywa na pesa utakayotumia. Usibebe pesa zaidi ya uliyopanga kutumia. 5. tumia glasi ndogo wakati wa kunywa na tumia vinywaji vyenye nguvu ndogo. Utafiti unaonyesha watu hunywa zaidi wakitumia glasi kubwa kuliko wakitumia glasi ndogo. 6.kunywa maji kabla hujaanza kunywa pombe. na unavyokuwa unakunywa pombe hakikisha unakuwa na maji ya kunywa karibu na uyatumie mara kwa mara. 7.jaribu kuepuka vishawishi vya kunywa. Watu wengi huwa tunashawishika kunywa kwenye mazingira fulani au tukiwa na watu fulani. Unachotakiwa ni kugundua ni vishawishi vipi hukufanya unywe na uanze kuviepuka.
8.kuwa na msimamo. Watu wengi ambao hujaribu kuacha pombe hukutana na wakati mgumu wanapopata ofa toka kwa marafiki. Njia sahihi ni kukataa bila kusitasita. Kusitasita kunaweza kukufanya uteteleke katika msimamo wako. Ni vizuri ukatafuta sababu ya kukataa ofa mapema kabla hata ya
35
kukutana na ofa. Mfano, unaweza ukasema sinywi au siongezi pombe nyingine kwa sababu nataka kupunguza uzito au sababu nyingine ambayo utakuwa umeitengeneza kama ulinzi wako. 9.epuka kunywa pombe ukiwa na kiu au njaa. Hii inapunguza kiasi cha pombe ambacho kitaingia kwenye damu hivyo utapunguza madhara yake. Pia inasaidia kupunguza kasi ya mtu kuwa mraibu/teja wa pombe. 10.hakikisha ndugu na marafiki wanajua kwamba umedhamiria kuacha pombe. hii itasaidia kupata msaada kutoka kwao pia hawatakuwa wanakushawishi sana unywe. Pia hili linaweza kukusaidia kupata marafiki wapya kwani changamoto mojawapo ya kuacha pombe ni kupoteza marafiki. 11. kama unakunywa kwa kutumia glasi hakikisha kinywaji kimeisha kabisa ndo uongeze tena. Hii itakusaidia kujua ni kiasi gani cha pombe ulichotumia. Kuna watu ambao mbinu hizo hapo juu zimeshindwa kabisa kuwasaidia kuacha pombe. msaada pekee ambao hubaki kwa watu hao ni kutumia dawa. Mara nyingi watu hawa ni wale ambao wanakuwa wametawaliwa sana na pombe na hupata madhara mara waachapo. Matibabu ya watu hawa hufuata hatua tatu muhimu.
1.hatua ya kwanza ni kutibu madhara yatokanayo na kuacha pombe. tumeshaona baadhi ya dawa zitumikazo kutibu madhara yatokanayo na kuacha pombe huko juu.
36
2.hatua ya pili ni kumsaidia mtu huyu kutotumia pombe. hatua hii ndio mara nyingi hutumia dawa. Tutaona dawa hizo hivi punde. Kumbuka kwamba dawa za kumsaidia mtu kutotumia pombe ni tofauti na zile za kutibu madhara yatokanayo na kuacha pombe. 3.hatua ya tatu ni kumsaidia mtu huyu asirudie tena kunywa pombe. Kuna dawa nyingi ambazo hutumika kusaidia watu kuacha pombe. baadhi ya dawa hizo ni kama disulfiram, fluoxetine ambayo kwa kawaida ni dawa ya sonona(depression). Dawa zingine ni pamoja na ondasentron, acamprosate, setraline na topiramate. Katika dawa zote disulfiram ndio imetokea kuwa maarufu sana na ndio tutakayo izungumzia sana katika kitabu hiki. Disulfiram ni dawa ambayo mtu akiitumia halafu akatumia pombe hupata madhara ambayo yatamfanya asitumie/asitamani pombe. ni kama vile kula yamini. Mtu anayetumia dawa hii huelezwa kwa undani madhara yatakayo mpata akitumia pombe. kwa kuogopa madhara mtu huyu hawezi kutumia pombe. toka mtu atumie dawa hii hatakiwi kutumia pombe hata kidogo ndani ya siku kumi na nne (wiki mbili) vinginevyo atapata madhara. Pombe hata inayopatikana kwenye vipodozi vya kupaka na mouth washes (dawa za maji za kusafisha kinywa) inaweza kusababisha madhara makubwa. Uzuri ni kwamba madhara haya hayaui na huisha yenyewe japokuwa mtu anaweza hitaji uangalizi wa mtaalamu wa afya kumpunguzia madhara ayapatayo.
37
Madhara yanayoweza mpata mtu akitumia pombe na disulfiram ni kama yafuatayo. Kuvimba uso, maumivu makali ya kichwa, kupata tabu kupumua, kichefuchefu, kutapika sana, kutoka jasho kwa wingi, kiu kali, maumivu ya kifua, moyo kwenda mbio, kushindwa kuona vizuri na kuchanganyikiwa. Watu wenye magonjwa ya moyo na magonjwa ya akili hawapaswi kutumia disulfiram kwa sababu inaweza sababisha madhara yanayoweza kuhatarisha maisha yao. Pia tuliona mwanzoni kuwa watu waliotawaliwa sana na pombe wakiacha ghafla wanaweza pata madhara yanayoweza kuhatarisha maisha yao. Watu hawa wanapaswa kutumia dawa hii kwa uangalifu wa karibu sana wa wataalamu wa afya. Pamoja na madhara ambayo mtu anaweza kuyapata atumiapo disulfiram na pombe pia disulfiram peke yake kama dawa ina madhara yake. Disulfiram inaweza kusababisha hali ya kuchoka na kujisikia kulala lala, kizunguzungu, matatizo ya tumbo, kuhisi ladha kama ya chuma mdomoni, harufu ya mwili na pumzi. Pia dawa hii ilionyesha kwamba inaweza punguza uwezo wa kufanya tendo la ndoa. Lakini pia utafiti ulionesha kwamba utumiaji wa pombe kupita kiasi unamadhara zaidi ya disulfiram katika kupunguza uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
Pia madhara kama yatokanayo na kutumia disulfiram na pombe mtu anaweza akayapata akitumia dawa nyinginezo na pombe. dawa hizo ni kama metronidazole ambayo Tanzania hujulikana zaidi kwa jina la fragyl na dawa za kisukari kama chlopropamide, tolbutamide na tolazamide.
 
Hii sredi nakomaa nayo mpaka mwisho.

Nataka kuacha but withdrawal symptoms huwa zinanitesa sana.

I can only stay a few hours without drinking.

Then I start shaking, headaches and anger spells.

The minute am sober, I drink some more.

I cant seem to stop.

Heeeelllpppp!!
 
Ni kazi sana kuacha pombe. Inabidi utumie nguvu zote. Maamuzi binafsi, msaada wakitabibu na wa kidini kama ni muamini.

Yaani ni bora ndugu yako akamatwe na simba au Osama unaweza mpigania, akikamatwa na pombe inamchakaza mbele yako na huna la kumsaidia, so sad!
 
Ushajaribu rehab?

Hii sredi nakomaa nayo mpaka mwisho.

Nataka kuacha but withdrawal symptoms huwa zinanitesa sana.

I can only stay a few hours without drinking.

Then I start shaking, headaches and anger spells.

The minute am sober, I drink some more.

I cant seem to stop.

Heeeelllpppp!!
 
Ni kazi sana kuacha pombe. Inabidi utumie nguvu zote. Maamuzi binafsi, msaada wakitabibu na wa kidini kama ni muamini.

Yaani ni bora ndugu yako akamatwe na simba au Osama unaweza mpigania, akikamatwa na pombe inamchakaza mbele yako na huna la kumsaidia, so sad!

ni kweli ndugu yangu, baba yangu aliteswa na pombe sana , tulihusunika sana bila kujua la kufanya maana hata harudi nyumbani bila kunywa kwanza, anaamkia bar bila kujali atafukuzwa kazi ambayo wanawe tulikuwa tunaitegemea, LAKINI KISUKari na BLOOD pressure ni kiboko hataki hata kusikia harufu ya pombe achilia mbali kuona chupa tu anahisi pressure na sukari vinapanda sasa kwa kweli hadhi yake katika jamii imeanza kupanda tena ! poleni sana mnaosumbuliwa na walevi!
 
Nazani hata ndugu yangu alikuwa na tatizo kama hilohilo na akashauliwa atumie maziwa ya mbuzi.

NB: HAYA MAZIWA YATAPUNGUZA UTUMIAJI WA POMBE NA SIO KUACHA KABSA

enjoy++
 
Back
Top Bottom